Kampuni ya mikopo ya OYA itakuwa na mwisho mbaya sana kama ilivyokuwa kampuni ya udalali ya MAJEMBE

Kampuni ya mikopo ya OYA itakuwa na mwisho mbaya sana kama ilivyokuwa kampuni ya udalali ya MAJEMBE

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Utu ni jambo muhimu sana kwenye huu uumbaji wa Mwenyezi Mungu

Kampuni ya mikopo midogomidogo ya OYA si kampuni rafiki na yenye UTU kwa wakopaji wake. Pamoja na kuwa na vibali halali vya kuendesha hiyo biashara lakini matendo ya wafanyakazi wake kwa wakopaji wanaoshindwa kurejesha kwa wakati yanatia shaka nia ya kuwasaidia watu.

Kuna ukatili mkubwa unyanyasaji, uonevu nk kwa wateja wao. Kwa kifupi wanaogopeka kuliko polisi.. Mbaya zaidi pesa zao ni kama zina laana hazilipiki ukikopa.

Nyakati za Kikwete iliibuka kampuni ya udalali ya MAJEMBE halafu ikapata kazi za serikali za kukamata wadaiwa na wrong parking.. Hakuna rangi wananchi wenye ishu za kikodi na wrong parking walipokutana na wafanyakazi wa MAJEMBE.

Mimi ni mhanga wao.. Walikamata gari yangu wakati kesi iko TRA 2014.. Gari ilikuja kupigwa mnada mwaka 2021 Majembe ikiwa tayari ni Marehemu kwenye biashara.

Nini kiliwapata?

Walikamata gari ndogo ya Professor wa chuo kikuu UDSM maeneo ya Magomeni wakidai alipoegesha ni wrong parking.. Prof akawaomba wamuoneshe alama inayoonesha NO PARKING lakini wakaleta ubabe na kuivuta gari mpaka kwenye maegesho yao mpaka prof alipe faini.

Prof. Akakimbilia mahakamani.. Majembe wakiwa wamepewa kazi ya wrong parking na manispaa ya Kinondoni wakati huo na wenye nguvu serikalini wakaisumbua sana mahakama. Prof. Akawa ana 'document' kila gharama anayotumia kwa kukosa kutumia gari yake.

Mwisho wa siku Gharama zikawa ni zaidi ya BILLION MOJA na utawala wa JK ukawa umefikia mwisho.. Hapo nyuma Prof alishashinda kesi maranyingi tu lakini kulipwa ilikuwa shughuli pevu. Baada ya Magufuli kuingia tu jumba jeupe.. Prof akarudi mahakamani kukazia hukumu.

Majembe sasa wakiwa hawana mbeleko tena.. Wakaamriwa walipe maramoja na wakishindwa mali zao zikamatwe zipigwe mnada.. Walipewa siku 14 kisha wakaongezewa saba jumla siku 21.

Muda ukaisha bila kulipa hata thumni.. Mali zao zikakamatwa na kupigwa mnada.. Mojawapo ilikuwa godown kubwa kona ya kwenda Cocacola pale Mwenge.

Soma Pia:
Prof. Akajikusanyia mabilioni na ndio ukawa mwisho wa MAJEMBE AUCTION MART WAZEE WA KAZI! Wafanyakazi wa OYA wanatuhumiwa kuuwa mtu kwenye kudai marejesho. Mahakama zenyewe huwa hazifungi wadaiwa. OYA keshajitia gundu. Ndugu wa marehemu wakipata mawakili wazuri OYA Inaenda Kufilisiwa. Na hata kama kesi hii watachomoa lakini mwisho wao hauko mbali.

20241009_171726.jpg
 
Hii notice inawaruka wale jamaa walioua, kujitetea kwao kutakuwa kugumu sana. Jela inawanyemelea. Wameleta sifa za kijinga zimewatokea puani. Marehemu kaokoa watu wengi sana, kuanzia Sasa OYA wataogopa kwenda majumbani. Uswahilini watu wana hasira sana, wanaweza kuchoma hata vi IST vyao.
 
Dawa ya deni ambalo ni halali ni kulipa.

MWANAMKE MSHENZI SANA.
 
Kaka sidhani kama wafanyakazi wa Oya wanafanya ukatili huu bila ya baraka za top management. Kumbuka kuna kesi/majalada mengi ya malalamiko yameshafunguliwa sehemu mbalimbali ( Dar na pwani) kuhusu kampuni hii. All in all kama hii ndio management culture yao basi naunga mkono hoja.
 
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kaloleni kilichopo Kata ya Janga, Ahmed Kilindo amesema kampuni ya OYA Microcredit imetoa mchango wa shilingi milioni moja (Tsh.1,000,000/=) kwa familia ya Juma Said Mfaume ambaye alifariki baada ya kupigwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo walioenda kudai sehemu ya mkopo waliomkopesha mke wa Juma.

Kilindo amesema kampuni hiyo imetoa fedha hizo kama sehemu ya pole kwa familia huku akieleza kuwa uongozi wa kampuni hiyo umesikitishwa na kitendo kilichofanywa na wafanyakazi wake kwani ni kinyume cha miiko na maadili ya kazi yao.

Kilindo ameeleza hayo wakati akitoa salamu za uongozi wa eneo hilo kwa familia ya Juma.

Aidha Juma amezikwa katika Makaburi ya Mtongani kwa Domo yaliyopo Mlandizi.
20241010_105005.jpg
 
Back
Top Bottom