inasikitisha kuona kwa busara zetu au kwa ujinga wetu watanzania leo hii tuko tayari kupoteza nafasi hii hadhimu ya kujenga mwanzo mpya.
badala ya kujadiliana kuandika katiba tunabishana na katika kubishana kamwe hatuwezi kuandika katiba.
kama watanzania tumeshindwa kuwa kitu kimoja katika mchakato huu na matokeo yake ni kuuuvuruga mchakato mzima na kuelekea kuendeleza nchi yetu ambayo ni tajiri kwa rasilimali kuwa masikini kwa kipato.
binafsi simuoni mtanzania yeyote msafi wala simuoni mtanzania yeyote mchafu,
sote kutokana na mifumo tuliyoijenga huko nyuma ndio imetufanya tuwe hivi tulivyo leo.
kama ungekuwa kwenye nafasi ya yule unayemnyooshea kidole wewe leo hii bila shaka ungefanya yale yale na wengine wangekuwa wanakunyooshea vidole wewe. na kama huyu unayemnyooshea vidole angekuwa kwenye nafasi yako angefanya yaleyale unayoyafanya wewe.
kwa haya tunayaona yanatendeka kama ni mazuri au mabaya si ya kuzaliwa nayo mtu bali mazingira yanayomzunguka mtu ndiyo huyasababisha.
ni bora tuadhimie sote kujenga mazingira mapya, mwanzo mpya ili sote tuweze kusonga mbele.
tukubaliane sote kuwa mabaya au mazuri yaliyopita yametokana na sisi wote kwa kila mmoja kuchangia kwa kiasi kilekile lakini kutokana na mapungufu tuliyoyaona basi tujipange turekebishe wapi ili mambo yawe mazuri zaidi.
wapo wenye jaziba lakini ambao mazingira yakibaki vile vile au yakibadilika wakapewa nafasi watafanya mambo yaleyale au mabaya zaidi ya yale wanayoyanyooshea vidole leo. wapo wenye hofu kuwa pengine mambo yakibadilika wanaweza kugeuzwa mbuzi wa kafara lakini yawezekana wakitengenezewa mazingira tofauti wanaweza kuwa mazuri.
tusiwaache watu hawa wenye jaziba na hofu kubishana kutuharibia mchakato wa katiba kwa kila mmoja kuvuta kule anakotaka. kwa hofu yake au jaziba yake.
tunahitaji busara ya kutafuta muafaka wa kuelekea mbele na hapa ni yote ya nyuma tuchukue mchakato wa katiba mpya kuwa ni nafasi ya kutumia uzoefu wa kila mtu kujenga mazingira bora yetu sisi na watoto wetu.
kujenga watoto wetu katika kutafuta na kulinda haki zao ndio njia pekee ya kuwapa watoto wetu urithi bora katika dunia hii inayoelekea katika utandawazi.
tukiweka mambo yaliyopita katika mchakato wa katiba hii tunawarithisha watoto wetu umasikini na hapa mtu yeyote asidhani kuwa yeye peke yake anaweza kuwapa watoto wake utajiri kwani jamii hii isipokaa pamoja na kufanya mambo kwa pamoja huko mbeleni mambo yanaweza kubadilika kwa yule anayedhani kamwachia mtoto utajiri anakuta kumbe kamwachia bomu yule aliyekuwa amekata tamaa akapata neema. mfano ni mimi babu yangu alikimbia utumwa na kipindi hicho alijua amesepona tena sana na marafiki zake wakachukuliwa utumwani. leo hii mimi mjukuu wake ninaishi maisha ya shida katika nchi masikini lakini wajukuu wa rafiki zake wakiishi maisha ya angalau kule marekani. babu siku moja aliwahi kuniambia mjukuu wangu ningejua maisha ya leo yatakuwa hivi kwa jinsi ninavyoona ningejipeleka mwenyewe kuwa mtumwa na leo hii pengine ungekuwa mmarekani mweusi.
tuweke mifumo bora kuwajengea watoto wetu maisha ya baadae badala ya huko mbeleni katika mambo yetu haya ya makundi kutaka kujitengenezea mazingira huko mbeleni wajukuu zetu wakatamani mababu wangekuwa katika hali fulani.