Kamwe usiolewe na mwanaume asiyeweza kukulipia mahari

Kamwe usiolewe na mwanaume asiyeweza kukulipia mahari

Umeolewa lini wewe hebu acha uhuni, mie ndio namalizia laki 5 nije kwa mzee stefano hapo.
Katika vitu siji kufanya basi ni kuolewa Mke wa pili.
Kama nikikosa mume kabisa ni kheri nisiolewe
 
Ni kweli kabisa. Mahari ni ujumbe wa kuomba ridhaa ya kuishi na mtoto wa kike.

Mahari ni jambo lisilo na utata katika kulijadili. Unapopenda mtoto wa mtu usiogope kwenda kuomba ridhaa. Najua maisha ni magumu, unajiona hauna hadhi ya kwenda kwa wazazi wa mtu kuomba ridhaa ya kuishi na binti yao.

Mahari kwa asili yake si gharama ya kutoa kwenye mfuko wa mwanaume bali ni swala la familia ya mwanaume.... Wajomba na baba wadogo kwa wakubwa, makaka, baba na mama watajikusanya kisha watamsapoti kijana wao kwenda kuposa. Tatizo familia za siku hizi hazina ushirikiano na wazazi wanawaachia watoto wadeal na mambo yao on their own ndio maana majanga ni mengi.

Ukikosa msaada wa familia yako hata rafiki na jamaa wanatosha kukupa sapoti. Washirikishe waje kukusaidia kuipata mahari. Na mahari haitolewi yote ukiambiwa milioni hata laki tano unapeleka, sasa why ufeli?!

Toa mahari, kisha tuma wazee wawanong'oneze ukweni kuwa harusi itasubiri kidogo mnaendelea kujipanga.


Maisha ukiyachukulia kwa standard ya juu huwa ni magumu sana kuyaanza, ila ukiyachukulia kwa uhalisia yanawezekana sana na nimepesi. Usiogope kupambana kupata unachotaka. Washirikishe ndugu na jamaa wa karibu wakusaidie.
Umenitia moyo sana kwa huu uzi, Ubarikie sana.
 
Bibie ulweso [emoji3] Hata mzazi wa kiume anahitajika kupewa asante kwa kukumkuza mwanae na kuja kumsitiri ,kumpa heshima (kumuoa) binti yako



Mahari sio lazima pia not necessary, mahari ni makubaliano,nikiwa sina sio kigezo cha kutokuoa ukiamua kutoa toa, ukipanga usipokee pia sawa.ndo maana kwa dini ya kiislamu binti anataja mahari anayotaka mfano wengi wanataja msaafu tu basi ( kitabu cha dini kama Bible)kama mahari yake na anaolewa hutasikia shuka la mzee ,pombe ,batiki za bibi ,boksa za babu ,sjui mabeberu kumi na NNE wala hutoskia

Mahari mnaifanya overrated ,kwanza mahari ni utumwa ndo maana kuna kabila ukiolewa kwa n'gombe kazaa utaenda wachunga utaenda tumikishwa ,ukizaa watoto wa kiume unawaletea umaskini kabila hili upendelea watoto wa kike kama mtaji hayo makabila ya tz na wanajijua sitaki ubaguzi so sitawataja [emoji3]

Miaka ijayo tutaoa bila mahari mark my words bado dunia inazunguka
Mahari si mamilioni ya pesa kile mnachopatana ndiyo hicho hicho pia ni heshima kwa wazazi, hivi una binti zako 2, mmoja anatolewa posa mwingine anatolewa tu unazani yupi atapata heshima? Chochote kile kitolewacho ni mahari, usiache kumtolea mkeo mtarajiwa mahari hizo no baraka hata kwa mwenyezi Mungu!
 
Kamwe usiolewe na mwanaume ambaye hawezi kukulipia mahari. Sikuwahi kuona kwenye Biblia mwanaume aliyepewa mke bure.

Tena wengine mnajifanya kupenda sana, unalazimisha kuolewa na mwanaume ambaye hawezi kukulipia mahari. Wengine mnaenda mbali zaidi na kuwasaidia kulipa hizo mahari.

Ukiona umemsaidia kulipa mahari usishangae na huko ndani akakuachia majukumu yote ya familia.

Kama unampenda msaidie mambo mengine lakini ikifika muda wa kulipa mahari hiyo ngoma mwache aicheze mwenyewe, ikimshinda basi huyo hakufai.

Kwanini hakufai??

Hakufai kwa sababu suala la kuoa siyo surprise ni suala la kujiandaa. Kama mchumba ameweza kununua mahitaji yake yote, atashindwaje kukulipia mahari!?!

Binti nakwambia usije thubutu kujifanya unamsaidia mwanaume kulipa mahari, hilo ni lake. Ukimpa mahari ujue umejioa mwenyewe dada.

Na wale vijana mnaolipiwa mahari na wazazi wenu pia siwaelewi jamani. Usije ukashangaa mke anakuwa wa ukoo, wao ndiyo wanamcontrol na hauwezi kufanya jambo bila wao.


Na
Winnie Kilemo
Tukumbushe kwenye kitabu cha Mwanzo, nipe mstari ambao Adam alimlipia mahari Eva. Je Adam alimuoa Eva? Kama hakumuoa sisi andiko la kufungishana ndoa tuli 'google' wapi? Kama alimuoa, je, mahari alipeleka kwa nani?
 
Ñi asante tu hio mama, mbona inatosha kabisa. Ndio maana watu hu appreciate zaidi jamii ya kiislamu sababu hawana mambo ya complication. Mandazi sufuria 2 na ubwabwa mtu anachukua mke.
Sio mandazi sufuria 2 ni kilo 2 za unga wa ngano
 
Hata hao wa kutokulipa mahari wapo bhac
 
MWANAMKE ANAYEPASWA KULIPIWA MAHARI NI BIKRA TU
Asiyeweza kulipia mahari asioe. Ni sawa ila ukumbuke hata wanaolipia mahari wanagongewa na wanaume wasiolipa mahari. Kamuulize Stamina atakupa majibu
Na wengi wanaojilipia mahari ndoa zimewatokea puani, wameishiwa kuuliwa tu, na kuteswa Hadi kuachwa walemavu, mwanaume asiyeweza kutoa mahari na asioe kabisa aisee mpaka awe vizuri
 
Back
Top Bottom