Zanzibar 2020 Kamwe Joni hawezi Kusafiri na Hussein kwenda nae Zanzibar, ila atasafiri na Makame ambaye si tu amemzoea bali pia anammudu sana

Hongera kwa kueleza hilo
Naunga mkono

Nilisikia kuwa hussein kagomea uwazir tangu march hivyo vikao vyote na wizaran haendi sikuhizi, nadhan zitakuwa na ukweli

Mpaka sasa joni anaoption nyingine ya act
sababu ni ipi?
 
Kwanza Hussein alikimbia JKT kwa mujibu wa sheria, tuanze na hilo, na hilo liliwezekana kwa sa avu baba yake ni raisi. Ilipaswa asipewe hata dhamana ya kuwa waziri wa mambo ya majeshi
  1. Hili siwezi lizungumzia, maana kupitia JKT kwa mujibu wa sheria sio miongoni mwa sifa za kugombea urais wa JMT or Zanzibar.
  2. Nakiri kuwa japo kupitia JKT kunaongeza uzalendo na ukakamavu!, hakuna uthibitisho wowote kwa wale wasiopitia JKT sio wazalendo au sio wakakamavu.
  3. Mimi mwenyewe nilipita JKT kwa mujibu wa sheria, kisha nikaunganisha na JWTZ, lakini nilikuja kutokomea Ughaibuni, wakati kuna watu kibao walijongo JKT ni wazalendo kuliko mimi.
  4. Kuna watu kibao walipita JKT ni wavivu, wazembe, na ndio mafisadi wakuu, ndio walarushwa wakuu ndio mamluki wakuu, na kuna ambao hawakupita JKT ni wazalendo, wachapakazi na waadilifu.
  5. Conclusion: Kutokupitia JKT sio hoja, sio kigezo, sio sababu!, tafuta kosa jingine au sababu nyingine yenye mashiko ya why not, lakini sio hii!.
P
 
Duh...!.
P
 

Hiyo siyo hoja
Kama ueledi wa kazi ungekuwa ndiyo kipimo cha kupewa majukumu basi isingetungwa sheria wakati huo mtu usiajiriwe popote kama hukupitia JKT au umedoji JKT.

Hussein kuna kila dalili kuwa alikimbia JKT kwa sababu hakuwa kwenye position ya kusuffer consequences kutokana nababa yake kuwa rais wakati huo.

Linganisha Hussein Mwinyi na Makongoro Nyerere mtu ambaye alikwenda vitani Uganda wakati baba yake ni rais,
Hussein alikimbia JKT kinyume cha sheria halafu leo tunataka kumfanya kamanda wa vikosi maalum vya Zanzibar na pia kuwa mpigiwa saluti na vyombo vya usalama kama raisi wa Zanzibar.

Kama kwenda JKT wakati huo ni kielelezo cha uzalendo basi Hussein Mwinyi siyo mzalendo maana hata kwenye reserve army hayumo tofauti na wote waliopitia huko.
Sasa unataka kumpa uraisi mtu aliyekimbia kujinoa ili. kuwa mlinzi wa akiba wa Taifa lake?
 
Si yupo pale lumumba mkuu..!? Au kwani ni lazima uende kwake? Mbona wengine hivyo vipeperushi wanavichukulia mashinani au ndio unataka kiki..!??

...lakini ujiandae kushikiwa akili na kuanza kuongozwa na remote!
Lazima awe Polepole for strategic reasons, kideo kiwepo, na kushika mike ili kuchana kidogo, na kuwapaka sana wapinzani ili kuonyeshea wewe ni asset, ili iwe rahisi kupenya ile chekecheke ya vikao vya uteuzi!.
P
 
ccm ni ukoo wa panya hakuna mwema hata mmoja wanatofautiana tu KIWANGO NA MBINU ZA USHETANI
 
Alikuwepo anaongea lugha gani na hao wazungu?
 
Duh...!. Kwa vile Tanzania tuna majeshi ya aina mbili ya Ulinzi na Usalama, mtu anaweza ku dodge JKT lakini akawa recruited 'kule'!.
Kitendo cha ku hold hiyo wizara tuu for all this time, (the longest serving), ni uthibitisho huyu sio mtu wa 'mchezo mchezo'!.
P
 
Huyo mzee amekuwa ni kero sana

Ukweli mzee hapo mwanzoni alikuwa icon ya salama, amani na kisima cha hekima lakini kadri siku zinavyooenda naye anadidimia na kusidi kukorogeka
 
No hajakurupuka bali ni mmoja wa vilaza tuu waliotamalaki humu jukwaani.
P
 
Kwa kipindi tulichopo kuelekea Uchaguzi Mkuu kila kitu kinajadilika.
Kwa hali ilivyo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Kijani : - ana influence ndogo sana kuhusu nani awe mgombea wa chama hicho huko Visiwani.
Anaweza akatoa ushauri lakini kwa kuzingatia miaka iliyopita naona ushawishi wake ni mdogo sana.

1. Mtoto wa Mzee Mwinyi - haonekani kuwa ni sehemu ya Visiwani, najua ilikuwa ni hatua za kisiasa kumpa jimbo kule Visiwani baada ya kutoka Pwani (wanaofuatilia siasa kuanzia 2000 watajua ninachosema). Kinachomlinda Zanzibar ni "influence" ya baba yake tu. Sio mwanasiasa mkongwe Zanzibar na hana marafiki kule kutoka kwa wenye nchi yao.

