Kangi Lugola: Rais Magufuli namfananisha na Yesu tofauti na Mbowe ambaye ni mlevi anayelewa Chako ni Chako

du yesu wa chato sijui ataishije bila kuabudiwa siku mfumo ukimtupa, salama pekee ni kufia madarakani.
 
Chezea kusamehewa makosa yake,pia huyo ni mwanafunzi wa yesu wa chato alikuwa ni Mwalimu wake,so kange atakuwa ndie batholomeo.

Kange ameamua kumtukana Rais na kumchonganisha na wakristo. Anapaswa Rais kwanza atume takukuru wamshike na wamsweke ndani pili atoe kauli. Hii akiifumbia itasambaa makanisani na sumu itakuwa mbaya sana . Kumbuka amechezea imani ya watu
 
Kange ameamua kumtukana Rais na kumchonganisha na wakristo. Anapaswa Rais kwanza atume takukuru wamshike na wamsweke ndani pili atoe kauli. Hii akiifumbia itasambaa makanisani na sumu itakuwa mbaya sana . Kumbuka amechezea imani ya watu
Hata siku moja ndio zinazomfurahisha.Sio Mara ya kwanza Wala ya mwisho hizi.Ukishazoea kuabudiwa sijui utaishije siku mfumo ukikutupa maana wakati ni ukuta
 
Unaamini Mwizi,Jambazi,Muuaji asiyeamini Yesu ni Mungu na UTATU ataingia peponi na yule mtenda mema anayeamini Yesu ni Mungu na UTATU ataingia motoni
Anaye amini UTATU pepo ni haramu kwake, vipi aingie peponi ?

Huyo mwizi,muuaji,jambazi unaweza kuniambia ataingia vipi peponi ? Kwa lipi ?
Kuliko kujitia umeshuka toka mbinguni unajua kinachoendelea kule kwamba imani fulani ni sahihi na imani fulani sio sahihi ni kheri ukafocus kwenye kutenda matendo ya kumpendeza Mungu unayemuamini.
Kujua yanayo endelea kule siyo lazima nitoke kule kijana, mangapi yaliyo pita tunayajua hali ya kuwa siai hatukuwa sehemu ya tukio husika au wenye kuhusika ? Hivi huwa mnafikri kwa kutumia nini ?

Hata akili ina kataa tu, haiwezekani Mola atuumbe halafu atuache tu tujiamulie tunayotaka katika njia kisha atulipe pepo, hili halipo, lazima tufate njia yake, na njia yake ni moja tu, tangu anaumba mbingu na ardhi.
Ila kama unaamini kule Mbinguni utaulizwa we Muislam, Mkristo, Muhindu au Budha sina comment nyingine.
Kuulizwa lazima uulizwe kijana, tena maswali yananzia baada ya kuzikwa tu.
NB : Kuamini Wakristo Wote wanaamini UTATU ni ujinga mwingine
Nani ameamini hilo ? Ukristo huwezi kuutenganisha na USHIRIKINA, kwa hali yoyote ile, kama hutaamini UTATU basi utaamini ya kuwa Yesu ni mwana wa Mungu au ni Mungu, usipo amini hivyo basi utaamini Yesu alikufa au alisulubiwa, au utaamini Yesu alikuwepo kabla ya kuumbwa dunia na vilivyomo, au utaamini ya kuwa Mola yuko popote, au utaamini ya kuwa Yesu anaponya, yaani hutoki.

Ahsante.
 
Hata siku moja ndio zinazomfurahisha.Sio Mara ya kwanza Wala ya mwisho hizi.Ukishazoea kuabudiwa sijui utaishije siku mfumo ukikutupa maana wakati ni ukuta

Siasa ni strategy, lowasa aliposema tu nataka niwe Rais kwasababu tangia nchi hii ipate uhuru hakujawahi kuwa na Rais mruthel hii ilikuwa ni mbinu ya devide and rule.


Kangi amesemwa sana na ameona amchafue mkuu kwa kumchonganisha na Wakristo.

