Mfiaukweli
JF-Expert Member
- Aug 30, 2018
- 5,636
- 8,779
Yes,kikubwa ufanisi na matokeo chanya.Kama hubani matumizi na kupunguza gharama halafu hakuna ufanisi ni bora kukubali kugharimia na kutobana matumizi ili kuwe na tija.
Safari hii wamekwisha!!
Umeandika nini hapa?Ulichoongea hukijui wala hauna uelewa nacho,,secta ya ukaguzi ni pana sana zaid unavyozan wewe.
Serikali imepunguza lakin haijaondoa na haiwez ondoa kamwe,
Serikali zote huwa na wakaguzi binafsi,
Alichokizungumza CAG ni sehem tu yakupunguza ila si kuondolewa.tender zipo nyingi na serikal haina ubavu wa kukagua mashirika yote..
Kiaje ladyred, si Kuna private companies kibao.Safari hii wamekwisha!!
Sina uhakika walaKiaje ladyred, si Kuna private companies kibao.
Seems una uhakika sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
Jana kuna mdau kaniambia kampuni karibu makampuni makubwa yote ya serikali yameandikiwa barua na cag kujulishwa kua watakua na wakaguzi wake na sio wa makampuni binafsi.Kuongeza idadi ya wafanyakazi kwa ajili ya kazi za miezi mitatu ilihali wewe utawalipa miezi 12 pamoja na lizizo ya mwaka nao si uamuzi sahihi. Kitu muhimu ilikuwa na Serikali kuingilia namna audit firm zinavyotoza ada zake za ukaguzi au kutumia zaidi kampuni ndogo na za kati.
NB: Nami ni mdau wa hizo kampuni za ukaguzi
Mkubwa sio kidogoNi msiba mkubwa!
Kuna makampuni yalikua yanatoa hadi 1.2b audit fee, sio hela kidogo hii.Sina uhakika wala
nasikia tu fee ya kukagua huko Serikalini ni kubwa sana
Yani hii sio habari njema kabisaa kwao
Private company ipi ama ngapi zina uwezo wa kulipa fee za milioni 500?!!
Tulipofikia Serikali imeacha wajibu wa kuborosha mazingira ya kufanya biashara badala yake serikali imekuwa msindani wa wadau wa sekta binafsi. Huko nyumba kutoka kazi wa ujenzi kwa makampuni binafsi haikuwa bahati mbaya; lengo lilikuwa kujenga uwezo wa kampuni binafsi. Leo kijana ukimwambia achukue PCM aje kuwa Engineer tayari anafahamu kinachoendelea kwenye hiyo sekta na jibu lake ni kuwa kazi zote zinafanywa na serikali.Jana kuna mdau kaniambia kampuni karibu makampuni makubwa yote ya serikali yameandikiwa barua na cag kujulishwa kua watakua na wakaguzi wake na sio wa makampuni binafsi.
Makampuni au taasisi kubwa kama BOT, mifuko ya hifadhi za jamii, Ewura, REA, Tanesco, Tpdc, Airtanzania, Tanapa, Ncaa, vyuo vikuu na kadhalika sasa yanakaguliwa moja kwa moja na wakaguzi wa cag.
Ni msiba mzito kwa kweli kwenye ajira za haya makampuni.