Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha Padre Rwegoshora kufuatia tuhuma za kuhusika mauaji ya Asimwe Novath

Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha Padre Rwegoshora kufuatia tuhuma za kuhusika mauaji ya Asimwe Novath

Mungu yupo ndani mwako,,,,kwenye hizi dini ndo walozi wengi wamejificha humo,,,,,na wanacheza sana na saikolojia za waumini wao, ukienda kichwakichwa unachezea ndoige za kutosha
Chifu kuna vitu mtu anaweza akateleza hili la huyu Padre limevuka mipaka yote yaani kwa jinsi wanavyodahili nashindwa hata kuelewa ilikuaje
 
Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha kutoa huduma za kichungaji Padri, Elipidius Rwegoshora kufuatia tuhuma zinazomkabili za kuhusika katika mauaji ya mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, Asimwe Novart.

Askofu wa Jimbo Katoliki Bukoba, Jovitus Mwijage ametangaza uamuzi huo kupitia gazeti la Kiongozi linalotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), toleo lake la Juni 21 -27, 2024

Gazeti hilo limemnukuu Askofu Mwijage akikiri kuwa mtuhumiwa ni padri wa jimbo lake na amemsimamisha kutoa huduma zote za kichungaji mpaka hapo suala lake litakaposhughulikiwa na vyombo vya sheria.

“Tunahuzunishwa na taarifa ya mauaji ya Asimwe, kwani sisi kama Kanisa Katoliki ni walinzi wa kwanza wa uhai wa wanadamu. Tunaiombea familia yake na kuiombea roho yake ipate pumzio la amani mbinguni.

“Hata hivyo, tumesikia taarifa ya watuhumiwa na mmojawapo akiwa ni Padri Rwegoshora. Ni kweli padri huyo ni wa jimbo Katoliki Bukoba na tumechua uamuazi wa kumsimamisha kutoa huduma zote za kichugaji mpaka hapo suala lake litakaposhughulikiwa na vyombo vya sheria.

“Baada ya vyombo vya sheria kumaliza kazi yake, ndipo taratibu nyingine za kanisa zitafuata,” amesema Askofu Mwijage.

Asimwe menye umri wa miaka miwili na nusu alinyakuliwa mikononi mwa mama yake na watu wasiojulikana Mei 30, 2024 katika Kijiji cha Bulamula, Muleba mkoani Kagera.

Interesting. Nataka kujua imetokeaje huyu jamaa akasoma na kumaliza masomo ya upadre, mpaka akapewa daraja la upadre. Ushirikina wake haukouonekana?
Je malezi ya seminary yamebadilika? Liberation theology is damaging the curch, left and right. Kweli kanisa limeoza
 
Back
Top Bottom