Michael mbano
JF-Expert Member
- Apr 4, 2022
- 820
- 570
Zipo baadhi ya kampuni za mabasi wahudumu wake wanakosa sifa za huduma bora ili kuepusha migogoro.
Mfano kuna kampuni inaitwa Kisumapai ya Songea, kuna siku nimesafiri nimepokelewa na mhudumu aliyevaa tishet yao akaweka mzigo wangu kwenye buti. Wakati huo mkatisha tiketi wa kampuni hiyo anaona.
Nilipofika kituo cha kushuka kondakta ananiambia lipia mzigo. Sasa ishu haikuwa kulipa ila kwanini hamumjulishi mteja mapema wakati mnapokea mzigo wake kuwa utagharimu kiasi fulani kabla gari haijatoka ili mtu ajijuwe mapema?
Kitendo cha kufika mahala pakushuka ndipo mnamwambia mnaleta mgogoro tena mgogoro unachangiwa na kondakta kwasababu anapaswa awepo wakati mizigo inapakiliwa. Ajabu pia anajibu hamjuwi aliyepokea mzigo kwahiyo walimuachaje mtu hadi anavaa tishet yao na kuwajibika kwenye gari yao?
Jambo hili limetokea kwa watu tofauti pia, hata ukituma maoni na ushauri ktk namba walizokuandikia haujibiwi. Mjirekebishe na siyo kampuni hiyo tu na kampuni nyingine pia wenye tabia kama hizo mtafukuza wateja.