Kamwe usiolewe na mwanaume asiyeweza kukulipia mahari

Mimi mahari yangu inapangwa na wazee.
Huo ni mfano,wa utumwa....zaman watumwa walikuwa wanauzwa kwa mfumo huo...mtumwa ni bidhaa anapangiwa Bei na boss wake/ muuzaji.

Samahan kwa mfano huo...panga mahari yako mwenyewe ile ni haki yako kumbuka ukiolewa mnakuwa mwili mmoja.
 
Mahari ni heshima sio DAI, ili iwe DAI awe msichana KIGORI......hebu tujiulize, mahari ndio inajenga ndoa imara?...mahari sio ya kulazimishana...
ukilazimisha ni sawa we exchange parcels........
 
Labda niweke mambo sawa. Mahari ni lazima kutolewa yote lakini suala la kulipwa vipi haija fungamana kisheria.

Kama kweli una mpenda bwana ako unaweza msaidia kiasi kidogo cha fedha ili aweze kukuoa. Ukisema alipe yeye tu wakati mahari ni kubwa utakosa mume. Mfano hai, hao wana jinadi kusema mahari yake 500m unadhani nani ataoa huyo mwanamke.

Kama baba mzazi anaweza kukulipia balance ilo bakia mbona hakuna tatizo.

Ukienda huko India mwanamke anatoa yeye mahari. Kwahyo wasiolewe.
Na mahari siku zote lazima iendane na mioaji mwenyewe. Kama familia hamtaki iseme mapema kuliko kupotezeana muda
 
Ngoja nikuzomee,hiloooooo!!!!,Wakati mimi nilipewa bure kabisa,nilichoambiwa ni kwamba nikaishi naye vizuri tu na leo hii ni mwaka wa nane(8).Nakuzomea tena,hilooooo!,hiloooo
 
Mkuu Sam, hapo kwenye kujipang ndio huwa hawataki kupasikia, hua wanaliza Unajipanga wewe umekua matofari ??
 
Mahari ni heshima sio DAI, ili iwe DAI awe msichana KIGORI......hebu tujiulize, mahari ndio inajenga ndoa imara?...mahari sio ya kulazimishana...
ukilazimisha ni sawa we exchange parcels........
Hata kwa huyo Kigoli.

Ukiweka mahari tu, unamuuza kama nyanya.

Kama ni heshima familia ya mwanamme mbona haipewi mahari? Yenyewe haistahili heshima?
 
Hata kwa huyo Kigoli.

Ukiweka mahari tu, unamuuza kama nyanya.

Kama ni heshima familia ya mwanamme mbona haipewi mahari? Yenyewe haistahili heshima?
so tukubaliane hakuna haja ya MAHARI.....
 
so tukubaliane hakuna haja ya MAHARI.....
Kama mwanamke anataka mahari kuna haja ya mahari. Katika kumuoa yeye.

Kama anataka kuolewa kanisani, hutakiwi kumlazimisha aolewe msikitini.

Hilo halina mjadala.

Ila, mahari inafanya mwanamke awe bidhaa. Ananunuliwa kwa bei. Bei ndiyo mahari.

Ndiyo maana jamii zilizotuzidi katika usawa wa binadamu, hakuna hqbari ya mahari.

Jamii zetu zimeweka mahari, kwa sababu mwanamke ni kama mali ya mwanamme.
 
Tutaazimia kwenye kikao chetu WANAUME..........kwanza hata kabla ya hilo la mahari keshakuchunaaaa weeee.......halafu eti mahari..........
............#No MAHARI#..........................
 
mambo binafsi hayo usiingilie mapenzi ya watu huwezi jua wamekubaliana nini??hahaaaa[emoji2956] umenikumbusha issue ya mabeste
 
hiyo laki tano iliyobaki inakuaje unailipa au ndo imetoka
 
hivi kiranga wazungu na black americans wana utaratibu wa kutoa mahari?
Marekani kwa mfano, wao sehemu nyingi huwa hawalipi mahari wanapooa, wanalipa wakati wa kuachana, inaitwa "alimony".

Na aliye na kipato zaidi anamlipa asiye na kipato zaidi.

Kwao ndoa kituo cha polisi, kuingia bure, kutoka unalipia.
 
huko inaonekana hakuna mfumo dume
 
Mimi ni nani mpaka nishindwe kulike comments nzuri kama hii
 
Kumbe nawewe hua unaongea point..naonaga unaparaganya na Cariha TU[emoji3][emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…