Kampuni ya mikopo ya OYA itakuwa na mwisho mbaya sana kama ilivyokuwa kampuni ya udalali ya MAJEMBE

hawa ndugu zake Januari kwakweli wamezidi yaani kila kona mitandaoni nawaona wao tu hivi wananini? janjajanja nyingi hawa , ila ukiona watu wanahangaika sana mikopo ujue hali mbaya kuna jinsi serikali inatakiwa ijitathmini kila kona ukipita kausha damu sijui kumekuaje huko Bongo.
 

Majembe walijaa wapigaji wa mali za watu wanadaiwa, hasa minada ya nyumba kupitia benki. Nategemea waliovuna wasipopanda wanaona hasara yake
 
Niko tofauti na wengi, ni kweli kuua mtu kwa deni la 300k, ni kosa kubwa.
Lakini tusipuuze umuhimu wa hii tasasisi kwa wafanya baishara wengine wengi, wanao nufaika na mikopo toka kwao.

Kukopesha mtu ni rahisi sana, na kurudisha marejesho/mikopo ni jambo gumu mno;
-Wanachama wa uvccm ni wadaiwa sugu toka DCB Commercial Bank mpaka leo
-Kuna makanisa yalianzisha banki zao, tayari hizo banki ni marehemu.
-Kuna bank zimevunja uhusiano wa kibiashara kutokana na wafanyakazi kutolipa mikopo yao
-Kuna wasomi walikopeshwa pesa wasome elimu ya juu, leo wangapi wamelipa?

Mbali ya OYA,
Kuna hizi "kausha damu" au "chupi mkononi".
je mnajua ni mangapi wakopaji wanapitia? Ni mwendo wa stress na kuzikimbia nyumba zao.

au basi tuseme ni watu wangapi leo wanaweza kukopa pesa bank za NMB, CRDB, DTB, EXIM, nk?

https://www.dcb.co.tz/

 
Sometimes we need to lend a voice to those who cannot speak

R I P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…