Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Noble Helium imetangaza kuchagua maeneo matatu ya kwanza kwa uchimbaji katika Mradi wa North Rukwa ikiwa ni hatua muhimu katika kuchunguza uwepo wa gesi kwenye maeneo yenye kina kifupi.
Maeneo haya yaliyochaguliwa ni sehemu ya maeneo 10 ambayo yanaonekana kuwa na potential ya uwepo wa gesi.
Kufikia sasa maandalizi ya kusafirisha vifaa vya uchimbaji yameanza, na vifaa muhimu tayari vimewasili nchini Tanzania vifaa hivyo vinatarajiwa kufika maeneo maalum ya uchimbaji wiki ijayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Noble Helium, Shaun Scott, alibainisha kuwa maeneo haya matatu yamechaguliwa kwa uangalifu kutoka kwenye maeneo 10 ya awali yaliyochaguliwa.
Uchimbaji wa kwanza utaanza katika eneo la Mbelele, ambalo lilionekana kuwa huenda lina gesi.
Soma pia:
Kufikia sasa kuna maeneo mengine yaliyopo eneo la kusini mwa mradi huo, maeneo ambayo yameonyesha dalili za uwepo wa gesi.
Noble Helium ni kamouni inayojihusisha na miradi ya uchunguzi wa rasilimali nchini Tanzania ikijumuisha eneo la North Rukwa, North Nyasa, Eyasi Basin, na Manyara Basin.
Kwa sasa, bei ya hisa ya Noble Helium ni dola 0.059.
Mradi Wa Helium Wa Rukwa Ni Nini?
Mradi wa Rukwa ni mradi mkubwa wa uzalishaji wa gesi ya helium wenye ubora wa juu, ukihusisha eneo la takriban kilomita za mraba 3,590 kusini magharibi mwa Tanzania.
Mradi huu una uwezo mkubwa wa kusaidia soko la kimataifa lenye uhaba wa gesi ya helium.
Mradi wa North Rukwa unakadiriwa kuwa na rasilimali ya gesi ya helium inayofikia futi za ujazo bilioni 176, na kufanya kuwa rasilimali kubwa zaidi ya helium inayojulikana duniani.
Hii inatoa fursa kwa Tanzania kuwa moja ya wazalishaji wakuu wa helium duniani.
Helium ina matumizi muhimu sana, ikitumika kwenye mashine za MRI hospitalini, vifaa vya kielektroniki, na hata katika safari za anga za juu.