DOKEZO Kampuni ya mabasi ya Ester ichunguzwe

DOKEZO Kampuni ya mabasi ya Ester ichunguzwe

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Tafuta pesa ndugu. Kuna Takukuru na TRA watachunguza.
Kitendo cha kusema, jamaa kaagiza mabasi 100 anatakiwa achunguzwe tayari huo ni wivu.
Tafuta hela, uishi maisha mazuri. Hapa duniani kila kitu kinawezekana tatizo ni wewe tu.
Umenena yaan kumbe tusisahau kupambana pia tujiandae kuwa wauaji
 
Kama niya mkopo. Bongo mtu asifanikiwe utasikia vimaneno vya kijinga jinga achunguzwe akisha chunguzwa unapata nni
Kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake mkuu ilo likae akilini
 
Huu sio uwanja wa matusi, hata ukiongea kistaarabu utaeleweka tu ilmradi unaongea facts.
Unaongea Kama Dem wa kimakonde kwenye mchiriku....jirekebishe dogo.

Tukimsema kipara ndio unagundua ni matusi au sio
 
Wenye mawazo ya kimasikini ni wote ambao wana roho ya ubinafsi. Maana Tangu kuwapo kwa Tawala mbalimbali za Binadamu duniani na historia inashuhudia kwamba hakuna mtu aliyejifanikisha mwenyewe na familia na watu wa karibu asiishie kupotea. Na hiyo iwe kwa halali ama kwa Dhuluma ama ufisadi.

Sasa kama ukitafuta pesa za halali ukawa mbinafsi Mwenyez Mungu anakuumbua sembuse za wavuja jasho.. Hahahhaha.. Aya Time shall Decide.

Endelea na hayo maombi yako sasa si ungefungua kanisa mzee
 
Kuna kampuni moja ya magari mabasi itwayo Ester tunaiomba serikali iichunguze kuhusu Kodi na utajiri wa ghafla leo inasemekana kashusha mabasi zaidi ya Mia mbili kutoka China je, Kodi ya bandarini imelipwa halali?
Duh! Gari 200!?
Kama ni kweli, SGR itasubiri sana kuanza kufanya kazi.
Wao sio wajinga.
 
Kuna kampuni moja ya magari mabasi itwayo Ester tunaiomba serikali iichunguze kuhusu Kodi na utajiri wa ghafla leo inasemekana kashusha mabasi zaidi ya Mia mbili kutoka China je, Kodi ya bandarini imelipwa halali?
Kama anawekeza ndani nakupatia ajira vijana siyo mbaya kuliko kwenda kuficha hela nnje ikiwezekana alete mengine miatano
 
Kuna kampuni moja ya magari mabasi itwayo Ester tunaiomba serikali iichunguze kuhusu Kodi na utajiri wa ghafla leo inasemekana kashusha mabasi zaidi ya Mia mbili kutoka China je, Kodi ya bandarini imelipwa halali?
Ndio zile bilioni zilizoongezeka kutoka Bilioni 37 hadi Bilioni 89, ndio mgao unatembea kwa ajili ya kutakatisha pesa
 
Hata ukijua utafanya nini? Wewe mwenyewe unajifanya msafi, ukipewa cheo utaiba tu.
Hapo ulipo ushawahi kuwadhulumu watu wangapi? Utakuta kuna mtu ushawahi kumkopa hela au kumfanyisha kazi na hautaki kumlipa mpk sasa.
Kweli tuna safari ndefu, sawa Mkuu wacha tuendelee kuibiwa
 
Na chawa zake zinaropoka huku pembeni tafuta hela. Sawa. Wacha tutafute za halali nyie ogeeni hizo za wanyonge.
Kweli kupiga hatua za Kimaendeleo kwa Nchi itakuwa vigumu mno kwa style hii.

Viongozi wanatuibia alafu wamewajaza Chawa wao kuweza kuwatetea kila uchwao humu.
 
Kweli tuna safari ndefu, sawa Mkuu wacha tuendelee kuibiwa
Wazazi wa Ben Saanane wamefanya nini?
Tundu Lissu amefanya nini baada ya kupigwa risasi?
Tafuta hela ili uishi maisha mazuri na familia yako.
Mahakama ya mafisadi na Takukuru imeshindwa, wewe km mtanzania ambaye ni wa kawaida ambaye hauna hata cheo utafanya nini?
*Tanzania tunasafari ndefu sana ya kufikia mafanikio kama hatutakuwa na katiba nzuri ambayo
  • Hazitawapa nguvu viongozi
  • Kuwaondolea viongozi kinga ya kutoshitakiwa. Viongozi wataanza kushitakiwa km watafanya ubadhirifu wowote wa mali za umma
  • Polisi, mahakama, Takukuru na tume ya uchaguzi kujitegemea.
  • Tafuta hela mkuu
 
Back
Top Bottom