Kampuni za kupima ardhi na mipango miji (Urasimishaji)

M2WAWA2

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2014
Posts
3,285
Reaction score
5,598
Ni miaka mitatu sasa tangu kuwepo kwa vuguvugu la Makampuni ya kutoa huduma za Urasimishaji Viwanja na mashamba kwa gharama ya 250,000 (baadaye gharama ikashuka kuwa 150,000). Lengo likiwa mwenye shamba /viwanja kupewa hati ya umiliki.

Kwa maeneo ya Tegeta Madale, Mivumoni, Goba, Msigani jijini Dar es Salaam, kuna kampuni zilipewa kandarasi kufanya kazi hii.Kwa sasa naona kimya hakuna kinacho endelea, Simu zao hazipatikani, ofisi zao zipo na mara nyingi hazifunguliwi.

Je huko kwenu zoezi hili limefanikiwa? Kuna walio pata hati? Tupeane taarifa wadau

NB: HII NI TAARIFA TANGU APRIL 2021.

https://habarileo.co.tz/habari/2021-04-166079e4141ca55.aspx#

SOMA HII PIA

Lukuvi ashusha gharama za urasimishaji, wanaoishi mijini sasa hati ni lazima

https://www.lands.go.tz/publications/12
 
Hii nchi hatuwezi kamwe kuendelea. Hatupo serious na mambo yetu kabisa. Ardhi yetu tungeweza kui manage vizuri, ni chanzo kikikubwa na cha uhakika. Kodi ya Ardhi na ya Majengo....tunakosa pakubwa sana. Na hili la ardhi kutopimwa lina athari nyingi sana kiuchumi, mathalani ni rahisi kupata mikopo ya kilimo na hata ujenzi kama ardhi ni rasmi (ina hati).

Huko kwenye Ardhi, sijua kwanini wameng'ang'ana na Mh. Lukuvi.....ameshachoka hawezi kuleta mabadiliko chanya.
 
Ada ya kupimiwa eneo na pesa ya hati ni tofauti

kupimiwa eneo 150,000

hati inategemeana na ukubwa wa eneo
 
Hii nchi hatuwezi kamwe kuendelea. Hatupo serious na mambo yetu kabisa. Ardhi yetu tungeweza kui manage vizuri, ni chanzo kikikubwa na cha uhakika. Kodi ya Ardhi na ya Majengo....tunakosa pakubwa sana. Na hili la ardhi kutopimwa lina athari nyingi sana kiuchumi, mathalani ni rahisi kupata mikopo ya kilimo na hata ujenzi kama ardhi ni rasmi (ina hati).

Huko kwenye Ardhi, sijua kwanini wameng'ang'ana na Mh. Lukuvi.....ameshachoka hawezi kuleta mabadiliko chanya.
Watu tunapenda mikopo. Hivi ukipewa mikopo ya kilimo si hiyo ardhi itachukuliwa tu. Imagine mvua kutonyesha, au bei kuwa chini wakati gharama za uzalishaji zipo juu
 
Kuna maeneo kampuni zimefanikiwa, hii ni kutokana na wananchi kushirikiana vyema na kampuni husika.
Gharama ya upimaji na ufanisi wa kampuni inategemea sana idadi ya waliojiandikisha na walio tayari kurasimisha, wanaohitaji kupimiwa kwa bei elekezi ya 150k wakiwa wachache (<10) gharama ni kubwa sanaaa kwa kampuni tofauti na wakiwa wengi >100
 
Watu tunapenda mikopo. Hivi ukipewa mikopo ya kilimo si hiyo ardhi itachukuliwa tu. Imagine mvua kutonyesha, au bei kuwa chini wakati gharama za uzalishaji zipo juu
Nchi tu yenyewe inakopa, itakuwa mimi na wewe ndugu yangu? Mikopo ikutumika vizuri inanyanyua biashara pakubwa tu hasa kama umejipanga vizuri. Wewe unalima wapi? Mimi ni mkulima (kilimo cha umwagiliaji), najua faida ya mikopo ya benki. Wengine huwa wanakimbilia mikopo ya vicoba (rahisi kuipata), lakini relatively in gharama kubwa sana. Riba za mabenki ni around 20% kwa mwaka, lakini huko kwenye vicoba, haishangazi kusikia hata 10% kwa mwezi (ambay effectivley ni 120% kwa mwaka!)

Nimetoa mfano tu ugumu wa mikopo. Lakini athari za ardhi kutopimwa ni nyingi zaidi.

Thamani ya ardhi yenye hati na isiyo na hati ni tofauti sana. Na nyumba pia, iliyo kwenye sehemu rasmi thamani yake inakuwa kubwa zaidi.
 
Nchi tu yenyewe inakopa, itakuwa mimi na wewe ndugu yangu? Mikopo ikutumika vizuri inanyanyua biashara pakubwa tu hasa kama umejipanga vizuri.

