Kampuni ya YÜTEK ya Uturuki yasaini mikataba ya ujenzi wa meli

Shughuli hiyo ilifanyika Leo Mwanza Tanzania ambapo wizara ya Ujenzi kwa niaba ya MSCL Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania na Yücel Tekin Shipbuilding Company YÜTEK kampuni toka Uturuki zilisaini mkataba wa thamani ya dola za kimarekani US$180 million sawa na shilingi 417,240,000,000.

04 December 2021
Dar es Salaam, Tanzania

PROF. MBARAWA AVUNJA BODI ZA TPA NA MSCL

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amevunja Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), na Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), kwa sababu ya uzembe na usimamizi mbovu wa miradi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa maboresho ya Gati namba 0 hadi 7 na uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa miundombinu ya Usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Pili (km 20.3) uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

"Leo tarehe 04/12/2021 kwa Mamlaka niliyonayo nimetengua Bodi za Wakurugenzi wa TPA na MSCL kutokana na kutokuwajibika ipasavyo katika kutoa ushauri na wakati wa ubadhirifu na ukiukwaji wa vipengele katika mikataba ya miradi walikuwepo", amesema Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amesema kuwa uamuzi huo umetokana na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan kutoridhishwa na utendaji kazi wa Bandari ya Dar es Salaam hasa katika usimamizi wa gati hizo zilizoboreshwa kutokuwa mzuri na kusababisha kuwepo kwa marekebisho ya baadhi ya gati ili viendane na viwango vinavyostahili kulingana na mkataba.

Prof. Mbarawa ameeleza pia kumeripotiwa matukio ya wizi katika mifumo ya bandari ambapo mkandarasi aliyefunga hiyo mifumo hakuitekeleza ipasavyo na kuacha mianya ya wizi ukaendelea.

Kwa upande wa Kampuni za Huduma za Meli Tanzania (MSCL), Prof. Mbarawa amebainisha kumekuwa na mapungufu kwa mkandarasi aliyeshinda kazi za ujenzi wa meli nne zinazotarajiwa kujengwa katika Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika na Bahari ya Hindi.

"Baada ya utiaji saini mikataba minne tarehe 15 Juni, 2021 Serikali ilitilia shaka uwezo wa mkandarasi na kuamua kufanya ufuatiliaji wa uwezo wa mkandarasi huyo aliyeshinda zabuni na kubaini kuwa hana uwezo wa kutengeneza meli na hakuwa na ofisi”, amefafanua Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri Prof. Mbarawa ametoa rai kwa watendaji wote waliopo chini ya Wizara yake kuwa waadilifu na kusimamia kwa karibu miradi yote inayoendelea kutekelezwa.

"Naomba nichukue fursa hii kuwataka watendaji wote kuwa waadilifu, wazalendo, tuumwe na nchi hii katika miradi ya kiamaendeleo", amesisitiza Prof. Mbarawa.

Bodi ya Wakurugenzi ya TPA ilikuwa na jumla ya wakurugenzi saba (7) ikiongozwa na Mwenyekiti Prof. Ignas Rubalatuka na Bodi ya MSCL ina wakurugenzi watano (5) ikiongozwa na Mwenyekiti Prof. Zacharia Mganilwa
 
Kumbe alikuwepo mwenyewe kushuhudia Mwanza [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] leo analaumu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Yaani wamebaki peke yao Bungeni na serikalini lakini wapi
 
MRADI HUU NI WA MAANA MNO HAKIKA RAIS TUMEPATA ANA AKILI KUPITILIZA,MRADI HUU UNAWATEJA WAKE STANDBAY YAANI NI SISI ABIRIA TUNAUSUBIRI TUZIJAZE MELI KWA MIZIGO YA KIBIASHARA,NA NYIE KAJAZENI MADEGE YENU NA MIRADI YA AJABU AJABU YA HASARA,MAMA KIROHO SAFI UZA MADEGE MAWILI UWALIPE WATURUKI WATUHARAKISHIE MELI ZETU.
bado unasubiri meli hewa
 
Kwasababu hakuna ushindani na makampuni yenye mapesa ya kumwaga kama Qatar, Emirate, Turkey, na wengine.

Pia ni mradi unaogusa na kuhudumia Watanzania wengi wa kipato cha chini na kati kulinganisha na shirika la ndege.

Kwa, mfano, kuna meli itakayokuwa na uwezo wa kubeba mifugo.

Moja ya meli zinazojengwa ina capacity ya kubeba tani 400. Nyingine inaweza kubeba mabehewa / wagon 26.

Meli pia zinajengwa[ 3 kati ya 4] hapahapa nchini hivyo upo uwezekano wa Watz kupata ajira, na knowledge and technology transfer itakuwepo. Ndege zinaundwa ktk nchi za mabeberu na kutoa ajira kwenye viwanda vya mabeberu.

Meli zinakwenda kuchangamsha biashara kati ya Tanzania na majirani zetu haswa wa DRC na Uganda.

