Uzima Tele
JF-Expert Member
- Jan 20, 2023
- 1,270
- 2,822
Kwani kuna ubaya gani ikiwa timu moja machachari chini ya Captain Dr Wlbroad Slaa akisaidiwa na kina Wakili Mwambukusi na Mdude Nyangali ikaendelea na mipango yake ya kuliamusha dude kwa maandamano yasiyo na ukomo huko Mbeya, Arusha, DSM na Mwanza huku timu ya CHADEMA chini ya kamanda Freeman Mbowe, Tundu Lissu, John Heche and others nao wakishambulia kwa jeshi la ardhini na angani kwa mikutano ya hadhara huko kanda ya Nyasa?Hakuna anayesema ameingilia mikutano yao isipokuwa nani asiyejua nchi hii itakombolewa kwa maandamano na si majukwaani?
Kulundikana sehemu moja wote si mkakati mzuri wa mapambano!!
Waambie wenzako wasihofu wala wasiogope. Waambie wasonge mbele tu. Wananchi maelfu kwa maelfu watajitokeza na watawaunga mkono kwani hata wao wanakubali kuwa nchi hii inahitaji ukombozi wa pili na wakati huo ni sasa!!
...... lakini it must be done kwa kutumia mikakati bora na yenye tija. Huo wa kwenu na kina Dr Wlbroad Slaa na wenzake una shida na hila ndani yake.Magazeti au awaye yote atuhusu sisi nini wapi, kama hoja zetu ni kuikomboa nchi kutokea kwa adui anayejulikana?
........nikuhakikishie jambo moja kuwa, wakati na majira ya Mungu kuiangusha na kuifuta CCM umeshafika na ni huu. Na kwa kuwa ni wakati wa Mungu, watapigwa na kufa hata kwa kutumia kombeo tu!!
Asomaye na afahamu