Kanali aliyetoroka sasa aipasua kichwa JWTZ. Halihitaji Kutangazia UMMA wamefikia Wapi!

Aleyn

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2011
Posts
21,058
Reaction score
36,272
LUTENI Kanali Coelestine Seromba aneyedaiwa kutoroka ndani ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), bado hajulikani alipo hadi hivi sasa. Msemaji wa JWTZ, Meja Erick Komba ameliambia gazeti hili jana kuwa kazi ya kumtafuta Luteni Kanali Seromba inaendelea kimyakimya na kusisitiza kuwa suala hilo halihitaji kutangazia umma wamefikia hatua gani.

Komba alisema wanajeshi kadhaa walikimbia katika jeshi hilo lakini hawajatangazwa na wao kama jeshi hawaoni sababu ya kufanya hivyo kwani wana utaratibu wao. "Huyo Luteni Kanali Coelestine Seromba anayedaiwa kukimbia ni mwanajeshi mtoro kama wanajeshi wengine watoro na pindi atapopatikana atatiwa hatiani kama kanuni za jeshi zinavyosema," alisema Meja Komba.

Akijibu swali aliloulizwa na mwandishi wa habari hizi kuhusu kuchelewa kukamatwa kwa Luteni Kanali Seromba, Meja Komba alisema hatua za kumfuatilia si lazima zitangazwe na pia mahali lilipofikia jeshi hilo katika kumtafuta ni siri yao.

Meja Komba alisisitiza kuwa Luteni Kanali Seromba hakuondoka na nyaraka yoyote ya jeshi hilo wala vifaa vyovyote kama inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Komba aliwasihi waandishi wa habari kuzingatia maadili ya uandishi kwa kuandika habari za kweli na zenye tija kwa pande zote ili kutojenga chuki baina ya jeshi na taasisi zingine.

Alitolea mfano kuwa miaka ya hivi karibuni ambapo baadhi ya wanasiasa walitamka wazi kuwa jeshi hilo linakula bure hivyo hakuna umuhimu wa kutengewa bajeti kubwa huku wakisahau jukumu la jeshi hilo ni kulinda amani ya nchi na mipaka yake ili wananchi waishi kwa usalama.

Meja Komba alitoa mfano wa vurugu zilizotokea bungeni hivi karibuni kuwa kama Polisi wangeshindwa kudhibiti vurugu hizo hatua ya mwisho ilikuwa jeshi kuingilia kati, lakini watu wanadai wanajeshi wanakula bure. "Kikubwa ninachoweza kueleza hapa ni kalamu za waandishi kutumika vizuri ili kutoweka chuki kati ya taasisi zingine likiwemo jeshi letu nje ya nchi," alisema Meja Komba huku akigusia namna msuguano kati ya viongozi wa Tanzania na Rwanda ulivyoripotiwa.

"Mengi yaliyoripotiwa ni kama nchi hii na Rwanda zinaingia vitani na uhasama huo kuhamia kwa wananchi na kujenga chuki na baadaye kuchukiana na hata kuweza kugombana wenyewe kwa wenyewe," alisema.

Pia aliwakumbusha wananchi kuendeleza amani iliyopo kwani vita vina gharama kubwa na endapo nchi ipo vitani hata Bunge linaweza kusitishwa kutokana na fedha nyingi kupelekwa katika mapigano.

Chanzo kimoja kutoka ndani jeshi hilo kimesema kutoroka kwa Luteni Kanali Seromba aneyedaiwa kukimbilia Rwanda hakuwezi kuleta tishio lolote ndani ya jeshi hilo.

Pia taarifa zilizopatikana ndani ya jeshi hilo zinadai kuwa kitengo alichokuwa Luteni Kanali Seromba ni kitengo cha kawaida na kwamba mafunzo yake hutolewa kimataifa na kila nchi ina mtu kama huyo.

Source:
Jambo leo|Na Peter Ambilikile
 
duh hii kali tena,wapi Moshe Dayan utausaidie kuweka taarifa sawa hapa.Huyu Luteni Kanali alikuwa kitengo gani na amepata mafunzo gani?kama kuanza kuchimba mahandaki tujue mapema.

