Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
.Na ukumbuke pia huwa wanabaki na kopi za structure kwani ukiingalia filam ya "The raid to Entebe", '90 minutes to Entebe' walitumia ramani ya ujenzi ambao ndiyo wao walikuwa wajenzi na kuondoka na mateka wao kule Entebe.
.
Waisrael wakijenga, sio kwamba wanabaki na copy, bali wanaondoka na original, na hawakuachii copy ili ya maeneo muhimu ili major service uwaite wao tuu.
Ndio waliojenga Kilimanjaro na 77 Hotels, hawakuacha ramani muhimu za umeme na maji, mpaka leo 77, wanashindwa kuikarabati. Jamaa aliewekeza Kempinski alifumua kila kitu na kutandika upya.
.Nikiwa familiar ktk extent fulani kwenye mambo ya ujenzi na contracts zake, kwa ukweli kabisa haya madai unayoyaleta hapa ni ya kushangaza!
Ukiwa kama client unapoingia mkataba na consultant au mjenzi, ni shurti the entire consideration na schedules zake ziwe ktk maandishi. Sasa kama wewe client hukuwa makini ujue imekula kwako. Kama hukuandikishiana kupewa makabrasha ya mradi baada ya mradi kukamilika ni wazi mjenzi au consultant hana obligation ya kukupa, na ina mpa fursa ya kuendelea kula kwako kwa uzembe wako client na timu yako.
Hivyo kimsingi hoja yako ni VOID.
.
Nashukuru angalau kumbe uko familia na mambo ya ujenzi na contracts zake, nimeleta madai ya kushangaza, hivyo ni VOID!.
Swali ni dogo tuu kwako, ramani waliacha au hawakuacha?. Mimi nimezungumzia the end results, hazipo and this is a fact!. Void ni mimi niliyetoa facts hazipo, ama anaejua mkutaba unaosema ziwepo ili hali hazipo?
Which is which?
Waisrael wakijenga, sio kwamba wanabaki na copy, bali wanaondoka na original, na hawakuachii copy
.Nway sina muda wa petty discussions hata hivyo nitakusaidia kwa mara ya mwisho. Quick recap, Wewe umekuja na generalization kuwa Waisrael huwa hawaachi kopi etc na ukaenda kutoa specific examples za Kempinsky na 77.
To be precise maneno yako ni haya.
Hii sentensi imekaa kikijiwenikijiweni hivi, haina nafasi ktk fani muhimu kama ujenzi.
Nikakuelewesha kuwa ujenzi waenda kwa mikataba. Muulize mdau yeyote wa mambo ya ujenzi atakwambia the same. Hivyo chochote kinachotokea wakati wa ujenzi na baada ya ujenzi kinaamuliwa based on mkataba. Na hapo ndio hoja yako inapokuwa VOID kwa sababu kama hakumkukubaliana jambo fulani ni wazi huna haki ya kulidai. Na kama mlikubaliana na upande mmoja hautelekelezi hapo ndo mnahamia kwenye vyombo vya maamuzi, huko mbele ya pilato.
Natumai nimeeleweka.
.
Kwa kuanzia, nakiri, mimi ni mtoto wa kijiweni.
Hoja yangu ni pure simple fact kwamba Hawakuacha ramani!. Maadam ramani hazipo, hoja yangu ni still valid na sio void, unless uproove otherwise.
Hapa nasungumzia materials, physical documents, wewe unaniletea theory ya mikataba ya ujenzi.
Nakuuliza tena na tena, ili kukusaidia jibu ndiyo, hapana au sijui
Unajua zilipo ramani za ujenzi wa Kilimanjaro Hotel na 77 Hoteli?.
Inashangaza sisi ngozi nyeusi kujinasibu kwa tamaduni na dini za wengine na hata kufikia hatua za kuingiliana maungoni kutoana jeraha au hata uhai. Hii inashangaza sana.
Ni kwanini tujisikie kuguswa na uarabu au uyahudi zaidi badala ya tamaduni zetu na maisha yetu na mustakabali wa taifa letu?? Tutakuwa mateka hadi lini?? Kwa wale mnaosema Gaddhaffi haienezi uislamu nawasemehe kwa sababu hamjui mtendalo na mmetindikiwa maarifat au uelewa. Lakini kumbukeni, mfano huu. Jinsi wakoloni walivyorecruit askari kutoka ktk mataifa waliokuwa wakiyakalia kwa mabavu. Na wale watu eti leo hii wanaitwa 'mashujaa'! Yaani pamoja na mkoloni kuwatawala na kuwatenda vibaya sana, walikuwa tayari kuweka maisha yao rehani kwa ajili ya huyuhuyu mkoloni. Inasikitisha jinsi ngozi nyeusi isivyotumia akili. Inatia hasira.
Watu wamemsifu Ghadaffi kwa kusaidia Tanzania (mafuriko).Tukumbuke huyu jamani alimsaidia Muislamu mwenzake Idd Amin Dada alipovamia Tanzania.Tangu siku hizo sijamuamini kabisa.
Do you think kama Tanzania tungekuwa na uhusiano na state ya Israel angetusaidia?Kwa hiyo suala linakuja ,kwa nini nchi yetu mpaka leo,
tumeshindwa kuwa na ubalozi huko nchini Israel wakati walitoa mchango mkubwa sana katika ujenzi wa landmark buildings kama Kilimanjaro hotel etc?
Wewe hujawa na hutokuwa mwanajeshi ndo maana unasema hayo, ulitaka waanzishe uasi jeshini ili wauawe?? Kazi ya askari ktk jeshi ni kutii amri ya kamanda basi.
Sasa wakati huo jeshi lilikuwa la wakoloni na wale waliajiriwa kama akari na walilipwa mshahara si kwamba walitumikia jeshi bure. kama ni ukoloni hata wamamrekani, wafaransa nao waliwahi kutawaliwa sema tunatofautiana miaka ambayo tulitawaliwa.
Ethiopia haikutawaliwa na wakoloni je leo wako wapi?
Mhh, mshaanza ya Udini!
Je mbona Vatican haijasaidia lolote eneo lililokumbwa bna mafuriko ambalo lina Wakristo wengi?
Mbona hata makanisa ya ndani na nchi za "Kikiristo" hazijaamka na kuisaidia Tanzania?
Wait a minute, tunamchukia Ghadafi kwa kuwa ni Mwarabu, Muislamu au kwa kuwa alisaidia adui wakati tukiwa katika vita?
Mbona hatujakataa misaada yake yote tangu tumalize vita na Uganda?
ungetangulia kuwatuliza wale Wapalrstina waache kuwarushia mawe Waisrael wenye siraha kali harafu tuone, heeee heeee huwezi zuia mvua hata kama huipendi, hakuna mtu mwenye aridhi duniani Mnyaaz M'ngu hakumwekea mipaka mwanadamu ya kuishi,Wakiristo wangapi walisaidia na kuchangia ubaguzi southafrica? na pia kusaidia mapinduzi ya kijeshi na vita africa na bado tunauhusiano nao?
Tanzainia sio wajinga kuwa na uhusiano na nchi vamizi Israel lililovamia ardhi ya Palestina na kuvunja UN rosolutions za kumtaka aondoke ardhi ya Palestina, na watanzania sio cheap kwa sababu Israel wamejenga Kilimanjaro ndio tusiwakemee kwa unyama wao dhidi ya wapalestina.
Nadhani unabidi ufumbue macho na ujifunze au uulize, hapa JF hatutokuambia una mapepo kwa sababu ya kuuliza, uliza ujifunze!