Hili silioni kama tatizo, jambo ambalo halizungumzwi ni uhusiano wa JWTZ na Gen Nzeyimana, hiki ndicho chanzo cha matatizo. Nzeyimana ni sehemu ya Interharamwe ambao walihusika na genocide huko Rwanda, halafu huyu mtu anaalikwa Tanzania na JWTZ kwa mazungumzo ili JWTZ wawe na usalama mashariki mwa Congo, wakipigana na M23. Usalama wa Taifa wanawajulisha Rwanda kuwa Nzeyimana yuko TZ. Nzeyimana akamatwa na Rwanda. Baadaye Kikwete anataka RPF wajadiliane na Interharamwe (ambayo waliua watutsi million moja na hawajaomba msamaha au kuonyesha nia ya kujutia walichafanya) na huyu askari anatoroka. Mimi ninafikiri kuwa:
1. Paul Kagame hatuelelwi tuna nia gani na Rwanda, kwa vile tunajadiliana na maadui zake, halafu tuamjulisha halafu tunafukuza watutsi huko Kagera, jambo linaloashiria kuwa tunaendana na sera za Interharamwe.
2. Kikwete alikosea kumwambia Kagame ajadiliane na FDRL kwa kuwa hawa FDRL kama wangeweza wangeendeleza sera yao ya mwaka 1994 ya kuua watutsi, mfano mzuri ni ule kwa kumwambia Moshe Dayan azungumze na Hitler, wapi na wapi? Hata Afrika ya Kusini makaburu walikubali kuwa wamekosea kabla upatanishi haukufanyika. Hili swala halikuwa limefikiriwa vizuri.
3. Sana sana huyo askari alikuwa 'mole' wa serekali ya Rwanda na amepeleka ripoti nyumbani ya yale yaliyozungumzwa na Nzeyimana. Vile vile kwa kuwa Nzeyimana yuko Kigali 'anaimba' labda ni muhimu taarifa anazotoa zikaonishwa na kile kilichopo kwenye kumbu kumbu za Military Inteligence za JWTZ.
4. Wote tuajua kuwa JWTZ wanaaleji ya kupoteza askari katika shughuli za kulinda amani, inawezekana kuwa kwasababu hizi shughuli zinalipa wanapendeleana lakini hawana mpango wa kuumia kazini, chanzo cha kuhitaji kujadiliana na Nzeyimana.