Kampuni ya Scancem yainunua Tanga Cement

Kampuni ya Scancem yainunua Tanga Cement

tang'ana

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2015
Posts
11,931
Reaction score
15,849
Dar es Salaam. Kampuni ya Scancem inayomiliki Twiga Cement imeafikiana na Kampuni ya Afrisam kununua asilimia 68.33 ya hisa za Tanga Cement ifikapo Juni 2022.

Bei ya hisa moja itakayolipwa na Scancem kwa Afrisam ni Sh3,157, hivyo kufanya jumla ya fedha zitakazolipwa kufika Sh137.329 bilioni kwa hisa zote.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa jana kwenye gazeti hili, masharti ya msingi yanayotakiwa kutekelezwa kabla ya kukamilisha ununuzi huo ni ruhusa ya Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) kwamba, ununuzi umekubaliwa kwa vigezo vilivyoafikiwa na pande zote mbili.

Pia, kuwe na ruhusa ya Tume ya Madini Tanzania (TMC) kwamba ununuzi umekubaliwa pamoja na ruhusa ya wanahisa wa Kampuni ya Tanga Cement kuhusu ununuzi huo kwa azimio maalumu la wanahisa.

Masharti mengine ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoa cheti cha uthibitisho kuwa kodi ya uuzaji wa hisa hizo imelipwa. Pia, kuwe na uthibitisho wa leseni zilizotolewa kihalali au zilizoombwa na Tanga Cement.

“Endapo masharti yote yatatekelezwa au yatasamehewa kutekelezwa mapema, basi ununuzi hautakuwa na masharti, hivyo utatekelezwa na utekelezaji wake unatazamiwa kufanyika mapema katika robo ya pili ya mwaka 2022,” linaeleza tangazo hilo.
Tangazo hilo la mauziano ambalo limethibitishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Tanga Cement, Laurence Masha linaeleza kuwa endapo ununuzi utakuwa hauna masharti na ukatekelezwa, utaifanya Kampuni ya Scancem kuwa mmiliki mkubwa wa kampuni ya Tanga Cement.

Endapo hilo litatokea na kama inavyotakiwa na kanuni kuu ya pili, tangazo hilo linaeleza, Scancem baada ya bei ya mwisho ya ununuzi kuwa imeamuliwa, itapeleka ofa ya jumla kwa Tanga Cement ya kutwaa hisa zilizobaki.

“Pande zote mbili zinaendelea kufanya mazungumzo na mamlaka za usimamizi, ikiwamo CMSA, Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), FCC na TMC kuhusu ununuzi huu. Matamko mengine yatafuata kadri mazungumzo yatakavyokuwa yanaendelea,” inasomeka sehemu ya tangazo hilo.

Hivyo, tangazo hilo linabainisha kwamba hakuna uhakika kama ofa ya jumla itapelekwa. Wanahisa wanashauriwa kuchukua tahadhari wanapofanya lolote kuhusiana na hisa walizonazo Tanga Cement mpaka tangazo litakapotolewa kuhusu kukamilika kwa ununuzi.

Kwa muunganiko huu, Twiga Cement itakuwa miongoni mwa kampuni kubwa za saruji nchini.

Chanzo: Gazeti la mwananchi la leo
 
Kumbe bwana Masha yupo nchini


Ajaribu Tena siasa mungu mtu katangulia kwa Sasa the ground is fair ajaribu
 
Bwana Masha anapambana walimkanyaga kwenye ule mladi wake ndege FastJet alikuwa anatudaidia sana
 
Naona ni mwendo wa kuuziana viwanda

Mbeya cement washa badili mmiliki naona hao tanga wanabadili mmiliki
 
Kuna huyu mchina Huaxin ni hatari kwa sasa East Africa yupo hapa tanga kiwanda chake hakina muda mrefu lkn ni hatari magari yanayopaki yafika hata miambili kila siku kunaingia magari kunatoka magari ... huyo Twiga anatakiwa ajiapange aje kuleta ushindani
 
Kuna huyu mchina Huaxin ni hatari kwa sasa East Africa yupo hapa tanga kiwanda chake hakina muda mrefu lkn ni hatari magari yanayopaki yafika hata miambili kila siku kunaingia magari kunatoka magari ... huyo Twiga anatakiwa ajiapange aje kuleta ushindani
Ana kiwanda cha nini?
 
Back
Top Bottom