Kampuni ya Marekani kununua korosho zote zilizobanguliwa Tanzania

Kampuni ya Marekani kununua korosho zote zilizobanguliwa Tanzania

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Ubalozi wa Marekani hapa nchini umetangaza kuwa Kampuni ya Kimarekani, Ward Holdings Intl. itanunua korosho zote zilizobanguliwa Tanzania kwa bei ya juu ya soko

Ubalozi huo umesema taarifa hiyo ni kubwa kwa Wakulima wa Korosho nchini na ni faida kwa Tanzania na Walaji wa Korosho nchini Marekani

Nani aliipigania dili hili, isije kuwa kama lile la Palamagamba Kabudi.

Toka Maktaba :
Mfanyabiashara atua na Ndege Binafsi Kununua Korosho za JPM
Muungwana Tv37,781 views30 Jan 2019
Bodi ya Nafaka na mazao imetia saini na Kampuni ya Indo Power Solution ya kwa ajili ya Ununuzi wa Korosho Tani laki moja ambapo viongozi mbalimbali wameshuhudia mkataba huo akiwemo Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba Kabudi ,Waziri wa Viwanda na biashara, Joseph Kakunda na Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa mkoani Arusha.
30 January 2019

Bodi ya Nafaka na mazao imetia saini na Kampuni ya Indo Power Solution ya kwa ajili ya Ununuzi wa Korosho Tani laki moja ambapo viongozi mbalimbali wameshuhudia mkataba huo akiwemo Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba Kabudi ,Waziri wa Viwanda na biashara, Joseph Kakunda na Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa mkoani Arusha

Toka maktaba :
16 May 2019
Profesa Kabudi, Ahusiki na Mkataba wa Kampuni ya Indo Power Solution - Kakunda
Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda,ameeleza kusikitishwa na kukanusha lawama dhidi ya Profesa Paramaganda Kabudi,kuwa alihusika na mkataba wa ununuzi wa korosho tani 100,000 ulioingiwa na Kampuni ya Indo Power Solution ya Kenya,iliyoshindwa kulipa fedha za korosho hizo.

Tunaamini baada ya dili lile la kuuza korosho Kenya kushindwa, hili kutokana na uzoefu litafanikiwa na kuwanufaisha wakulima , sekta ya korosho na taifa kwa ujumla
Firm secured to buy all processed cashewnuts in Tanzania
6 hours ago — Tanzania Cashew nut Board. Ward Holdings Tanzania Ltd (WHT) president Godfrey Simbeye said the company was keen to develop

Nasikia sauti inayotambulika ya mwandishi mmoja msomi wa ngazi ya PhD

  • Who We Are​

WHI-Team-and-TCPA-Mbrs-REVISED.jpeg

As a market-maker, Ward Holdings International, a US based capital partner firm, utilizes the vast global expertise of its partner group to actualize great ideas to assist in the formation of strategic partnerships with governmental entities, as well as private sector businesses, to create profitable and sustainable businesses that strengthens a country’s treasury, infrastructure, builds an economy that provides jobs for its people and improves the human conditions for all.​

“Tanzania – The Soul of A New Africa”​

Ward Holdings International, LLC (WHI) recognized the numerous opportunities to learn more about the beautiful country of Tanzania and its people during a visit by WHI executives, who immediately established Ward Holdings Tanzania Limited (WHT) in January 2020.

Since then, the WHI and WHT teams have been intrigued and captivated by the annual premium Tanzania cashew nuts harvest and the existing opportunities to assist in the transformation and industrialization of the cashew nut sub-sector in the bountiful agricultural economy. We have developed numerous relationships with various Tanzanian stakeholders, including the farmers, processors, private business owners, entrepreneurs and government officials, to better understand its people and the communities where we are establishing partnerships.
“Tanzania – The Soul of A New Africa” tells the story of why WHI and WHT believe that 2020 began and will continue the decade of significant progress for all things Africa and specifically, Tanzania!

Source: “Tanzania – The Soul of A New Africa”
 
Kwa nini tujifunge kwa soko moja tuu? Wakulima na wafanya biashara ya korosho wapewe fursa ya kuchagua wateja siyo kulazimishwa kuwauzia Ward Holdings tuu hata kama kuna mteja mwingine yuko tayari kulipa zaidi. Kama wahindi wanakuja na bei zaidi wauziwe, kama Ward Holdings wanakuja na bei zaidi wauziwe. Kujifunga kwa mteja mmoja ni kukosa.
 
Hilo la kujifunga kwenye soko moja umelitoa wapi tena? Wenyewe wamesema wanauwezo wa kununua korosho yote kwa bei ambayo ni juu ya soko. Hawajazuia mwingine kununua,kama anaweza.
 
Dah! Huyo mwamba hapo kulia nyuma ya mzungu basi nkajua Hamza wakuu
 
Mwezi uliopita China walitangaza kununua korosho za Tz, mwezi mmoja mbele Marekani anasema atanunua kwa bei kubwa kuliko zote, kuna nini kinaendelea?
 
Hilo la kujifunga kwenye soko moja umelitoa wapi tena? Wenyewe wamesema wanauwezo wa kununua korosho yote kwa bei ambayo ni juu ya soko. Hawajazuia mwingine kununua,kama anaweza.
Bosi mimi naenda na nilichokisoma tuu siyo kingine. Kama wataruhusu wateja wengine itakuwa ni poa. Lakini kwa jinsi hilo tangazo lilivyoandikwa hapo twitter ni kama wao watanunua korosho zote. Sasa wakinunua zote wengine tutawauzia nini? Kwa nini wasiseme watanunua korosho kwa bei ya juu ya soko tuu sasa? Kwa nini waliongeza hilo neno "zote"?
 
Mwezi uliopita China walitangaza kununua korosho za Tz, mwezi mmoja mbele Marekani anasema atanunua kwa bei kubwa kuliko zote, kuna nini kinaendelea?
Jibu ni kwamba sasa Rais Samia ameiweka rasmi Tanzania kwenye ramani ya Dunia. Ni muda uchumi wa Tanzania unaenda kukua kwa kiwango cha juu kabisa kupitia haya marekebisho anayoenda kuyafanya Rais Samia.

Ni wakati Wizara ya Kilimo na Wizara za fedha zikajipanga ipasavyo kutumia fursa hii adhimu.
 
Ni kweli huyu mama yupo vizuri kwenye baadhi ya maeneo. Bado kwenye madini atuletee makampuni ya ulaya na Marekani waje kuchimba.
 
Back
Top Bottom