Kanali Martini Mkisi kweli maisha ni gwaride

Hukuwaza Walioongoza jeshi wakiwa na vyeo wakati wa idd amini walivipataje?
Mimi zamani nilikuwa najua kwamba mwanajeshi hawezi kupanda cheo bila nchi husika haipo kwenye vita. Nilijua vita pekee ndo vinaweza kumpatia cheo mwanajeshi.
 
Ila hata huyu mbuge kabla hajaonekana na magufuli nasikia amesota sana na cheo kimoja kwa muda mrefu na kufanyiwa sana figisu hadi kuhamishwa ruvu
Majungu hayo

U'CO' mtu anahamishwa na Rais

Isitoshe alipanda kwenda ukanali mwaka 2017 au 2018 nadhani sasa Cheo cha Kanali ni cheo kikubwa sana ingawa ni Cheo cha mwisho kuwa CO kwa hiyo baada ya kupanda cheo pale ilikuwa lazima apewe majukumu mengine
 
Ndugu yangu MASAMILA, mbona umemkalia koo sana Jenerali Mbuge? Huyo keshaenda hivyo; kadri unavyomlalamikia ndivyo yeye anazidi kusonga mbele. Utashangaa kuwa ataweza kuwa Cheif of Staff labda baada ya miaka mitatu tu hivi, kwani General Mohammed karibu anastaafu, hasa ukikumbuka kuwa machief of staff wengi wa JWTZ hutokea kamandi ya JKT. Unaweza ukashangaa kuwa hata Mkisi anaweza kuwa anawashinda cheo maafisa aliomaliza nao kadeti wakati mmoja. Inaonekana kuwa umeumizwa sana na mafanikio ya Mbuge kuwa jenerali, lakini sasa achana na hilo kwani utakuwa unatoa kilio cha samaki tu, machozi yako yote yatakwenda na maji tu, hakuna atakeyaona kwani huwezi kumpangia kazi Amiri Jeshi Mkuu

Elewa kuwa siyo askari wote hupanda vyeo kwa wakati mmoja hata kama wana sifa zinazolingana. Kuna vyeo ambavyo hutegemea kitengo cha mtu; Mbuge kapanda haraka kwa vile alikuwa JKT na kamanda wa JKT alikuwa anastaafu. Kama Col Mkisi (sijui kama ni mtoto wa General Nelson Mkisi) amekaa sana na cheo kimoja huenda cheo alicho nacho ndicho cha juu kwenye kitengo chake. Na kama bado yuko kwenye siasa, ataendelea na cheo hicho mpaka pale jeshi litakapomrudisha kwenye active duty tena. Kapteni Mkuchika aliingia kwenye siasa akiwa kapteni na wala hajarudi tena kwenye active duty na amebaki kuwa Kapteni akiwa ni wa siku nyingi sana kuliko maafisa wote wa jeshi waliopo leo. Mwaka juzi Kanali Gaguti alipokuwa Mkuu wa Wilaya Buhingwe alirudishwa jeshini na kupandishwa cheo kuwa kuwa Brigadier General.
 
Kwenye ngazi za kijeshi zimepigwa sarakasi hapo maana sio fair junior umrushe juu ya seniors labda mabifu au utashi wa Jiwe Ila hamna namna
Niliwahi kumjibu mtu humu JF, kwenye jeshi; kuingia kwenye level za General (One star na kuendelea) ni suala la favor za amiri jeshi mkuu wa wakati huo, sio merits. Hata Mabeyo kawapita wengi tu mpaka kufika hapo. Ni favor za bwana mkubwa huko.
 
Niliwahi kumjibu mtu humu JF, kwenye jeshi; kuingia kwenye level za General (One star na kuendelea) ni suala la favor za amiri jeshi mkuu wa wakati huo, sio merits. Hata Mabeyo kawapita wengi tu mpaka kufika hapo. Ni favor za bwana mkubwa huko.
Hao waliopitwa na Mabeyo walipotelea majini tu sababu Mabeyo mwenyewe kapata umeja jenerali miaka 34 nyota ya Kwanza
 
Niliwahi kumjibu mtu humu JF, kwenye jeshi; kuingia kwenye level za General (One star na kuendelea) ni suala la favor za amiri jeshi mkuu wa wakati huo, sio merits. Hata Mabeyo kawapita wengi tu mpaka kufika hapo. Ni favor za bwana mkubwa huko.
Haloo ni kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…