Miaka ya nyuma, wakati nasoma O-level niliwahi kuwa na girl fulani kimapenzi. Kwakweli alikuwa ni mzuri, hii ilinifanya nivimbe Sana.
Mahusiano yetu yalikuwa vizuri kuanzia form one hadi form four, baada ya matokeo ya kidato Cha nne kutoka, Mimi nilikuwa nimefaulu, Ila yeye alifeli, basi Mimi nilienda advance yeye alibaki kitaa.
Hiyo haikuleta shida yeyote kwenye mapenzi yetu, wakati namalizia muhula wa mwisho form six, akanipa taarifa kuwa anaenda chuo Cha mipango DODOMA, Daaah, yaani alibadilika hata sikuamini aiseeh, unampigia hapokei na hakutafuti mpaka nimtafute mimi, akikosea anataka mimi ndo ninyenyekee kwake wakati namweleza, Mara status ambazo hazieleweki, mara picha akiwa kwenye ndinga kali.
Aiseeh niliumia sana,nilikuwa na mawazo muda wote, Ilinifanya nishindwe hata kuzingatia masomo yangu, Combie yenyewe ilikuwa Ni ngumu(PCB).Baadae niliamua kuachana nae, akamaliza hako ka course kake, akarudi kitaa, maisha yakampiga, jamaa wakampiga mimba bila kumuoa. Huwa nikimuona namsikitikia Sana.
Nilimpenda Sana, na hata sasa bado nampenda Sana tu, na sidhani kama nitakuja kupenda mwanamke mwingine kama jinsi ilivyo kwake,Ila ndoivyo siwezi kuwa nae, ingawa anaonyeha kila namna ya kujutia yake aliyonifanyia.Acha ibaki historia.