Kamwe miti ya matunda ya kisasa haiwezi lingana na ya asili iwe utamu au kuzaliana

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Jf salaam

Huwa nashangaa sana mtu kuanza kuinadi hii miti ya kisasa akiiponda ya kienyeji (asili).

Ukweli ni kwamba miti ya matunda ya asili inazaa sana iwapo itatunzwa kidogo tu!

Na daima ni mitamu sana na mivumilivu mno katika Hali zote!

Hii yenu hii iliyoibuka hata nusu haiwezi fikia

Chukulia embe dodo asili linavonukia vizuri vile ule utamu wake!

Angalia mti unavyoweza kuwa mkubwa na kutengeneza kivuli Cha kutosha iwe kiangazi au masika!

Miti ya kisasa ubora wake ni kwamba inaiva Kwa muda mfupi tu na sio vingine.

Matunda sio matamu ladha ya kula Kwa hisia yaani unakula embe dodo huku ukivuta hisia za dodo asili ndo upate mzuka!
Miti ya kisasa inaozesha sana matunda.

Na kuhusu kuambiwa inazaa sana huo ni uongo. Inahitajika nguvu ya ziada mno kuitunza Ili ukupe mavuno mengi tofauti na asili ambapo wenyewe unategemea wingi wa maji tu ukupe kile unachohitaji.

Nilikuwa Kijijini nimeona mapapai hapo nyumbani umebeba mno na matunda ni makubwa.

Ikabidi niulize kwanza walisema ulijiotesha wenyewe yaani walikula mbegu wakatupa ovyo ukaota

Hayupo mtu aliyewa wahi shughulika kupulizia dawa za kujua wadudu au kumwagilia maji.

Matunda uliyo beba Hadi unavunja baadhi ya matawi yake!

Nihitimiahe Kwa kusema iwapo mti wa asili ukiiutunza ukaweka na mjonjo unayofanya Kwa miti ya kisasa nakwambia mavuno utapata ni hakika sio miembe au mapapai.

IMG_20240427_144651_607.jpg
IMG_20240427_144756_987.jpg
IMG_20240427_144659_616.jpg
 
Ni kweli kabisa matunda asilia yana ladha yake na virutubisho vyake. Hili halipingiki hata kidogo.

Ila changamoto iliyopo kwa sasa ni ongezeko la watu na uhitaji wa matunda. Huwezi kusema usubilie embe la kienyeji msimu hadi msimu, wakati kuna biashara zinahitaji embe kila siku. Mfano parachichi linahitajika kila siku kwenye mlo haya viwandani.

Zamani tulikuwa wachache ila sasa tupo wengi na maarifa yameongezeka kikubwa tu ni kuangalia mbegu zipi na madawa yapi yatumike ili kuondoa magojwa ya hapo baadae.
 
Sikupingi mkuu

Tatizo ni muda mkuu ndio unafanya watu wakimbilie kupanda ya kisasa

Mnazi wa kienyeji unachukua miaka kuanzia 10 kuzaa wakati wa kisasa miaka miwili tu

Embe dodo asili ukipanda leo wataanza kuvuna wajukuu zako
 
Jf salaam

Huwa nashangaa sana mtu kuanza kuinadi hii miti ya kisasa akiiponda ya kienyeji (asili).

Ukweli ni kwamba miti ya matunda ya asili inazaa sana iwapo itatunzwa kidogo tu!

Na daima ni mitamu sana na mivumilivu mno katika Hali zote!

Hii yenu hii iliyoibuka hata nusu haiwezi fikia

Chukulia embe dodo asili linavonukia vizuri vile ule utamu wake!

Angalia mti unavyoweza kuwa mkubwa na kutengeneza kivuli Cha kutosha iwe kiangazi au masika!

Miti ya kisasa ubora wake ni kwamba inaiva Kwa muda mfupi tu na sio vingine.

Matunda sio matamu ladha ya kula Kwa hisia yaani unakula embe dodo huku ukivuta hisia za dodo asili ndo upate mzuka!
Miti ya kisasa inaozesha sana matunda.

Na kuhusu kuambiwa inazaa sana huo ni uongo. Inahitajika nguvu ya ziada mno kuitunza Ili ukupe mavuno mengi tofauti na asili ambapo wenyewe unategemea wingi wa maji tu ukupe kile unachohitaji.

Nilikuwa Kijijini nimeona mapapai hapo nyumbani umebeba mno na matunda ni makubwa.

Ikabidi niulize kwanza walisema ulijiotesha wenyewe yaani walikula mbegu wakatupa ovyo ukaota

Hayupo mtu aliyewa wahi shughulika kupulizia dawa za kujua wadudu au kumwagilia maji.

Matunda uliyo beba Hadi unavunja baadhi ya matawi yake!

Nihitimiahe Kwa kusema iwapo mti wa asili ukiiutunza ukaweka na mjonjo unayofanya Kwa miti ya kisasa nakwambia mavuno utapata ni hakika sio miembe au mapapai.

View attachment 2977591View attachment 2977592View attachment 2977593
Hoja yako ni ipi? Maana kuna masuala haujayaweka sawa ni aidha hauyajui au unafanya kusudi kutoyajua.
 
Ni kweli kabisa matunda asilia yana ladha yake na virutubisho vyake. Hili halipingiki hata kidogo.

Ila changamoto iliyopo kwa sasa ni ongezeko la watu na uhitaji wa matunda. Huwezi kusema usubilie embe la kienyeji msimu hadi msimu, wakati kuna biashara zinahitaji embe kila siku. Mfano parachichi linahitajika kila siku kwenye mlo haya viwandani.

Zamani tulikuwa wachache ila sasa tupo wengi na maarifa yameongezeka kikubwa tu ni kuangalia mbegu zipi na madawa yapi yatumike ili kuondoa magojwa ya hapo baadae.
Una hoja ya kusikilizwa
 
Nina mparachichi wa kisasa hapa kwangu (maparachichi yake yanakua kama na vipele vipele kwa nje) umezaa tangu mwaka jana ila matunda hayakomai zaidi ya mwaka sasa. Hata nikiyachuma hayaivi! Tatizo ni nini?
Vipelepele ni parachichi aina nyingi zina hiyo outside texture. Yaweza kuwa Hass,fuerte au Pinkerton
 
Back
Top Bottom