Itazame kwa jicho la tatu. Leo zungukeni makanisani lazima itasemwa tu
 
Hivi watanzania ule utaratibu wetu wa kuapa kwa vitabu vya Mungu tunaushika kweli?
Mbona haya yanatokea na hakuna anaediriki kusema?

Yesu kristo Ni mwokozi wetu sore tulioamua kumfata na hafananishwi na binadamu.
inamaana umeshindwa kumtafakari kangi na kumuelewa ni mtu wa aina gani?? hebu achana na watu wanaotumia kichwa kama mfuniko wa mwili,
 
As per attachment
Tunakuomba Mungu uturehemu
 

Attachments

  • IMG-20200613-WA0033.jpeg
    112.2 KB · Views: 1
Wakati akiyasema hayo wagonga meza walio wengi walizigonga meza kushangilia hii kufuru.
Hapo ndiyo utaona jinsi tulivyo na bunge la ajabu.
 
Nna imani hii mkuu utaipinga,nakumbuka kuna sehemu kwenye bible kuna MTU alimuita yesu kwa Nina la mkuu mwema,then yesu akamuuliza kwanini mnaniita mwema? Akasema hakuna aliye mwema ila ni Mungu peke yake
 
Dini ya kikikristo inaonewa sana, nimeelewa kwanini waislamu wako strict na dini yao. Yaani Magufuli raia wa Chato unamlinganisha na Yesu! Ndo maana waislamu ukimtaja ovyo mtume wao unatangaziwa fwatwa. Lugola kawakosea sana wakristo. Hata kama yeye haoni yesu ni mtakatifu kwake asiwaingilie wafuasi wa Yesu katika Imani yao. Tunajua Lugola kwa mauno anayokata wakati muziki wa kidunia unapopigwa atakuwa anaamini zaidi wapiga ramli kuliko yesu.
 
Hujakosea kabisa

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Isaya 42: 8

8 Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu.
 
Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
___________
Kufuru haina kinga. Kwa Wakristo, dhambi isiyosameheka katika Agano Jipya ni kumkufuru Roho Mtakatifu. Na katika Agano la Kale ni ibada ya sanamu (idolatry). Amri ya kwanza aliyopewa Musa inasema, "Mimi ni Bwana Mungu wako, usiwe na miungu mingine" (Kutoka 20:3-6).
_
Kufuru haina kinga duniani wala mbinguni. Ghadhabu ya Mungu iko wazi katika vitabu vyake vyote.

Tuzitendee haki kumbukumbu zetu;

1. Mwaka 2005 mjinga mmoja alitumia uhuru wake vibaya huko Denmark. Akachora katuni yenye kumdhihaki Mtume Muhammad (S.A.W). Dunia nzima iliwaka moto.

2. Mwaka 2010 mpuuzi mwingine huko Marekani akachoma moto Quran tukufu. Hakuna jiwe lililosalia juu ya jiwe.

3. Mwaka 2012 huko Mbagala utoto ukavuka mipaka. Msahafu ukakojolewa. Amani yetu ilitoweka kwa muda. Majivu yakawa majivu.

4. Huko Sumbawanga, msimu wa uchaguzi kama huu, ulimi wa mmoja uliteleza. Akaufananisha UTATU mtakatifu na mafiga matatu ya chama chake. Hapakutosha. Mzee Pinda (mtu wa amani), ana cha kusimulia mpaka leo.

Mungu wetu hafananishwi. Mungu wetu halinganishwi. Mungu wetu hashindanishwi. Ni ibada ya sanamu kupenda kitu kingine kuliko unavyompenda Mungu wako. Ni ibada ya sanamu kuchukia kitu kingine kuliko unavyomchukia shetani. Ni ibada ya sanamu kumlinganisha Muumbaji na uumbaji wake.

Hatumtendei haki Mungu kumlinganisha na aliowaumba. Hatuwatendei haki wale tuwapendao kwa kuonesha kuwa tunawapenda kuliko tunavyompenda aliyewaumba.

Walinzi na waangalizi wa imani (viongozi wa dini), kama hatuwezi kukemea hili (la Lugola) basi angalau tuchukie na tuonekane kweli tumechukizwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…