Kampuni za wakopeshaji pesa zilizozagaa mtaani kwa lugha ya pesa chap chap!
Baadhi zinafanya vizuri na baadhi zinafanya vibaya!
Ifahamike mtandao wa biashara unapoajiri vijana wengi huhitaji weledi wa juu sana kuweza kuwakumbusha Hekima ya biashara!
Nitoe mfano hai!
Jeshi la polisi lina vijana wenye mafunzo na weledi mzuri kutoka chuo cha mafunzo!
Lakini mara moja moja huwa tunashuhudia baadhi yao wanapofikishwa vituo vya kazi huweza kuadhibu watuhumiwa hata matukio kadhaa huwa tunasikia watuhumiwa kufia mahabusu!
Sasa makosa kama hayo ya askari mmoja kumwazibu raia hata kuuwa huwa hakiwezi kufuta taasisi nzima ya jeshi la polisi!
Hivyo basi! Makosa ya kibinadamu kwa watendaji hayapaswi kufuta taasisi kwasababu katiba ya taasisi huwa haina sera ya kuuwa mtu katika madai!
Taratibu za mikopo zinafahamika! Kila mkopaji na mkopeshaji huwa wanamakubaliano!
Utekelezaji wa hayo makubaliano unapovunjwa na wahudumu siyo busara kufuta taasisi nzima!
Nashauri linapotokea jambo kama hilo lililotokea kampuni ya OYA Kesi isikilizwe kama kesi zingine za mauaji mahakamani na inapobainika wahusika wa tukio wawajibishwe wao kama wao!
Lakini kwa upande mwingine WAKOPAJI (WATEJA) Baadhi yao wamekuwa chanjo cha kuvunja makubaliano!
Unachukua mkopo OYA Halafu unakwenda kufanyia shughuli ambazo hazizalishi, hili nalo linachangia usumbufu katika marejesho, lugha na ushirikiano wa wateja baadhi siyo rafiki wengi huzima simu na kujificha!
Sasa Pesa za wakopeshaji ni za mzunguko kwamba wateja wasipolipwa nao hawalipwi n.k
Mambo kama hayo yanaweza ibua vita ya kudaiana!
Ushauri wangu!
Elimu itolewe kwa wakopeshaji na endapo kukiwa na ukiukwaji wa masharti ya malipo, basi wakopeshaji wahakikishe wanachukua barua kutoka kwa mwenyekiti wa mtaa wanapokuja kuchukua dhamana kwa mteja wao!
Pia wakopaji wajiridhishe uhalali wa dhamana kama ina mhusu mkopaji haiwezekani mme hana taarifa ya mkopo halafu wakoshaji wafike kuchukua dhamana!
KUKOPA SHEREHE KULIPA MATANGA!
Soma:
=> Pwani: Wafanyakazi wa kampuni ya mikopo ya OYA, mbaroni kwa tuhuma za mauaji