Naona Kama inakuuma sana [emoji3][emoji3][emoji123]
Usilie kamanda ...ngangamara[emoji1787][emoji1787][emoji123]
Sent using
Jamii Forums mobile app
Kisa kakupinga ndo maana unaona inamuuma. Tangu nisome historia ya kijeshi sijwahi kuona kamanda yeyote wa miaka 30+ na early 40 akifanya maajabu kama hana experience. Ukisoma list ya WW2 mfano, Wehrmacht (jeshi la Nazi) lilikuwa na majenerali na Field Marshall wenye uzoefu na WW1 na umri wao miaka 40+ na 50+ uko. Kina Goeling, Heinz Gudelian, Desert Fox, Rundstedt, Kesselring na wengine wengi sana hawakuwa matoto madogo. Walikuwa watu wenye experience zao na hata Adolf Hitler alipigana WW1.
Britain walikuwa na PM wao mzembemzembe ambaye hakuwahi shiriki vita, nchi ilimshinda ikabidi wamchague Winston Churchill ambaye alishiriki WW1. Ukitaka kuona vita inataka experience, Churchill alipomaliza vita tu alishindwa uchaguzi mkuu kwakuwa hakuwa anajua chochote kuhusu uchumi wala maendeleo, still anarank top 3 ya PMs bora kwa Waingereza. Bado majenerali wao kina Montgomery hawakuwa watoto.
France hawa ndo mfano wa jeshi la kisiasa, walichaguliwa kipuuzi kabisa na Ujerumani ilipovamia wakakimbia mapigano. Majenerali walikuwa wapuuzi tu, mpaka badae msaada wa Mwingereza kina de Gaulle ndo wakaja kuipigania nchi. Hawa hawakuwa wa kisiasa wala watoto.
USA wao hawakuwa na experience na vita kumbuka WW1 hawakuhusika. Majenerali wao kina Omar Bradley na McArthur waliteseka kwanza ingawa tech iliwabeba mno, sana.
Kwa Warusi, huyo Stalin alifanya purges miaka ya 1930s akaondoa viongozi muhimu walioshiriki WW1 akaweka wale wa ndio mzee. Kilichotokea mwanzoni kwa vita tunakijua, Germany ilikuwa inawapiga kama watoto. Baadae ndo watu wenye experience zao na umri mkubwa kina Georgy Zhukov na Konstantin Rokossovsky walikuja kuwa game changer.
Uliona majenerali wa Japan, kina Admiral Yamamoto na Admiral Yamaguchi. Hawakuwa watoto wa kubebwa, walikuwa watu wenye experience sana.
Wewe ushawahi ona wapi majenerali wasio na uzoefu wanafanikiwa kwa kawaida. Kule Nigeria watoto ndo walikuwa wanawaza mapinduzi na ilipotokea Biafra ndo wakaonekana maandazi kabisa. Walikuwa wanapigwa na vijeshi vya kurecruit kutoka kirabuni.