Na ile ya kubeba mabehewa itawezesha bandari yetu kusafirisha mizigo mingi zaidi kwenda Uganda.

NB:

Hili halihusiani na meli zinazojengwa, lakini nimesikia kuna ukanda wa biashara kati ya Tz -- Uganda -- Drc kupitia mpaka wa Mutukula. Watu wengi na haswa serikali hawafahamu kuhusu potential ya ukanda huo. Hilo nimelisikia toka kwa Balozi wa Tz nchini DRC.
Kumbe kampuni yenyewe fanfa, ni Richmond nyingine hii.
 
Huu mradi ulisainiwa na serikali ya awamu ya sita chini ya usimamizi wa Mama Samia Suluhu Hassan kwa 100%.
Nani atabisha kuwa, Samia anahusika na hii skendo?
Masalia ya Magufuli ndio walipiga hii deal wakamdanganya mama, sasa mama baada ya kupata ukweli kupitia vyombo vyake amechukuwa hatuwa.

Dawa ni kuondowa chawa wote wa Magufuli na kuvunja baraza la mawaziri aliunde upya tuanze upya.

Huu ni ufisadi wa genge la wahuni wa Magufuli.
 
04 December 2021
Dar es Salaam, Tanzania

PROF. MBARAWA AVUNJA BODI ZA TPA NA MSCL

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amevunja Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), na Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), kwa sababu ya uzembe na usimamizi mbovu wa miradi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa maboresho ya Gati namba 0 hadi 7 na uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa miundombinu ya Usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Pili (km 20.3) uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

"Leo tarehe 04/12/2021 kwa Mamlaka niliyonayo nimetengua Bodi za Wakurugenzi wa TPA na MSCL kutokana na kutokuwajibika ipasavyo katika kutoa ushauri na wakati wa ubadhirifu na ukiukwaji wa vipengele katika mikataba ya miradi walikuwepo", amesema Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amesema kuwa uamuzi huo umetokana na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan kutoridhishwa na utendaji kazi wa Bandari ya Dar es Salaam hasa katika usimamizi wa gati hizo zilizoboreshwa kutokuwa mzuri na kusababisha kuwepo kwa marekebisho ya baadhi ya gati ili viendane na viwango vinavyostahili kulingana na mkataba.

Prof. Mbarawa ameeleza pia kumeripotiwa matukio ya wizi katika mifumo ya bandari ambapo mkandarasi aliyefunga hiyo mifumo hakuitekeleza ipasavyo na kuacha mianya ya wizi ukaendelea.

Kwa upande wa Kampuni za Huduma za Meli Tanzania (MSCL), Prof. Mbarawa amebainisha kumekuwa na mapungufu kwa mkandarasi aliyeshinda kazi za ujenzi wa meli nne zinazotarajiwa kujengwa katika Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika na Bahari ya Hindi.

"Baada ya utiaji saini mikataba minne tarehe 15 Juni, 2021 Serikali ilitilia shaka uwezo wa mkandarasi na kuamua kufanya ufuatiliaji wa uwezo wa mkandarasi huyo aliyeshinda zabuni na kubaini kuwa hana uwezo wa kutengeneza meli na hakuwa na ofisi”, amefafanua Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri Prof. Mbarawa ametoa rai kwa watendaji wote waliopo chini ya Wizara yake kuwa waadilifu na kusimamia kwa karibu miradi yote inayoendelea kutekelezwa.

"Naomba nichukue fursa hii kuwataka watendaji wote kuwa waadilifu, wazalendo, tuumwe na nchi hii katika miradi ya kiamaendeleo", amesisitiza Prof. Mbarawa.

Bodi ya Wakurugenzi ya TPA ilikuwa na jumla ya wakurugenzi saba (7) ikiongozwa na Mwenyekiti Prof. Ignas Rubalatuka na Bodi ya MSCL ina wakurugenzi watano (5) ikiongozwa na Mwenyekiti Prof. Zacharia Mganilwa
Hayo ndo mambo ya PPRA wanayependa eti kampuni imeshinda tenda na hiana hata uwwzo ww kufanya hiyo kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Masalia ya Magufuli ndio walipiga hii deal wakamdanganya mama, sasa mama baada ya kupata ukweli kupitia vyombo vyake amechukuwa hatuwa.

Dawa ni kuondowa chawa wote wa Magufuli na kuvunja baraza la mawaziri aliunde upya tuanze upya.

Huu ni ufisadi wa genge la wahuni wa Magufuli.
Ila Kuna sehemu mnatuchanganya pia, kipindi mradi unasainiwa mlimsifia mama kuwa kaleta mradi mzuri, Sasa mnasema ni wa watu wa magufuli
 
Duh,hiyo nchi mbombo ngafu.
Kuna jamaa sijui mkurugenzi wa TPA nimemuona akijieleza anatetemeka na missread kibao, aisee nikajua tu huyu analiwa kichwa na yametokea.
 
Back
Top Bottom