Kamwe! Usikate tamaa!

Mkuu ni Mungu tu hata siyo uwezo wetu.

Ila Kuna broo anasave 150,,000 kwa siku na bado ni WA kawaida Wala huwezi mdhania
 
Kinachokufanya usianini ni nini?
Story yako haina mpangilio
Kwanza hujasema huo mji uliokwenda ni mji gani?
Hujataja biashara gani.

Umekuja kukimbilia kusema unasevu hela kiasi flani hujaeleza matumizi ni kiasi gani ( operation costs) huwezi tu ukawa unasave pesa.

Kwenye story yako uliandika unafanya kazi na biashara nilipokuhoji unawezaje kujigawa ndipo ukaja na version nyingine kwamba unakijana wa kazi.

Haujataja bidhaaa unazouza na najua huwezi kuzitaja manake ni uongo
Mwisho acha kudanganya kifala fala
 
Mtu anayetaka ufafanuzi Mimi ni muwazi nitamfafanulia

Pengine akitaka nitampa Hadi location ili tu ajiridhishe,

Kwanini haujatoa ufafanuzi mapema kama sio chai?
Umetunga story moja ya hovyo Mimi naomba nitumie picha tu duka lako lilivyo Kwa ndani
 

Its too good to be true, hivi motivational za hovyo kabisa:

 
Mtu anayetaka ufafanuzi Mimi ni muwazi nitamfafanulia

Pengine akitaka nitampa Hadi location ili tu ajiridhishe,
Usifanye hivyo.

Hakuna faida ya kufanya hivyo

Mitandaoni humu huwezi kumridhisha kila mtu. Maadam wewe unajua kuwa stori yako ni ya kweli basi yatosha. Atakayepata cho chote cha kujifunza kutoka kwayo atafanya hivyo.

Wewe endelea kupambana mpaka siku moja huyo boya aliyekutelekeza stendi akikuona aone aibu!
 
Kuna mawili
1,kuamini
2, kupuuza,

Kwa hiyo
Ulitaka niweka data zote hapa kuanzia mji nilipo, kazi nayo fanya oparation coast ,ili muamini?
Hapana lengo langu siyo Hilo,
Lengo langu ni kuwatia moyo wale wenye kipato kidogo wasiache kazi ili wajiajiri Bali wajiajiri wakiwa kazini
 
Asante sana mkuu!!!
 
Tunajifunza kwa mifano halisia acha tantalila
 
Mimi hapa,ningependa ushee na sisi hiyo biashara na namna unasave
Nitashea kidogo tu
Niko katika eneo lenye baa, migahawa mingi, na majiko mengi ya kupikia na kuchoma kitimoto, pamoja na maeneo ya kuuza pombe na sigara. Eneo hili ni la shughuli nyingi sana, hasa wakati wa usiku.

Biashara yangu ni kuuza mahitaji yote ya jikoni, kama vile karatasi za aluminiamu, viungo vya jikoni kama vile sosu ya soya na viungo vingine, vinywaji baridi, pombe, sigara, gasi, voucha, nafaka, sabuni, na vifungashio vya plastiki na karatasi. Ninapokea malipo ya kifedha na pia ninanunua mafuta ya alizeti na kuuza kwa Lita 1 au nusu Lita.

Kwa sababu niko katika eneo ambalo wauzaji wengine wanauza kwa bei kubwa, mimi huwa ninauza kwa bei nafuu kidogo. Kwa kuuza vitu hivyo, ninapata faida ya asilimia 30% au zaidi, isipokuwa kwa mauzo ya gasi na voucha ambapo faida yangu ni ndogo kidogo. Ninaweka sehemu ya faida kando ili kuendeleza biashara yangu.
 
Nimekusoma! AHSANTE
 
Kwa kuongeza tu, ili kupata faida katika biashara hii, ni muhimu kutafuta vyanzo vya bidhaa kwa bei rahisi. Kwa mfano, unaweza kupata soy sauce dark kwa bei ya jumla ya 125,000 badala ya bei ya maduka mengi ya 145,000 kwa carton. Vilevile, Mama Sita inauzwa kwa 218,000 badala ya bei ya kawaida ya 232,000.

Kuna bidhaa nyingine nyingi ambazo zinaweza kupatikana kwa bei rahisi kwa kutafuta katika machimbo. Kwa kuongezea, ninauza wine na spirit kwa bei rahisi kuliko bar, ambayo inavutia wateja wengi kuja kununua kwangu kuliko bar hasa wakati wa usiku
 
wewe ni wa ku puuza kwani unaeleza vitu ambavyo sio vya kiuhalisia , kadanganye wajingawajinga wenzako pumbavu mkubwa wewe.
Sasa kwa hiyo story yako ambayo hata haieleweki unafikiria utamtia moyo nani. Halafu sijui watu wengine kichwani kwenu kuna matope na sio ubongo.
Unatumia muda mwingi kuandika upumbavu ambao haueleweki halafu unasema eti unawatia moyo watu.
You are rubbish
 
Humu hamna tea bila sugar kweli? Anyway Big Up.
 
So unahisi anakudanganya ili apate faida gani

Unamjua huyu jamaa wote hatumjui
. Nadhani tungejikita kwenye theme ya message ya jamaa kutokata tamaa mengine tumwachie yeye na mungu wake
 
"Nikaamua kumpeleka shule" Ada ya shule mjini si chini ya laki 5 kwa muhula, mshahara wako ni laki 1, ukijitahidi sana na biashara yako unapata laki 2, Na hapo unasema uliendelea na kazi yako na hiyo biashara unayohangaika kusave! Mbona hii chai haina tangawizi
 
Tena bado unasema ulikuwa na mfanyakazi ambaye unamlipa 🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…