Kamwe usiolewe na mwanaume asiyeweza kukulipia mahari

Kamwe usiolewe na mwanaume asiyeweza kukulipia mahari

Kamwe usiolewe na mwanaume ambaye hawezi kukulipia mahari. Sikuwahi kuona kwenye Biblia mwanaume aliyepewa mke bure.

Tena wengine mnajifanya kupenda sana, unalazimisha kuolewa na mwanaume ambaye hawezi kukulipia mahari. Wengine mnaenda mbali zaidi na kuwasaidia kulipa hizo mahari.

Ukiona umemsaidia kulipa mahari usishangae na huko ndani akakuachia majukumu yote ya familia.

Kama unampenda msaidie mambo mengine lakini ikifika muda wa kulipa mahari hiyo ngoma mwache aicheze mwenyewe, ikimshinda basi huyo hakufai.

Kwanini hakufai??

Hakufai kwa sababu suala la kuoa siyo surprise ni suala la kujiandaa. Kama mchumba ameweza kununua mahitaji yake yote, atashindwaje kukulipia mahari!?!

Binti nakwambia usije thubutu kujifanya unamsaidia mwanaume kulipa mahari, hilo ni lake. Ukimpa mahari ujue umejioa mwenyewe dada.

Na wale vijana mnaolipiwa mahari na wazazi wenu pia siwaelewi jamani. Usije ukashangaa mke anakuwa wa ukoo, wao ndiyo wanamcontrol na hauwezi kufanya jambo bila wao.


Na
Winnie Kilemo

Kulipiwa mahari na wazazi kwa baadhi ya makabila ni tradition
 
Wahindi mwanamke ndie anaetoa mahari! Imekaaje! Hakuna anaestahili kulipa mahari, wote wametunzwa na wazazi wao. Ni kiasi tu cha kuachana na wazazi na kuambatana na mpendwa wako. Shukrani zitoka kwa pande zote mbili
Wahindi wajanja, mke anatoa mahari ili akienda kwenye ndoa akiwaza hela yake imuume aache ufara 😂😂😂 na wazee wamkazie kwamba tumelipa hela mbwa wewe hebu kaa kwa kutulia.😂
 
Una-discuss issue ya mahari,je huyo anayepaswa kutolewa hayo mahari anazo sifa za kukaa chini na washenga yakajadiliwa hayo.

Maana mabinti wengine wameshatumika kiasi mahari itabidi watoe baba zao na kuwapa asante wale vijana watakaosaidia kuchukua binti zao wakiwa na makopo ya vyoo vya stand katikati ya ya mapaja yao.
Duuh sentensi ya mwisho umezidisha maneno makali mkuu.
 
Hiyo 2m ni kutulisha upepo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mimi tangu dada zangu waanze kuolewa sijawahi ona vitu havijatolewa[emoji23][emoji1787][emoji23]
Vitenge,mashati,mablanket,viatu,yaani vitu Kama vyote
Na katika ununuaji wa hivyo vitu dada anaomuorodheshea shemeji kabisa[emoji1787]

Labda sijui kama utaratibu utabadilikia kwangu.
We tutakuoa kwa biblia tu
 
Sio kwamba hawana uwezo wa kulipa ila wengine wanathaminisha huyo mtoto wa kulipiwa hiyo mahari wanaona haiendani wanaamua kujifanya hawawezi.

Rafiki angu ashawahi ambiwa atoe mahari 4M. Alikimbia hakuwahi kurudi tena.
 
Neno la MUNGU litasimama.
Mambo yote yatapita bali Neno litasimama...acheni kutaka kuhalalisha wake wengi kwa kisingizio hicho.

Hadi limeandikwa kwenye Bible ujue ni la kweli
Wake lazma wawe wengi bana, hao watume wenyewe walikuwa na wake kibao.
 
