SI KWELI Kampuni ya Pepsi ya Israel imetoa soda mpya zenye rangi za bendera ya Palestina ili zinunuliwe na Wapalestina

SI KWELI Kampuni ya Pepsi ya Israel imetoa soda mpya zenye rangi za bendera ya Palestina ili zinunuliwe na Wapalestina

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Salaam ndugu zangu,

Nimeona picha inasambaa ikieleza kuwa Kampuni ya Israeli ya PEPSI imebadilisha muundo wake na kuandika Palestina ili kuepuka kufungiwa na Palestina.

IMG_20231031_074747_963.jpg
 
Tunachokijua
Pepsi ni jina la chapa ya kinywaji cha soda kinachotengenezwa na kampuni ya PepsiCo. Ni kinywaji maarufu cha soda kinachopatikana ulimwenguni kote. Pepsi inapatikana katika aina mbalimbali, kama vile Pepsi Cola, Diet Pepsi, Pepsi Max, na kadhalika. Kwa kawaida, Pepsi ina ladha ya cola na ina kaboni (mafuta ya carbon dioxide) ili kutoa burudani na uchachu.

Kumekuwapo na uvumi umesambaa kuwa kiwanda Cha Pepsi ya Israel kimetengeneza soda zake mpya na kuziandika neno Palestina kwa lengo la kuepuka kinywaji hicho kuzuiwa kuuzwa ndani ya Palestina. Uvumi huu unaenda sambamba na ajenda za kuwataka watu wa Palestina kutokubali kurubuniwa na kupinga kinywaji hicho cha pepsi kinachotoka Israel. Tazama kwenye picha hapa chini:

1698754082509-png.2798957

Upi ukweli kuhusu uvumi huu?
JamiiForums imepitia vyanzo rasmi vya Kampuni ya PepsiCo kutafuta taarifa hii ambapo imekutana na ujumbe maalumu uliowekwa kama rambirambi ya kuzipa pole familia zilizokubwa na matatizo Gaza, Palestina. Hata hivyo, hakuna tangazo wala taarifa yoyote inayoelezea kuwapo au kutengenezwa kwa vinywaji vyenye bendera na jina la nchi ya Palestina ili kuiunga mkono kama uvumi unavyodai.

Zaidi ya hayo, JamiiForums imepitia bidhaa zote zinazotengenezwa na Kampuni ya PepsiCo kwa sasa lakini hakuna bidhaa hata moja inayooneshwa kutengenezwa maalumu kwa ajili ya kuwaunga mkono Palestina.

Je, Pepsi ni bidhaa ya taifa la Israel
currentaffairs.adda247.com Wanaeleza kuwa Pepsi sio bidhaa ya taifa la Israel. Hata hivyo, Pepsi inamiliki Mkondo wa Soda SodaStream, kampuni ya Israeli inayotengeneza vifaa vya kutengeneza maji ya madini ya kaboni. Pepsi ni chapa ya soda ya Marekani ambayo inazalishwa na kusambazwa na na kampuni iitwayo PepsiCo, ambayo ni kampuni ya kimataifa ya chakula na vinywaji iliyoko nchini Marekani.

Baada ya kupitia vyanzo mbalimbali JamiiForums imebaini kuwa hoja hii ya kuwapo kwa Kampuni ya Pepsi Israel imesambaa kwenye kurasa za watu Binafsi hasusan wale wanaotetea matukio yanayoendelea Ukanda wa Gaza.

Hivyo, kutokana na vyanzo hivyo JamiiForums inaona kuwa hoja inayodai kwamba Pepsi imetengeneza bidhaa maalumu yenye jina na bendera ya Palestina halina ukweli.
kuepuka kufungiuwa na palestina.. ? hebu kafanye reasearch palestina anaifungiaje kampuni ya israle ikiwa 90% ya mahitaji yao yanapitia huko.. mi naona wametoa hizo aidha kuhadaa ulimwengu au ni siasa za ndani ya israel katika kuonyesha hawakubaliana na serikali yao inachikifanya.. kumbuka sio kila myahudi anasupport.. wenyewe kuna mtifuano wa kisiasa ..

so hao hawajatengeneza illi wawaplease palestina.. wana agenda zao
 
Back
Top Bottom