2. Profesa Makame aliyehudumu na bado anayehudumu kwenye Wizara mbalimbali za Muungano: huyu pia sio mwanasiasa kigogo huko Visiwani, kama isingekuwa mzee wa Msoga kumpa Wizara basi huyu hakuna ambaye angemzungumza kwa sasa. Ni kiongozi mzuri na presidential material lakini anahitaji "back up" kubwa sana kutoka Bara kwa kuwa ni Mpemba, visiwani watu wanataka Muunguja kwa sasa.

3. Shamsi Vuai Nahodha:- huyu atakuwa anajaribu bahati yake kwa mara nyingine tena. Kosa kubwa la kisiasa alilofanya baada ya kutoka kuwa Waziri Kiongozi kwa miaka 10 kutoka mwaka 2000 mpaka 2010 chini ya mtoto Karume ni kukubali nafasi ya uwaziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa chini ya mzee wa Msoga. Ile kashfa na kutenguliwa imempunguzia "influence" kubwa sana Zanzibar. Huyu naye alipata nafasi kubwa akiwa bado mwanasiasa mchanga na mwenye umri miaka 38 tu. Amebaki na historia tu ya miaka 10 iliyopita huku akiwa hana ushawishi wa kutosha. Inawezekana hakukuwa kisiasa na historia itabaki kuwa tu ni Waziri Kiongozi.

4. Hamadi Yusuf Masauni: mbunge wa Kikwajuni ambaye naye pia anatajwa sana siku za karibuni. Ila kiukweli hana umaarufu wala ushawishi ndani ya Chama cha Kijani, sio Zanzibar tu hata huku bara. Wengi wanamuona kama mtu mdogo sana kwenye siasa za Zanzibar kwa umri alionano pia miaka 46 anapambana na watu wenye umri mkubwa zaidi yake na ambao wana mizizi ndani ya serikali na chama. Huyu nafasi yake ni ndogo japokuwa katika siasa lolote linaweza kutokea.

5. Ali Abeid Karume: huyu anabebwa na jina la Karume na sio vinginevyo. Kwa umri alionao wa miaka 69 sioni Chama cha Kijani kikimpa nafasi ya kuwa mgombea wao huko Visiwani. Amekaa sana nje ya Tanzania kama Balozi na nafasi yake ya Uwaziri wa Vijana, Michezo na Utamaduni ni nafasi ya kusogeza siku lakini hana influence Zanzibar na hana nafasi.

Pamoja na yote haya ambayo nimeeleza, siasa huwa zina maajabu yake na kwa nchi zetu ambapo viongozi huwa hawaandaliwi lolote linaweza likatokea.

Naomba kuwasilisha.
 
Kila mara unarudia rudia Kumtaja Polepole ndiyo tukuone kuwa uko karibu nae sana na Viongozi Wakuu wa CCM au? Ujuha unakusumbua mno.
Duh...!, simtaji Polepole ili mnione namjua, namjua Polepole since when he was nothing hadi sasa he is something!. Primary nimesoma na mtoto wa Nyerere, Msasani tumecheza sana!. Tambaza darasa moja na mtoto wa Ben, na kuwa nae US, Ben akija New York, tunashinda nae pale Intercontinental ya Crowe Plaza!. UDSM nimesoma na Riz1 na ni close friend mpaka kesho!. JPM ni homeboy wangu, kila nikienda pande zile nafikia kwake and there was an incident ilimbidi Janet kuingia jikoni in person kuandaa menu fulani!.

Hivyo nawajua wote in person!.
Pia kwa mimi being in the media unajua what does that mean, kama ni lobbying uteuzi, ningeisha lobby kitambo!.

Kwa vile humu vilaza ni wengi, wanaodhani Pasco Mayalla ana lobby uteuzi, acha wadhanie, faraja yangu ni ma GT wa JF who can read me in between the lines!, vilaza wengi kwenye mabandiko yangu, wanaishia chaka!.
Pole.
P
 
Hakunaga msukuma mjanja ata kama ushaga enda ughaibuni still bado ni mshamba tu acha kujifanya unajua sana kama nkurunzinza
Kwa Wasukuma ushamba ni jadi yetu!, tena nikiwa Ughaibuni kuna familia nilikuta wamelowea huko hadi ugali wanakula kwa umma, mimi nilishindwa!, nakula kwa mkono!.
P
 
Lazima awe Polepole for strategic reasons, kideo kiwepo, na kushika mike ili kuchana kidogo, na kuwapaka sana wapinzani ili kuonyeshea wewe ni asset, ili iwe rahisi kupenya ile chekecheke ya vikao vya uteuzi!.
P

Basi sawa mkuu, ukipata access usisite kunitonya ili niungane na wewe, niwe angalao mpiga kayamba, naamini ukishamaliza kuchana njia itakuwa nyeupe kupita kwenye uteuzi! Hivyo basi kwa utaalamu wa kupiga kayamba na marimba nilionao na kwa namna nitakavyoutumia siku hiyo basi bila shaka nafasi ya kushika vile vi burufukesi hutosita kunipa ili sasa hata wakati utakapokuwa busy na vikao, makala na mabandiko yako nitakuwa nayapandisha hapa jf kwa niaba...
 
Mkuu Affinitytz, this is very good objective analysis, uchambuzi kama huu ni rarely sana siku hizi humu jf, vilaza wametamalaki

Prof. Mbarawa ni Presidential material! Tuwaspot na kuwagroom Presidential materials au tumwache tu yeyote awe?
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…