Hakuna haja ya kuchimba mahandaki.
 
duh hii kali tena,wapi Moshe Dayan utausaidie kuweka taarifa sawa hapa.Huyu Luteni Kanali alikuwa kitengo gani na amepata mafunzo gani?kama kuanza kuchimba mahandaki tujue mapema.
IT -Info technology
 
IT -Info technology
kwahiyo bwana Lt.kanali inaweza akawa amesepa na launch codes za mambo yetu yaleee na manini na nini.duh Mungu saidia apatikane.i wont feel safe till he is found either dead or alive
 
Kweli mkuu,,,baadhi ya vyombo vya habari vinapotosha sana wananchi nakuwaweka roho juu juu,,,wapo wengi sana wanaotoroka jeshi,,,na sababu ni nyingi,,mfano kujiendeleza kielimu, kupata dili inayolipa zaidi ya jeshi,,,nasababu nyingine zakibinafsi,,,,,vyombo vya habari vizingatie kanuni na maaadili ya kazi zao,,,big up sana meja erick komba.
 
kwahiyo bwana Lt.kanali inaweza akawa amesepa na launch codes za mambo yetu yaleee na manini na nini.duh Mungu saidia apatikane.i wont feel safe till he is found either dead or alive

Kama anaweza akae huko alipo kwa kufunga na kuomba kila siku, AKIKAMATWA ATAJUTA.
 
By tru rasta

duh hii kali tena,wapi Moshe Dayan utausaidie kuweka taarifa sawa hapa.Huyu Luteni Kanali alikuwa kitengo gani na amepata mafunzo gani?kama kuanza kuchimba mahandaki tujue mapema.


Hakuna haja ya kuchimba mahandaki.

HUJAJIBU SWALI MKUU RUDI KWENYE SWALI UJIBU UPYA AU WEKA MAELEZO YA ZIADA KWANINI TUSICHIMBE MAHANDAKI?
 
Kutoroka kwa wanajeshi wengi sio issue sana, issue ni:
Mwanajeshi gani katoroka?
Alikuwa na cheo gani?
Amepata mafunzo gani ya kijeshi?
Ni siri gani za jeshi inazifahamu?

Msemaji wa jeshi anasema ni wanajeshi wengi wametoroka,lakini umma haujatangaziwa, lakini kwanini huyu iwe big issue? kuna kitu hapa, na inawezekana jamaa kaondoka na nyaraka muhimu sana!
 
Kumbe polisi wngeshindwa Bungen jamaa wangeenda na mavifaru pamoja na siraha zingine......duh yaan ata mbunge wangu angepigwa....lazima tungeandamana.
 


Duh!
Soon tutaona VIfaru Bungeni,
naamini kama walikuwa bado hawaamini basi Bunge lijalo na hasa la mwaka 2015 wajiandae.
 

Mkuu, Ana Adam na Hawa kisha na nyota mbili. Ni Mkubwa sana Jeshini ndio maana Ishu imekuwa ni nzito.
 
Kumbe polisi wngeshindwa Bungen jamaa wangeenda na mavifaru pamoja na siraha zingine......duh yaan ata mbunge wangu angepigwa....lazima tungeandamana.

ukiandamana upigwe tu nasema tumechoka upigwe tu
 
Komba anakaribia kuwa kama nape, anasema usiongee halafu yy kutwa anadata na mic
 
Komba anakaribia kuwa kama nape, anasema usiongee halafu yy kutwa anadata na mic

Hebu huyu msemaji wa jeshi atuondolee upumbavu wake vurugu zitokee bungeni wao kama jeshi waende kufanya nini hivi anajua sheria za jeshi au kasomea journalism yake na kuwekwa ppale na ndg yake muimba kwaya ktpn msinzia bungeni, anapswa kufahamu kazi za jeshi ni nini na pia atambue kuwa wao wanawajibika kwa bunge na sio kuliwajibisha bunge ile ni taasisi huru na ni ya wananchi na ina sheria na taratibu zake na wao kama jeshi la wananchi ni wajibu wao kulinda mipaka ya nchi na kuwasilisha bungeni kupitia wizara yao ya ulinzi mahitaji na utekelezaji wa kazi zao kwa mujibu wa sheria ya jeshi la wanainchi, Mwisho anpaswa kutambua bungeni si mahala pa vita na pia wana askari wao nawao wanajua wajibu wao pale ni nini
 
JWTZ halina msemaji wabunge na vitambi vyao wanauwezo gani wa kufanya vurugu za kuishinda polisi kutuliza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…