BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mtangazaji mkongwe ambaye ni mmiliki wa Platforms za Simulizi na Sauti ameituhumu kampuni ya Nishati ya Lake Energies (zamani lake oil) kuwa imemdhulumu malipo ya kazi aliyoifanyia kampuni hiyo na kila anapojaribu kufuatilia amekuwa akizungushwa.
Kitendo hicho kimefanya afikie hatua ya kuweka mawasiliano ya madai yakionesha akikumbushia malipo yake kwa mmoja wa watumishi wa Lake Energies.
Kupitia ukurasa wake mtandaoni ameshea screenshot ya majibizano na muhusika wa kampuni hiyo na kuandika;
“Kwenye hii kazi, tunapitia changamoto nyingi sana, ila tunaamua tu kukausha na kuyaanika ya kufurahisha pekee. Tulijitoa sana kwenye hii campaign ya Lake Energies Tanzania. Kuhudhuria press conference, kutengeneza content, kushare, kufanya promo kwenye vipindi n azote tumewekeza fedha, tukijua tunafanya kazi na watu smart malipo tutayapata tu. Ni mwezi wan ne sasa nadai jasho langu.
“Amini, nimetumia njia zote za kiungana kudai haki yangu. Njia pekee iliyobaki ni hii na nilionya kuwa nitafanya hivi, ila mlipuuza kama kawaida. Tafadhali naomba mnilipe haki yangu.”