Ni kweli kabisa. Mahari ni ujumbe wa kuomba ridhaa ya kuishi na mtoto wa kike.
Mahari ni jambo lisilo na utata katika kulijadili. Unapopenda mtoto wa mtu usiogope kwenda kuomba ridhaa. Najua maisha ni magumu, unajiona hauna hadhi ya kwenda kwa wazazi wa mtu kuomba ridhaa ya kuishi na binti yao.
Mahari kwa asili yake si gharama ya kutoa kwenye mfuko wa mwanaume bali ni swala la familia ya mwanaume.... Wajomba na baba wadogo kwa wakubwa, makaka, baba na mama watajikusanya kisha watamsapoti kijana wao kwenda kuposa. Tatizo familia za siku hizi hazina ushirikiano na wazazi wanawaachia watoto wadeal na mambo yao on their own ndio maana majanga ni mengi.
Ukikosa msaada wa familia yako hata rafiki na jamaa wanatosha kukupa sapoti. Washirikishe waje kukusaidia kuipata mahari. Na mahari haitolewi yote ukiambiwa milioni hata laki tano unapeleka, sasa why ufeli?!
Toa mahari, kisha tuma wazee wawanong'oneze ukweni kuwa harusi itasubiri kidogo mnaendelea kujipanga.
Maisha ukiyachukulia kwa standard ya juu huwa ni magumu sana kuyaanza, ila ukiyachukulia kwa uhalisia yanawezekana sana na nimepesi. Usiogope kupambana kupata unachotaka. Washirikishe ndugu na jamaa wa karibu wakusaidie.