Kamwe usiolewe na mwanaume asiyeweza kukulipia mahari

Umeolewa lini wewe hebu acha uhuni, mie ndio namalizia laki 5 nije kwa mzee stefano hapo.
Katika vitu siji kufanya basi ni kuolewa Mke wa pili.
Kama nikikosa mume kabisa ni kheri nisiolewe
 
Umenitia moyo sana kwa huu uzi, Ubarikie sana.
 
Mahari si mamilioni ya pesa kile mnachopatana ndiyo hicho hicho pia ni heshima kwa wazazi, hivi una binti zako 2, mmoja anatolewa posa mwingine anatolewa tu unazani yupi atapata heshima? Chochote kile kitolewacho ni mahari, usiache kumtolea mkeo mtarajiwa mahari hizo no baraka hata kwa mwenyezi Mungu!
 
Tukumbushe kwenye kitabu cha Mwanzo, nipe mstari ambao Adam alimlipia mahari Eva. Je Adam alimuoa Eva? Kama hakumuoa sisi andiko la kufungishana ndoa tuli 'google' wapi? Kama alimuoa, je, mahari alipeleka kwa nani?
 
Ñi asante tu hio mama, mbona inatosha kabisa. Ndio maana watu hu appreciate zaidi jamii ya kiislamu sababu hawana mambo ya complication. Mandazi sufuria 2 na ubwabwa mtu anachukua mke.
Sio mandazi sufuria 2 ni kilo 2 za unga wa ngano
 
Hata hao wa kutokulipa mahari wapo bhac
 
"Mahari ni zawadi au ahsante...." Ushaona wap unapangiwa zawad
Mtoa mada kwani Mahari ni nn?
 
MWANAMKE ANAYEPASWA KULIPIWA MAHARI NI BIKRA TU
Asiyeweza kulipia mahari asioe. Ni sawa ila ukumbuke hata wanaolipia mahari wanagongewa na wanaume wasiolipa mahari. Kamuulize Stamina atakupa majibu
Na wengi wanaojilipia mahari ndoa zimewatokea puani, wameishiwa kuuliwa tu, na kuteswa Hadi kuachwa walemavu, mwanaume asiyeweza kutoa mahari na asioe kabisa aisee mpaka awe vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…