Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO), Anslem Namala amesema meli ya New MV Victoria inaendelea na maboresho na kwamba hivi karibuni wanatarajiwa kutoa tamko juu ya chombo hicho cha usafiri kurejea kwenye ratiba zake kama kawaida.
Ameeleza kuwa tamko rasmi linatarajiwa kutolewa muda wowote kuanzia leo Mei 12, 2025.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kuhoju juu ya ukimya wa mchakato wa maboresho ya Meli hiyo, kusoma zaidi bofya hapa ~ Miezi miwili imepita bado meli ya Mv-Victoria haifanyi kazi, wananchi tuelezwe nini kinaendelea