Kampuni za betting zinapataje faida?

Kampuni za betting zinapataje faida?

weka na leo salzburg ashinde ndio utaelewa wanapataje faida
Sasa ww kwa akili yako kuna mwenye akili timam anaweza akampa salzburg leo ushindi?

Salzburg yupo ugenini dhidi ya bayern Munich

Ni mwendawazim pekee ndo anaeweza mpa salzburg ushindi
 
Mikeka yangu mitano imechanika. Ila sikati tamaa nacheza tena
Usikate tamaaa... Mafanikio yanakuja taratibu.. Na ulitaka kula sana weka ela nyingi... Then jifunze zile bet za cassino..[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Uweke na screenshot vinginevyo ni porojo
 
Haya makampuni yanavuna kweli kweli..juzi nlikuwa katika betting shop ya thronebet nacheki game ya man utd, aiseee wale jamaa ilipokaribia mida ya kufunga wakawa wanaenda kupakua pesa kutoka katika zile slot machine..aisee niseme th ukweli ni kuwa watu wanaliwa sana pesa.Wale jamaa wa throne bet walijaza box zima la noti noti.
 
Mi nawanyoosha. Naweka elfu 1 mechi 18. Watajua hawajui. Hela yao niliyoshinda juzi ndiyo naitumia kubet. Sina hasara
Hivi hapa asiyejua ni wenyewe kweli ?

Tuseme unachukua odds za favourites kabisa tena Double Chance yaani 1X; 2X au 12 hapo nakupa odds nzuri za 1.2 (ingawa hapa unaweza ukapewa chini ya hapo)

accumulator ya 18 kwa odds za 1.2 = 26.6 kwa buku yako unapata 26,000/= (Hapo Serikali hajachukua chake 15%)

Na probability ya kupatia timu zote 18 huenda ni mara moja katika kila chaguzi 100 au tuseme 50, au hata tuseme 30, In short hapo ukijapiga hesabu mwisho wa mwaka unaweza kujikuta una minus..., Kuna watu wana miaka kadhaa wanafukuzia accumulator na katika miaka 10 walishashinda kama mara 5 (ila wengi wanakumbuka hizo tano na wanasahau vipigo vya kila siku)
 
Mkuu unashauri nchi ichukue hatua gani juu ya huu utapeli wa kisasa?
 
Leo nimecheza viligi vya Kuwait huko na.Austria hukoo. Nikishinda nakula laki 4. Nimeweka 2550 tu odds 200 total.
😂😂😂😂 Umekaribishwa vibaya sana zaidi ya sana kwenye betting world.

Mkuu ni afadhari ukabet ukaliwa, utajua uchungu na hapo unaweza kuamua uache au uendelee ama lah utabet kwa kujifurahisha tu.

Ila wewe umekaribishwa vibaya kwa kushinda pesa mingi na mbaya zaidi una imani kua wao hawapati faida. Mkuu ushaingi kwenye kubet na sijui kama utaacha.

Wao wanapata faida kwa wale wanaoliwa, wewe umebet hivo ila kuna mamia huko wamebet mechi kama zako ila tofauti na ww.
 
Mkuu unashauri nchi ichukue hatua gani juu ya huu utapeli wa kisasa?
Ni ngumu kwa nchi kuchukua hatua directly sababu wana-assume kwamba kila mtu anafanya kwa wito wake na anaupeo kwa kutosha (ni mtu mzima)..., Ila nchi inashangilia kwa kodi wanazopata bila kujali long term effects...

Bali inachobidi kufanyika ni kupunguza matangazo directly ambayo yanafanya recruitment hata kwa watoto..., Betting Firms / Outlets zote ziwe na kibali na wahakikishe under 18 hawaingii wala kufanya betting...

Pili mchezo huu uende na ushauri sio tu kuwaambia watu watusue mapeme bila kuwahabarisha hatari ya kutusuliwa wao......, Yaani kila tukioneshwa Mtu aliyepata trillioni kadhaa kule Nigeria pia tuone aliyeuza nyumba na kufukuzwa na mke wake kule Naivasha....

Addiction yoyote ni mbaya, kwahio hizo pesa Serikali inazopata through gambling / addiction zitumike pia kutoa elimu ya madhara ya gambling as well as watengeneze sera za kuwapatia watu ajira zenye ujira ili watu wapate kipato na sio hizi illusion za one day Yes....
 
Sahihi kabisa, juzi nliingia kwenye betting shop moja mitaa ya kinondoni dah nliskitika kwa kweli.99% ya nyuso za wanaobeti mule hazina furaha na idadi ya wanaochana mikeka ni kubwa sana. Yaani ktk watu 1000 wanao-wager basi ni watu 5 tu ndio wanaopata
 
Leo nimehamia M-BET kidogo. Hawa ndugu wana option nzuri sana. Hasa hii ya "both teams to score". Yaani leo ndiyo watajua hawajui. Tuonane saa 6 kushangilia mtu alivyonyooshwa. Utaratibu ni uleule, stake elfu 2 odds 100. I WAS BORN TO WIN
 
Sasa kwanini usitangazie na wengine huo uwezo wako wa kupata odds 100..., Na hapo huenda ukapata pesa maradufu bila hata kutumia senti yako moja....

Unawapa watu odds wanakula wanakupa commission...

Nina uhakika ulimwengu mzima watakutafua na hata kama sio 100% hata ku-maintain 80% winning Streak bado itakuwa an outstanding Job.....

If I was a Betting Man ningebet a large amount kwamba BTT odds mia moja kupata zote unaweza ukacheza mara 1000 na usipate hata mara moja..., hapo kwa haraka haraka ni 2000/= mara hicho kipigo mara 1000 utakuwa umewachangia hao M-BET na Serikali 2,000,000/=

NB: Hio Betting Option ipo kwa Bookies wote kwani ni chanzo chao kizuri pia kinachowaweka mjini....
 
Back
Top Bottom