Kamwe usiolewe na mwanaume asiyeweza kukulipia mahari

Kamwe usiolewe na mwanaume asiyeweza kukulipia mahari

Huo u used umesababishwa na nini?
dah unauliza kwamba hujui?........

tazama, dunia hii hii, na nchi hii hii, na jamii hii hii, kuna mabinti wamejitunza na wakavuka kwa kishindo. do you think hao ambao hawajavuka salama wana any excuse?

kusema vijana/wanaume ndio wanawaharibu mabinti sio excuse ya binti kukubali kutumika!.....

ushauri wangu, kama umejitunza keep it, ukimsubiri mmeo, kama hujajitunza you better repent (God is faithfull will forgive you), then unamsubiri mmeo!.......
 
Jacob alichunga Mifugo miaka mingi tu.....ili aoe,
Labban( kama sijakosea) akampa Dada wa binti aliyekusudiwa, Jacob akasema anamtaka chaguo lake lile lile,
Akaambiwa achunge tena mifugo ili apewe huyo anayemtaka.
Jumla ya miaka unaweza fika 10, alitumia kuchunga mifugo ili aoe.
Hii ni adhabu tosha.
Hivyo ndivyo system iliwataka kufanya.
Siyo adhabu hiyo..kama ingekuwa adhabu basi angeacha tu.
 
Wahindi mwanamke ndie anaetoa mahari! Imekaaje! Hakuna anaestahili kulipa mahari, wote wametunzwa na wazazi wao. Ni kiasi tu cha kuachana na wazazi na kuambatana na mpendwa wako. Shukrani zitoka kwa pande zote mbili
Ni utamaduni wako.

Huku kwetu lazima mwanaume atoe mahari
Na ndiyo maana kuna mwanaume na mwanamke.. Hakuna wanawake tu
 
ila wewe unaongea vitu ambavyo huna uhakika navyo!

hivi awamu hii ya Magufuli unataka mahari kuanzia mil 2 unasema za kawaida? tena hapo bado mkaja wa mama, debe la mtama, mahindi, kuku, mbuzi, n.k n.k

kuhusu bikra mimi huwa sipendi kuongelea hili jambo, ila tafsiri ya mahari ni shukrani kwa wazazi wa binti kwa kumtunza binti yao vizuri, sasa kama binti hajatunzwa vizuri (sio bikra) unataka shukrani ya nini?

Saint Anne hivi unaelewa kwanini Mungu aliiweka bikra kwa mwanamke? au unaelewa kwanini Yesu alikaa kwenye tumbo la bikra?....... kama wewe ni mfuasi wa Kristo then unajua!

btw, mimi haya mambo ya bikra huwa sipendi kuyajadili sana,,,,,,........
Mimi nayaelewa vizuri na purity ni kwa wote na si kwa mwanamke pekee.

Mahari lazima mtoe kwa sababu hata wanaume si wasafi!!
Sitetei uchafu Ila naongea kilichopo.

Kitu gani nimeongea nisicho na uhakika nacho?
 
dah unauliza kwamba hujui?........

tazama, dunia hii hii, na nchi hii hii, na jamii hii hii, kuna mabinti wamejitunza na wakavuka kwa kishindo. do you think hao ambao hawajavuka salama wana any excuse?

kusema vijana/wanaume ndio wanawaharibu mabinti sio excuse ya binti kukubali kutumika!.....

ushauri wangu, kama umejitunza keep it, ukimsubiri mmeo, kama hujajitunza you better repent (God is faithfull will forgive you), then unamsubiri mmeo!.......
Tunapaswa kuwaonya vijana wote wa kike na wa kiume kujitunza.
Na si kuwanyoshea vidole watoto wa kike tu.
 
Una-discuss issue ya mahari,je huyo anayepaswa kutolewa hayo mahari anazo sifa za kukaa chini na washenga yakajadiliwa hayo.

Maana mabinti wengine wameshatumika kiasi mahari itabidi watoe baba zao na kuwapa asante wale vijana watakaosaidia kuchukua binti zao.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Shida sio mahari shida ni mahitaji yanayohitajika kwenye hiyo mahari, Ng'ombe 3, wanini? shuka la ba mkubwa, lanini? Jogoo wa babu,wanini? Sufuria ya kilo 7 ya shangazi,yanini? Zulia la MAMA,la nini? na pesa taslim Laki 7.

yani ukiangalia mahitaji unaona wanacheza mule mule kwenye vitu vyao vya kila siku walivyoona vimeisha sasa,wanataka mimi niwanunulie,ki ufupi ni kwamba Mahari ni swala la mke na mume washirikiane (ikibidi) unamuachia kila kitu mwanaume ndio ndani ya ndoa ANAKUMILIKI haswa

maaana katoa hela yake,hujui katoa wapi mahari yako ukute alikopa,aliiba,nk halafu unataka aamke akute hamna chai mezani lazima mueleze kwa herufi kubwa kwann mezani hamna chai,kwann hujamuandalia nguo,nk Kakununua kwa hyo uwe tyr kuishi kama bidhaa ndani ya ndoa yako.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ila kweli
 
Yaani baba zao watoe mahari??
Mke wa hivyo huwezi kupata mkuu
Kwanini nisipate?chukua nafasi ya baba bint yako ameshazalishwa na mjukuu unalea wewe na kila ukiangalia kulia na kushoto dalili kwamba binti atatulia hakuna muda wowote unaona kabisa hapa atakuja mjukuu mwengine halafu anajichanganya kijana kwamba nataka nimuowe huyu......