Nimetoa mfano tu ugumu wa mikopo. Lakini athari za ardhi kutopimwa ni nyingi zaidi.

Thamani ya ardhi yenye hati na isiyo na hati ni tofauti sana. Na nyumba pia, iliyo kwenye sehemu rasmi thamani yake inakuwa kubwa zaidi.
Usiige kupoo kwa tembo.... Kukopa kwa Serikali si sawa na kwa mimi na wewe. Angalia hata mashirika ya dini mfano juzi Malasusa anadaiwa 1.9B akazigawanya kwa waumini wake. Wewe na mimi ni majanga hasa kipindi hiki ambacho hatuna mabenki ya uwekezaji bali ya biashara.

Ni kweli hata mimi nina mikopo of course ila si kila mtu anaweza kukopa ndiyo maana kila siku kuna minada na mpaka Kigamboni jamaa ana kesi ya kuua baada ya Kituo chake cha mafuta kunyakwa na Benki.
 
Hii nchi hatuwezi kamwe kuendelea. Hatupo serious na mambo yetu kabisa. Ardhi yetu tungeweza kui manage vizuri, ni chanzo kikikubwa na cha uhakika. Kodi ya Ardhi na ya Majengo....tunakosa pakubwa sana. Na hili la ardhi kutopimwa lina athari nyingi sana kiuchumi, mathalani ni rahisi kupata mikopo ya kilimo na hata ujenzi kama ardhi ni rasmi (ina hati).

Huko kwenye Ardhi, sijua kwanini wameng'ang'ana na Mh. Lukuvi.....ameshachoka hawezi kuleta mabadiliko chanya.
I agree with you, Lukuvi alianza vizuri but he is now out of new tricks & innovation apewe mtu mwingine. Imagine angalau 50% ya ardhi yote iwe imepimwa na hati kutolewa ni kodi halali kiasi gani hapo ingepatikana?
 
  • Thanks
Reactions: SMU

Mkuu mkopo siyo kitu rahisi hivo. Mkopo ni mtego na wabongo tusivyokuwa serious, tutaishia kuuziwa hayo mashamba
uswahili mwingi
 
Hoja yako ni nini hasa? Kwamba kwa kuwa mikopo ni hatari (risky), then hakuna umuhimu wa ardhi kurasimishwa? Maana mada kuu hapa ni urasimishaji wa ardhi.

Mimi nimetolea unafuu au urahisi wa mikopo kama mojawapo ya faida za kurasimisha ardhi. Kwa hivi lisitutoe kwenye mada kuu hapa ya hitaji la kurasimisha ardhi na madhara yake kiuchumi na kijamii tunayopata kwa kuwa na ardhi isiyopimwa/rasimishwa. Mikopo ina faida na hasara zake. Sidhani tunaweza kupishana katika hilo.
 
Oh! Kurasimisha ni muhimu ila masuala ya mikopo
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Mkuu mkopo siyo kitu rahisi hivo. Mkopo ni mtego na wabongo tusivyokuwa serious, tutaishia kuuziwa hayo mashamba
uswahili mwingi
Upo sahihi kabisa. But ukijipanga mikopo haina shida.

Nina mikopo kadhaa y la kilimo na so far sijapata tatizo lolote. Naanzia sokoni.....ninalima kitu ambacho kina mteja tayari na bei na gharama kwa sehemu kubwa zinajulikna zinajulikana.

But kama hujajipanga, mikopo ni hatari. Hilo halina ubishi na sifikiri kama hoja yako hapa ni kuwa ardhi isirasimishwe kwa kuwa watu wataitumia kukopa na kuishia kunyang'anywa na mabenki!?
 
Tunataka hela zetu au la wakamilishe zoezi la urasimishaji mpaka hati.
 
I agree with you, Lukuvi alianza vizuri but he is now out of new tricks & innovation apewe mtu mwingine. Imagine angalau 50% ya ardhi yote iwe imepimwa na hati kutolewa ni kodi halali kiasi gani hapo ingepatikana?
Exactly my point.
 
Ni miaka mitatu sasa tangu kuwepo kwa vuguvugu la Makampuni ya kutoa huduma za Urasimishaji Viwanja na mashamba kwa gharama ya 250,000 (baadaye gharama ikashuka kuwa 150,000). Lengo likiwa mwenye shamba /viwanja kupewa hati ya umiliki.

Kwa maeneo ya Tegeta Madale, Mivumoni, Goba, Msigani jijini Dar es Salaam, kuna kampuni zilipewa kandarasi kufanya kazi hii.Kwa sasa naona kimya hakuna kinacho endelea, Simu zao hazipatikani, ofisi zao zipo na mara nyingi hazifunguliwi.

