Kamwe usiolewe na mwanaume asiyeweza kukulipia mahari

Kamwe usiolewe na mwanaume asiyeweza kukulipia mahari

Kamwe usiolewe na mwanaume ambaye hawezi kukulipia mahari. Sikuwahi kuona kwenye Biblia mwanaume aliyepewa mke bure.

Tena wengine mnajifanya kupenda sana, unalazimisha kuolewa na mwanaume ambaye hawezi kukulipia mahari. Wengine mnaenda mbali zaidi na kuwasaidia kulipa hizo mahari.

Ukiona umemsaidia kulipa mahari usishangae na huko ndani akakuachia majukumu yote ya familia.

Kama unampenda msaidie mambo mengine lakini ikifika muda wa kulipa mahari hiyo ngoma mwache aicheze mwenyewe, ikimshinda basi huyo hakufai.

Kwanini hakufai?

Hakufai kwa sababu suala la kuoa siyo surprise ni suala la kujiandaa. Kama mchumba ameweza kununua mahitaji yake yote, atashindwaje kukulipia mahari!?

Binti nakwambia usije thubutu kujifanya unamsaidia mwanaume kulipa mahari, hilo ni lake. Ukimpa mahari ujue umejioa mwenyewe dada.

Na wale vijana mnaolipiwa mahari na wazazi wenu pia siwaelewi jamani. Usije ukashangaa mke anakuwa wa ukoo, wao ndiyo wanamcontrol na hauwezi kufanya jambo bila wao.

Na
Winnie Kilemo
😀😀 Win, wakati ww una sema ivyo na sisi wanaume tunasema katu usilipe mahari yote kwa mwanamke kanjanja lisilo jua majukumu yake
 
Ni kweli kabisa. Mahari ni ujumbe wa kuomba ridhaa ya kuishi na mtoto wa kike.

Mahari ni jambo lisilo na utata katika kulijadili. Unapopenda mtoto wa mtu usiogope kwenda kuomba ridhaa. Najua maisha ni magumu, unajiona hauna hadhi ya kwenda kwa wazazi wa mtu kuomba ridhaa ya kuishi na binti yao.

Mahari kwa asili yake si gharama ya kutoa kwenye mfuko wa mwanaume bali ni swala la familia ya mwanaume.... Wajomba na baba wadogo kwa wakubwa, makaka, baba na mama watajikusanya kisha watamsapoti kijana wao kwenda kuposa. Tatizo familia za siku hizi hazina ushirikiano na wazazi wanawaachia watoto wadeal na mambo yao on their own ndio maana majanga ni mengi.

Ukikosa msaada wa familia yako hata rafiki na jamaa wanatosha kukupa sapoti. Washirikishe waje kukusaidia kuipata mahari. Na mahari haitolewi yote ukiambiwa milioni hata laki tano unapeleka, sasa why ufeli?!

Toa mahari, kisha tuma wazee wawanong'oneze ukweni kuwa harusi itasubiri kidogo mnaendelea kujipanga.


Maisha ukiyachukulia kwa standard ya juu huwa ni magumu sana kuyaanza, ila ukiyachukulia kwa uhalisia yanawezekana sana na nimepesi. Usiogope kupambana kupata unachotaka. Washirikishe ndugu na jamaa wa karibu wakusaidie.
Mungu akubariki kwa ujumbe huu, hakika umenitia nguvu sana.
 
DAS wa Taifa!✊✊✊
20201214.jpg
 
Wasoma Biblia wengi huwa wanafanya cherry picking.
Winnie Kilemo kuna vitu huwa anaandika huko facebook hadi namwonea huruma, wakati flani namwona kama mtu aliyekaa kwenye wokovu miaka mingi ila ni mchanga kwenye mambo ya kiroho (kifalme)

mi nadhani angeaza kwa kushauri wazazi kutopanga mahari kubwa sana , au angeshauri mabinti wanaoposwa wawambie wazazi wao kwamba mtarajiwa wangu hana uwezo kwaio msipange mahari kubwa!

Anyway, ukitumia biblia, anaetakiwa kulipiwa mahari ni binti kigori tu. ndivyo torati inavyoeleza. ukikuta sio kigori warudishie wenye mtoto nao warudishe mahari!
 
Back
Top Bottom