Bata wawili??
Wallah[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]kuna mzazi atakubali kutoa mtoto kwa bata wawili??
Embu kuweni na huruma[emoji23]
Ñi asante tu hio mama, mbona inatosha kabisa. Ndio maana watu hu appreciate zaidi jamii ya kiislamu sababu hawana mambo ya complication. Mandazi sufuria 2 na ubwabwa mtu anachukua mke.
 
Kuna mmoja alichukua mpaka mkopo kabisa kampa bwana akatoe posa, kweli akazitoa lakini mpaka sasa walisha achana mwaka wa tatu huu na kamwachia mtoto 1
 
Mbona Isaka mpaka yule mwanamke Rebeca aliye muoa alitafutiwa na baba yake Ibrahim? Unasoma biblia gani? Kulipiwa mahari sio lazima kuwa muoaji ameshindwa kutafuta mwenyewe
 
"ukitumia biblia, anaetakiwa kulipiwa mahari ni binti kigori tu....... ndivyo torati inavyoeleza!.."
Ahaa
Wanao oa ni hao hao watoaji wa hizo bikira, unamtoa huyu ukimwacha anaoa mwenzio nawewe unaenda oa aliyetolewa na mwingine hakuna kulalama
 
Kulipia mahari kwa lugha kamili ya Kiswahili ni kununua mtu.
Sasa ole wako nikununue alafu ukumbuke kwenu! Nina mamlaka ya kuifanya bidhaa yangu niliyoinunua kwa pesa yangu vile nitakavyo
Mahari ni asante kwa wazazi, wewe unaweza nunua mtu kama ng'ombe? Hakuna kitu kama hicho.
 
Jacob alichunga Mifugo miaka mingi tu.....ili aoe,
Labban( kama sijakosea) akampa Dada wa binti aliyekusudiwa, Jacob akasema anamtaka chaguo lake lile lile,
Akaambiwa achunge tena mifugo ili apewe huyo anayemtaka.
Jumla ya miaka unaweza fika 10, alitumia kuchunga mifugo ili aoe.
Hii ni adhabu tosha.
Jumla miaka 14, ila chaguo lake alipewa baada ya kumaliza siku 7 , na licha ya kupewa aliambiwa amlipie miaka 7 baada ya hiyo ndiyo akaomba alipwe mshahara sasa, na ndiyo maana hakumpenda sana yule wakupewa kama karata tatu.
 
Mahari ni asante kwa wazazi, wewe unaweza nunua mtu kama ng'ombe? Hakuna kitu kama hicho.
Bibie ulweso [emoji3] Hata mzazi wa kiume anahitajika kupewa asante kwa kukumkuza mwanae na kuja kumsitiri ,kumpa heshima (kumuoa) binti yako



Mahari sio lazima pia not necessary, mahari ni makubaliano,nikiwa sina sio kigezo cha kutokuoa ukiamua kutoa toa, ukipanga usipokee pia sawa.ndo maana kwa dini ya kiislamu binti anataja mahari anayotaka mfano wengi wanataja msaafu tu basi ( kitabu cha dini kama Bible)kama mahari yake na anaolewa hutasikia shuka la mzee ,pombe ,batiki za bibi ,boksa za babu ,sjui mabeberu kumi na NNE wala hutoskia

Mahari mnaifanya overrated ,kwanza mahari ni utumwa ndo maana kuna kabila ukiolewa kwa n'gombe kazaa utaenda wachunga utaenda tumikishwa ,ukizaa watoto wa kiume unawaletea umaskini kabila hili upendelea watoto wa kike kama mtaji hayo makabila ya tz na wanajijua sitaki ubaguzi so sitawataja [emoji3]

Miaka ijayo tutaoa bila mahari mark my words bado dunia inazunguka
 
Ñi asante tu hio mama, mbona inatosha kabisa. Ndio maana watu hu appreciate zaidi jamii ya kiislamu sababu hawana mambo ya complication. Mandazi sufuria 2 na ubwabwa mtu anachukua mke.
Bata wawili?
 
Back
Top Bottom