Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha Padre Rwegoshora kufuatia tuhuma za kuhusika mauaji ya Asimwe Novath

JOHNGERVAS

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2016
Posts
1,011
Reaction score
1,681
mwananchi.png
Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha kutoa huduma za kichungaji Padri, Elipidius Rwegoshora kufuatia tuhuma zinazomkabili za kuhusika katika mauaji ya mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, Asimwe Novart.

Askofu wa Jimbo Katoliki Bukoba, Jovitus Mwijage ametangaza uamuzi huo kupitia gazeti la Kiongozi linalotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), toleo lake la Juni 21 -27, 2024

Gazeti hilo limemnukuu Askofu Mwijage akikiri kuwa mtuhumiwa ni padri wa jimbo lake na amemsimamisha kutoa huduma zote za kichungaji mpaka hapo suala lake litakaposhughulikiwa na vyombo vya sheria.

“Tunahuzunishwa na taarifa ya mauaji ya Asimwe, kwani sisi kama Kanisa Katoliki ni walinzi wa kwanza wa uhai wa wanadamu. Tunaiombea familia yake na kuiombea roho yake ipate pumzio la amani mbinguni.

“Hata hivyo, tumesikia taarifa ya watuhumiwa na mmojawapo akiwa ni Padri Rwegoshora. Ni kweli padri huyo ni wa jimbo Katoliki Bukoba na tumechua uamuazi wa kumsimamisha kutoa huduma zote za kichugaji mpaka hapo suala lake litakaposhughulikiwa na vyombo vya sheria.

“Baada ya vyombo vya sheria kumaliza kazi yake, ndipo taratibu nyingine za kanisa zitafuata,” amesema Askofu Mwijage.

Asimwe menye umri wa miaka miwili na nusu alinyakuliwa mikononi mwa mama yake na watu wasiojulikana Mei 30, 2024 katika Kijiji cha Bulamula, Muleba mkoani Kagera.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma
 
Padre kufikia hatua hiyo ina maana kuna shida kwenye udahili wa hawa viongozi wa KANISA, watu wanaingia upadre bila wito bali shida za familia zao ndio zinawapeleka kanisani kwa imani ya maisha mazuri.
 
Hawa ndo wale usipoenda kwenye jumuiya na kutoa michango wanatoa povu kama lote,,,,halafu mwisho wa siku wanachokutishia ni misa siku ukifa,,,,kudadeki kama kufa kwenyewe ndo unakuja kufanyiwa misa na paroko kama huyu bora tu tusielewane kila mtu aendelee na formula zake,,,,,,,kanisani tunakuja na sadaka tunatoa ile tu ya kwenye misa mengine kila mtu na 50 zake
 
Padre kufikia hatua hiyo ina maana kuna shida kwenye udahili wa hawa viongozi wa KANISA, watu wanaingia upadre bila wito bali shida za familia zao ndio zinawapeleka kanisani kwa imani ya maisha mazuri.
Mungu yupo ndani mwako,,,,kwenye hizi dini ndo walozi wengi wamejificha humo,,,,,na wanacheza sana na saikolojia za waumini wao, ukienda kichwakichwa unachezea ndoige za kutosha
 
Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha kutoa huduma za kichungaji Padri, Elipidius Rwegoshora kufuatia tuhuma zinazomkabili za kuhusika katika mauaji ya mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, Asimwe Novart.

Askofu wa Jimbo Katoliki Bukoba, Jovitus Mwijage ametangaza uamuzi huo kupitia gazeti la Kiongozi linalotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), toleo lake la Juni 21 -27, 2024

Gazeti hilo limemnukuu Askofu Mwijage akikiri kuwa mtuhumiwa ni padri wa jimbo lake na amemsimamisha kutoa huduma zote za kichungaji mpaka hapo suala lake litakaposhughulikiwa na vyombo vya sheria.

“Tunahuzunishwa na taarifa ya mauaji ya Asimwe, kwani sisi kama Kanisa Katoliki ni walinzi wa kwanza wa uhai wa wanadamu. Tunaiombea familia yake na kuiombea roho yake ipate pumzio la amani mbinguni.

“Hata hivyo, tumesikia taarifa ya watuhumiwa na mmojawapo akiwa ni Padri Rwegoshora. Ni kweli padri huyo ni wa jimbo Katoliki Bukoba na tumechua uamuazi wa kumsimamisha kutoa huduma zote za kichugaji mpaka hapo suala lake litakaposhughulikiwa na vyombo vya sheria.

“Baada ya vyombo vya sheria kumaliza kazi yake, ndipo taratibu nyingine za kanisa zitafuata,” amesema Askofu Mwijage.

Asimwe menye umri wa miaka miwili na nusu alinyakuliwa mikononi mwa mama yake na watu wasiojulikana Mei 30, 2024 katika Kijiji cha Bulamula, Muleba mkoani Kagera.
wamefanya maamuzi mazuri sana.
maana kalichafua kanisa sn.
mauaji ya mtoto albino yanasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom