KERO Kampuni za Mikopo Mtandaoni zinakiuka masharti ikiwemo kuweka Riba 52% BoT, Wizara ya Fedha mpo kimya tu!

KERO Kampuni za Mikopo Mtandaoni zinakiuka masharti ikiwemo kuweka Riba 52% BoT, Wizara ya Fedha mpo kimya tu!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

hotstoryg

Member
Joined
Apr 16, 2011
Posts
18
Reaction score
14
Hizi kampuni za mikopo online zimekuwa na kero kubwa kwa wakopaji, yaani mtu unakopa laki moja (100,000) unalazimishwa kurudisha Sh 152,000 ndani ya siku 5. Ambayo ni riba ya asilimia 52, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ipo wapi? Serikali ipo wapi kwa huu unyanyasahlji unaofanyika kwa Watanzania?

Kero ya pili ni kwamba Waziri Mkuu Mr Mwigulu alikemea tabia ya hizi taasisi kuwapigia simu watu ambao sio wadhamini wa mkopo pindi mtu anapochelewesha kulipa, lakini hizi taasisi ukichelewa kulipa kwa siku moja tu wanawatumia meseji watu wako waliomo katika contacts na kuwaambia kuwa wewe na wao ni matapeli wakati hao watu hata kwenye udhamini wa mkopo sio wahusika.

Hii imekua kero kubwa sana, tunaImba BoT iingilie kati, kulipa asilimia 52 (52%) kama Riba kwa mkopo wa siku 5 sio sawa kabisa na pia wamekuwa waongo ukikopa katika App inakuambia unalipa baada ya siku 7 ila ikifika siku 5 wanakusumbua sana na kusema kwenye masharti ambayo hayaonekani katika App wakati unakopa eti yanasema ni siku 5, sasa kwa nini wadanganye wakati unakopa na kusema ni siku 5!

Waziri wa Fedha na BoT tunaomba msaada wenu, mkitaka ushahidi wa matusi na meseji zakuchafua mkopaji nipo na nipo tayari kuwakilisha kwenu.

Soma pia:

1) DOKEZO - BoT na Serikali imeshindwa kudhibiti mikopo ya mitandaoni!? Au kwasababu zinamilikiwa na wachina

2) DOKEZO - Responded - Taarifa Binafsi zinakusanywa na "Kampuni za Mikopo Mtandaoni" ni Hatarishi kwa Faragha ya Mtu

3) KERO - Nakerwa na mikopo ya mitandaoni hasa inayotolewa na Kampuni ya EasyBuy

4) Polisi yakiri changamoto za Mikopo Mtandaoni, TCRA yajiweka kando yasema "haituhusu"

5) BoT yakataza rasmi kampuni za mikopo mitandaoni kuchukua mawasiliano ya wateja ili kuwadhalilisha. Yatoa mwongozo mpya!

6) Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yaanika Application 69 zilizofungiwa kwa utoaji mikopo kidijitali bila leseni

7) Uchunguzi: Wakopeshaji wa mitandaoni hawajasajiliwa na BoT wala BRELA na uendeshaji wao umejaa vitendo vya udhalilishaji

8) BoT Inawatambua Wakopeshaji wa Mitandaoni Wanne Pekee!
 
Wakati unakopa, hiyo riba hukuonyeshwa?

Wakati unaruhusu hiyo app ya mkopo kuweza kupata contact za watu wako ulisoma ni namna gani watazitumia taarifa hizo? Au ulikuwa na mzuka wa kupata hiyo pesa bila kusoma masharti?

Ukisubiri benki kuu ama Ndugu Lameck Madelu akusaidie kufikiri kwenye vitu vilivyo ndani ya uwezo wako wa kiakili hapo wewe ndio tatizo.

BTW, I don’t assume my “obvious” is universal, I know common sense isn't common to every human being.
 
Kwakweli ni unyonyaji mkubwa sana unaofanywa na izo kampuni na haikubaliki popote pale!...

lakini na wewe ni mpumbavu, mjinga uliotawaliwa na tamaa ya pesa kwani ndugu kabla hujachukua hizo pesa ukusoma/kupewa maelekezo na je kwani vigezo na mashart si ulikubali mwenyewe kabla ujachukua pesa?

(bila shaka huna pesa ya kurejesia ndio maana na wao wanaanza kukuzalilisha na wewe unakuja kulia uku JF)
 
Back
Top Bottom