Kampuni ya TECNO kuja na toleo la POP 7

Kampuni ya TECNO kuja na toleo la POP 7

TECNO Tanzania

Senior Member
Joined
Jul 6, 2016
Posts
192
Reaction score
217
Tukiwa tume uanza mwaka mpya kampuni ya simu ya TECNO iliojizolea umaarufu hasa kwenye uuzaji wa simu janja zenye ubora kwa bei nafuu inatarajia kuzindua toleo jipya kwenye mtiririko wake wa simu za POP na sasa wanakuletea toleo jipya la POP 7 lenye ubora zaidi hasa kwenye uhifadhi wa kumbukumbu.

Toleo la POP lina amika kuwa ni moja kati ya matoleo ambayo yana muwezesha mteja ambaye anatatumia simu janja kwa mara ya kwanza kufurahia matumizi ya simu yake kwenye ulimwengu wa kisasa. Toleo hili litazindulia siku zijazo na wateja wetu watapata kufurahia ubora na utofauti mpya kwenye matoleo ya POP.

WhatsApp Image 2023-01-05 at 11.08.47 (1).jpeg

Picha: Muonekano wa toleo la POP 7 linalotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni

Toleo la POP 7 inasemekana kuwa litakuja na suluhisho kwa wenye uhitaji mkubwa wa simu isiyo Gandaganga na yenye uhifadhi mkubwa wa kumbukumbu ikiwa na RAM ya 4GB yenye uwezo wa kuongeza mpaka 7GB RAM na ina 64GB ROM.

WhatsApp Image 2023-01-05 at 11.08.47 (2).jpeg

Picha: Mfumo wa uhifadhi kumbukumbu wa POP 7

Pia kuna maboresho mengi yamefanyka hasa kwenye usalama wa simu ambapo toleo hili la POP 7 limekuja na mfumo wa usalama wa simu wa aina mbili moja ni kwakutumia kidole (Fingerprint system) na nyingine ni kwa kutumia sura (Face Unlock system). Pia simu hii ina Screen kubwa ya 6.6 inches HD na itatumia chaji za Type C.

WhatsApp Image 2023-01-05 at 11.08.47.jpeg

Picha: Sifa kuu zilizoboresha kwenye Toleo la POP 7
 
Back
Top Bottom