Je huko kwenu zoezi hili limefanikiwa? Kuna walio pata hati? Tupeane taarifa wadau

NB: HII NI TAARIFA TANGU APRIL 2021.

https://habarileo.co.tz/habari/2021-04-166079e4141ca55.aspx#

SOMA HII PIA

Lukuvi ashusha gharama za urasimishaji, wanaoishi mijini sasa hati ni lazima

https://www.lands.go.tz/publications/12
FRANCIS DA DON kampuni yako imekula hela za watu ukala kona na kuingia mitini.
 
Upo sahihi kabisa. But ukijipanga mikopo haina shida.

Nina mikopo kadhaa y la kilimo na so far sijapata tatizo lolote. Naanzia sokoni.....ninalima kitu ambacho kina mteja tayari na bei na gharama kwa sehemu kubwa zinajulikna zinajulikana.

But kama hujajipanga, mikopo ni hatari. Hilo halina ubishi na sifikiri kama hoja yako hapa ni kuwa ardhi isirasimishwe kwa kuwa watu wataitumia kukopa na kuishia kunyang'anywa na mabenki!?
Hoja yangu ni kuhusu kukopa tu na siyo kurasimisha ardhi
Kwanza benki haiwezi kuangalia ardhi tu na kukupa mkopo, itaangalia namna gani utalipa huo mkopo
Tatizo kubwa la kilimo ni kukosa masoko
kama wewe una pa kuuzia una heri
mwaka 2019 may nilivuna gunia 90 tarime za mpunga , juzi hapa mwezi huu wa 9 ndo nilipata soko
 
Yap vigezo vya mikopo ni vingi sio collateral pekee. BUT kama vigezo vyote vipo sawa kwa wakopaji na wote wanataka kutumia ardhi au nyumba zao kama collateral, mwenye ardhi/nyumba iliyo na hati ya serikali, ni rahisi kuthibitisha umiliki wake na hivyo kwa mkopeshaji (benki) ni bora zaidi kuliko ardhi/nyumva isiyo na hati iliyotolewa na serikali. Mbona ni mambo basic tu haya.!
 
Hii nchi hatuwezi kamwe kuendelea. Hatupo serious na mambo yetu kabisa. Ardhi yetu tungeweza kui manage vizuri, ni chanzo kikikubwa na cha uhakika. Kodi ya Ardhi na ya Majengo....tunakosa pakubwa sana. Na hili la ardhi kutopimwa lina athari nyingi sana kiuchumi, mathalani ni rahisi kupata mikopo ya kilimo na hata ujenzi kama ardhi ni rasmi (ina hati).

Huko kwenye Ardhi, sijua kwanini wameng'ang'ana na Mh. Lukuvi.....ameshachoka hawezi kuleta mabadiliko chanya.
Lukuvi na wasaidizi wake ni wa hovyo kabisa! Ile wizara inahitaji mchapakazi kama Aweso
 
Ni miaka mitatu sasa tangu kuwepo kwa vuguvugu la Makampuni ya kutoa huduma za Urasimishaji Viwanja na mashamba kwa gharama ya 250,000 (baadaye gharama ikashuka kuwa 150,000). Lengo likiwa mwenye shamba /viwanja kupewa hati ya umiliki.

Kwa maeneo ya Tegeta Madale, Mivumoni, Goba, Msigani jijini Dar es Salaam, kuna kampuni zilipewa kandarasi kufanya kazi hii.Kwa sasa naona kimya hakuna kinacho endelea, Simu zao hazipatikani, ofisi zao zipo na mara nyingi hazifunguliwi.

Je huko kwenu zoezi hili limefanikiwa? Kuna walio pata hati? Tupeane taarifa wadau

NB: HII NI TAARIFA TANGU APRIL 2021.

https://habarileo.co.tz/habari/2021-04-166079e4141ca55.aspx#

SOMA HII PIA

Lukuvi ashusha gharama za urasimishaji, wanaoishi mijini sasa hati ni lazima

Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Development
Hawa walikuwa majambazi walikuwa 150,000 Arusha hovyo sana hawa watu. Na serikali haifanyi chochote inawangalia tu
 
Hii nchi hatuwezi kamwe kuendelea. Hatupo serious na mambo yetu kabisa. Ardhi yetu tungeweza kui manage vizuri, ni chanzo kikikubwa na cha uhakika. Kodi ya Ardhi na ya Majengo....tunakosa pakubwa sana. Na hili la ardhi kutopimwa lina athari nyingi sana kiuchumi, mathalani ni rahisi kupata mikopo ya kilimo na hata ujenzi kama ardhi ni rasmi (ina hati).

Huko kwenye Ardhi, sijua kwanini wameng'ang'ana na Mh. Lukuvi.....ameshachoka hawezi kuleta mabadiliko chanya.
uko sahihi kabisa, Lukuvi choka mbaya, amejikati tamaa ingawa he did a good job at the beggining
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Back
Top Bottom