Kampuni za ujenzi barabara za mwendokasi zaomba kuongezewa muda wa kukamilisha mradi huo

Kampuni za ujenzi barabara za mwendokasi zaomba kuongezewa muda wa kukamilisha mradi huo

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, leo Jumatano Machi 26, 2025, ameongoza kikao muhimu kati ya viongozi wa serikali na viongozi wakuu wa kampuni za wakandarasi zinazotekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Nne (BRT4), madaraja pamoja na barabara nyingine nchini.

Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kufuatia ucheleweshaji wa miradi hiyo na malalamiko ya msongamano mkubwa wa magari katika maeneo husika.

Pia soma Waziri Ulega: Wakandarasi Mwendokasi Awamu ya Nne (BRT 4) wamekuwa wazembe kupita kiasi

Akizungumza baada ya kikao hicho, Waziri Ulega amesema mkutano huo ni mwendelezo wa hatua alizochukua baada ya ziara yake ya Machi 4, 2025, ambapo alikagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya BRT4 na kupelekea wakandarasi waliokuwa eneo la mradi kukwama na kushindwa kutoa majibu ya msingi kuhusu ucheleweshaji wa kazi, jambo lililopelekea kuitwa kwa viongozi wakuu wa kampuni hizo kutoka makao makuu yao nchini China.

“Tuna furaha kuwa leo viongozi wa kampuni hizo wamefika Tanzania na tumepata nafasi ya kuzungumza nao. Wameeleza changamoto zao, ingawa hazilingani na muda mwingi uliopotezwa. Hata hivyo, tumeweka ahadi mpya za kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa,” alisema Waziri Ulega.

Katika kikao hicho, makampuni mbalimbali yalifanya ahadi za kimaandishi kwa serikali kuhusu ukamilishaji wa miradi. Miongoni mwao ni kampuni ya Shandong, inayotekeleza ujenzi wa miundombinu ya BRT kutoka Mwenge hadi Tegeta.

Kampuni nyingine ni China Geo Corporation (CGC), inayojenga barabara ya kutoka Katikati ya Jiji hadi Mwenge na Mwenge hadi Ubungo kupitia barabara ya Sam Nujoma.

Katika hatua nyingine, Waziri Ulega ameweka mkazo juu ya ucheleweshaji mkubwa wa kampuni ya Shandong kwenye mradi wa barabara ya Omurushaka - Kyerwa. Viongozi wa kampuni hiyo wamekiri tatizo hilo na wameahidi kuanza kazi mwishoni mwa Aprili 2025, huku Waziri akipanga kufanya ukaguzi mwanzoni mwa Mei mwaka huu.

Kwa mujibu wa Waziri Ulega, mradi wa BRT4 unapaswa kukamilika ifikapo Aprili 30, 2025, lakini wakandarasi wameomba nyongeza ya muda wa miezi 12.

Kufuatia hilo, Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi inachakata ombi hilo kwa kuzingatia njia mbili: kuvunja mikataba au kuongeza muda

 
Back
Top Bottom