Unadhani utakuwa na muda wa kuandaa vikao na kuita ndugu mkae chini mjadili kuhusu mahari?i swear japo hutatamka asante kijana akaisikia ila kimoyo moyo na Mungu wako lazima utajisemea “asante sana kijana”,kwanza bint aliyeshazalishwa hairuhusiwi hata kwa bahati mbaya kukaa kujadili mahari na kama mimi ndiye nayetaka kumuowa nikisikia habari hizo wakikaa wakasema toa hata 50,000/= sitoi navunja uchumba.

Kuna nini humo cha kutoa 50K,kachukueni kwa aliyemzalisha na kumtoa bikra.
 
Kamwe usiolewe na mwanaume ambaye hawezi kukulipia mahari. Sikuwahi kuona kwenye Biblia mwanaume aliyepewa mke bure.

Tena wengine mnajifanya kupenda sana, unalazimisha kuolewa na mwanaume ambaye hawezi kukulipia mahari. Wengine mnaenda mbali zaidi na kuwasaidia kulipa hizo mahari.

Ukiona umemsaidia kulipa mahari usishangae na huko ndani akakuachia majukumu yote ya familia.

Kama unampenda msaidie mambo mengine lakini ikifika muda wa kulipa mahari hiyo ngoma mwache aicheze mwenyewe, ikimshinda basi huyo hakufai.

Kwanini hakufai??

Hakufai kwa sababu suala la kuoa siyo surprise ni suala la kujiandaa. Kama mchumba ameweza kununua mahitaji yake yote, atashindwaje kukulipia mahari!?!

Binti nakwambia usije thubutu kujifanya unamsaidia mwanaume kulipa mahari, hilo ni lake. Ukimpa mahari ujue umejioa mwenyewe dada.

Na wale vijana mnaolipiwa mahari na wazazi wenu pia siwaelewi jamani. Usije ukashangaa mke anakuwa wa ukoo, wao ndiyo wanamcontrol na hauwezi kufanya jambo bila wao.

Na
Winnie Kilemo

Kulipiwa mahari na mwanamke huo ni upuuzi grade A. Ndo matokeo yake unaanza kupapaswa matter call kwenye mahusiano.... Hilo TUNAKUBALIANA

hilo la pili la mahari kutoka kwa wazazi ni mambo ya mila. Sisi kabila letu ng’ombe wa mahari lazima atole kwenye boma la baba sio la kwako

Vivyo hivyo na kuna maneno pale mshua anayasema anavyokukabidhi kwamba kama nilivyokuozesha wewe na wewe una jukumu la kuwalipia wanao mahari ukoo wetu ukue. So ni mambo ya taratibu tu. Ndomaana hata vikao vya kupanga mahari bwana harusi haihusiki, na pia kutokana na changamoto za kiuchumi unamkabidhi baba mahari ndo anayeenda kukutolea kama zake(Kama mshua apeche lolo)

NB: vyovyote iwavyo point yako bado inahold, kama mwanamke akiona mume/baba watoto mtarajiwa hana hata uwezo wa kujilipia mahari manaake ni kwamba huo uzao wenu watashindwa hata kuoa nao(Ni jukumu lake). na kikwetu unatengwa na wanaume wenzako hata pombe kilabuni unakunywa kwenye kibuyu cha kwako,sio cha wazee wote sumtym hata viboko utachapwa
 
Kamwe usiolewe na mwanaume ambaye hawezi kukulipia mahari. Sikuwahi kuona kwenye Biblia mwanaume aliyepewa mke bure.

Tena wengine mnajifanya kupenda sana, unalazimisha kuolewa na mwanaume ambaye hawezi kukulipia mahari. Wengine mnaenda mbali zaidi na kuwasaidia kulipa hizo mahari.

Ukiona umemsaidia kulipa mahari usishangae na huko ndani akakuachia majukumu yote ya familia.

Kama unampenda msaidie mambo mengine lakini ikifika muda wa kulipa mahari hiyo ngoma mwache aicheze mwenyewe, ikimshinda basi huyo hakufai.

Kwanini hakufai??

Hakufai kwa sababu suala la kuoa siyo surprise ni suala la kujiandaa. Kama mchumba ameweza kununua mahitaji yake yote, atashindwaje kukulipia mahari!?!

Binti nakwambia usije thubutu kujifanya unamsaidia mwanaume kulipa mahari, hilo ni lake. Ukimpa mahari ujue umejioa mwenyewe dada.

Na wale vijana mnaolipiwa mahari na wazazi wenu pia siwaelewi jamani. Usije ukashangaa mke anakuwa wa ukoo, wao ndiyo wanamcontrol na hauwezi kufanya jambo bila wao.

Na
Winnie Kilemo
Kuna dada zangu ambao wakiona usiku unaingia anaamua kujipigia Assit mwenye na kufunga anafunga mwenyewe na wapo wengi siku hizi.
 
Back
Top Bottom