Kampuni ya Vunja Bei yashinda tenda ya jezi za Simba Sc

Kwanza Hii Tenda Ya kutengeneza Jezi Za Simba Ilitangazwa Lini? Na Ni Kampuni Zipi Ziliomba Hiyo Tenda?
Ulitaka tangazo la tenda ulione kwa Millard Ayo au? Simba ilikuwa bado na mkataba na Uhl Sport kitendo cha kutangaza tenda hadharani unadhani kingekuwa na tija?

Unadhani kipi bora kuwatangazia watu wote hata wewe ambaye hata chelehani ya ushonaji huna (achana na kumiliki kampuni) au kuwafuata makampuni husika moja kwa moja?
 
Mkataba Wa Simba + Uhl Sports uliisha Lini? Na Makubaiano ya Simba Na VB yalianza Lini? Wamedai Kwamba VB wameshinda Tenda, Ndio Maana Nikauliza Hii Tenda Ilitangazwa Lini? Hata Kama Sijaona Huko MA
 
Uyo Vunja bei ndio level za mbumbumbu fc msitake mambo makubwa.
 
Mkataba Wa Simba + Uhl Sports uliisha Lini? Na Makubaiano ya Simba Na VB yalianza Lini? Wamedai Kwamba VB wameshinda Tenda, Ndio Maana Nikauliza Hii Tenda Ilitangazwa Lini? Hata Kama Sijaona Huko MA
Lakini kuna aina nyingi za manunuzi kwanini unawazia hiyo iliyo kichwani mwako tu?
 
Mo kajipigia pande kiaina, kwenye jicho la upembuz tumeshajua Vunja Bei yupo hapo kama wakala tu.
 
Naamini ameshaonesha sample kidogo..asije kuleta jezi kama za mabonanza..Simba inabidi ivae jezi za kuvutia na quality..na mashabiki wanaonunua original replica basi waone kidogo thamani ya hela yao hata kama ni 30k.

Big up VB
 
Atapata hasara tu,mijezi yenyewe haitanunuliwa,iko kama mitambaa ya Deki
 
Bora hii tenda kapewa huyu. Bei za jezi za Nike na Adidas tusingeziweza.
Vunja bei atatuvunjia vifurushi vya bei kulingana na uwezo wako.

Nimeupenda ubunifu wa Idea yao ya kutengeneza Viatu, Kofia, Saa na Cover za Simu za Simba. Hapa watawagusa hadi watu wa kipato cha chini.
 
Mkuuu umepigia kwa bei ya kuuuza hapa means akiuza jez hzo atakuwa amepata Faida je mchakato mzima upoje mpka jezi kuitwa jez na simba kuvaaa
Hiyo B3 ni makadirio ya kawaida, maana Pcs. 100000 unauza kwa mikoa mi 4 tu. Dar, Mwanza, Arusha, Dodoma. Ongeza Pcs 15000 za mikoa mingine

Ukitoa gharama za uzalishaji hakosi B1 au B1.5 kama faida kumbuka yeye analipa B1 kwa msimu.

Hapo bado kava za simu, kofia, skafu, miwani na makorokoro kama hayo.

Cha mwisho jamaa ana maduka mikoa mingi kwa hiyo ni rahisi kuuz Jezi nyingi zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…