Kampuni ya Marekani kununua korosho zote zilizobanguliwa Tanzania

China imetoa pesa gani Tzn hii? Miaka yote akina Marekani ndio wako top
China kuwa soko la mazao ya biashara inajenga ushawishi mkubwa kuliko pesa za misaada. Ni nadharia tu kuwa huenda hili soko la Marekani limepatikana ili kumkata moto mchina sababu kikawaida Soko la Marekani huwa lina masharti chungu nzima.
 
Je, ni zoezi la kudumu ama ndiyo leo wakulima wanacheka, kesho wanarudi palepale? Na vipi kuhusu bei? Bei ya juu isijekuwa ya JUU
 
Hilo la kujifunga kwenye soko moja umelitoa wapi tena? Wenyewe wamesema wanauwezo wa kununua korosho yote kwa bei ambayo ni juu ya soko. Hawajazuia mwingine kununua,kama anaweza.

Tatizo watu wengine huwa wanasoma only headings
 
Taratibu tutamuelewa mama binafsi nampa mda tu lakini anaweza kuwa ndio raisi atayefanya makubwa kwenye uchumi, hayo mengine sitaki zungumzia.

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
 
Hili ndio huwa linaniuma sana,kwanini mpaka nchi ya mbali,US,au UK ndio inunue korosho zetu?wao wanaziuza wapi?au je hata kama wanazitumia kama malighafi,kwanini na sie tusiwe na viwanda tufanye hivyo
 
15,000 kwa kilo 1
Ngoja nikazinunue kwa 5000,per kg nizifiche store then wamarekani wakianza kununua mie nipate faida ya 10k kwa kilo.

Hii ni fursa ya kupata utajiri hao konde na chinga wamezubaa sana 😆
 
Hii ni habari kubwa kwa wakulima wa korosho Tanzania. Kampuni ya Kimarekani, Ward Holdings Intl. imetangaza kununua korosho zote zilizobanguliwa Tanzania kwa bei ya juu ya ile ya soko. Hii ni faida kwa wakulima wa Tanzania na walaji wa Marekani.

Chanzo Ubalozi wa Marekani.
 
Korosho, Kahawa, Mbaazi, Ufuta, Parachichi, Katani ni hot cakes ila huwa vinarudishwa nyuma na siasa za kisenge
 
Waweke wazi kilo moja watanunua kwa Bei gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…