Kamwe usiolewe na mwanaume asiyeweza kukulipia mahari

Neno la MUNGU litasimama.
Mambo yote yatapita bali Neno litasimama...acheni kutaka kuhalalisha wake wengi kwa kisingizio hicho.

Hadi limeandikwa kwenye Bible ujue ni la kweli
kwani mimi nimesema si la kweli?......


mimi nimeongelea purpose ya hilo Neno, je limekuja kwa mtu mahsusi au kwa jamii yote?...... kumbuka Paulo huyo huyo amesema maaskofu wasiwe watu wanaopendelea kulewa (je ana maana wanywe kidogo?)
 
kwani mapenzi tumeumbiwa sisi tuu? ntaoa asiekua na wazazi wala ndugu ilimrad tu nisitoe mahari.

kwanza mwanamke usikukubali kutolewa mahari maana utakua unauzwa kama KUNTA KINTE
Kwamba asiye na wazazi na ndugu alijilea pekeyake?
Sasa hao waliomlea ndiyo wazazi wake utakaowapelekea mahari.
 
kwani mimi nimesema si la kweli?......


mimi nimeongelea purpose ya hilo Neno, je limekuja kwa mtu mahsusi au kwa jamii yote?...... kumbuka Paulo huyo huyo amesema maaskofu wasiwe watu wanaopendelea kulewa (je ana maana wanywe kidogo?)
Umehamia tena kwenye pombe??
Alijua madhara ya ulevi ndiyo maana akasema vile na akawaacha watumie busara zao.

Sasa kwanini uweke doubt kama unaamini ni la kweli?
 
Umesahau Mkuu na magunia 20 ya mchele jogoo 30 na suti mpya 10 kwa Baba njemba ikasepa binti akistuka mimba tayari! Acha kabisa wahuni!
Huyo uliyemnukuu alilipiwa mahari kiasi gani?

Kuna wazee wakuda wanataja mahari ndefu utadhani wanataka kupata mtaji wa biashara...

Sijui kreti mia za bia, ng'ombe kumi, mbuzi sijui wangapi...
 
Nasema hivi mahari inalipwa kwa mwanamke ambaye ni bikra Mosi hilo pili ukisoma bible waliolipa mahari hawakuoa mke mmoja. So jitathimin je ulifaa kulipiwa mahari kama ndo ingekuwa wew
Nafaa kulipiwa mahari na wala hakuna mwanamke asiyefaa kulipiwa mahari.

Hata unaowaona hawafai ni kwa sababu yenu wanaume..wanaume wa zamani hawakuwa fungua zipu hovyo..nyie wa siku hizi mnapanda ngano mkitegemea kuvuna mahindi!! We ulisikia wapi [emoji23]?
 
Kwa kweli la kwanza ni mimi kuokoka.
La pili napambana nipate hata bata wawili nilete nikuchukue.
Bata wawili??
Wallah[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]kuna mzazi atakubali kutoa mtoto kwa bata wawili??
Embu kuweni na huruma[emoji23]
 
Nikipata mtoto wa kike Mimi Kama baba naweza muozesha mwanangu bila mahari! Kikubwa yeye na mwenzake wanihakikishie kuwa wataishi kwa upendo na amani hiyo tu ndo itakuwa Kama mahari kwa binti yangu!.. mahari imeficha msingi wa ununuzi tu lkn inatofauti ipi ya kununua kitu..?
Kwani wazazi wa mwanaume wao hawajatunza mtoto wao..??

Mahari ni utamaduni tu uliowekwa ila sio lazima kuufata ni maamuzi ya mtu na mtu.. maana hata Adam hakutoa mahari kwa Eva!
Kila mtu na mtazamo wake na binafsi ndio naweza nikaoa kwa mahari ila sifikirii Sana kuja kuozesha mwanangu kwa mahari!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…