Kanisa Katoliki latoa taarifa ya "kutoonekana" kwa Padre Camillus Nikata wa Jimbo Kuu la Songea

Kanisa Katoliki latoa taarifa ya "kutoonekana" kwa Padre Camillus Nikata wa Jimbo Kuu la Songea

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
TAARIFA YA KUTOONEKANA KWA PADRE CAMILLUS NIKATA​

Kwa niaba ya wanajimbo Kuu la Songea tunapenda kutoa taarifa kwamba Mheshimiwa Padre Camillus Nikata wa Jimbo Kuu la Songea, ambaye ni Mhadhili katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT), Mwanza, haonekani wala hapatikani kwenye simu yake.

Padre Nikata alikuwa ametokea Dodoma kwenye mafundisho ya moyo ya mapadre wanaofundisha katika Vyuo vikuu vya TEC, akiwa na mhadhili mwenzake, ambaye ni Padre wa Jimbo hili. Hapa Songea alikaa katika nyumba ya mapadre, St. Vianney. Alikuwa amepanga kusafiri kwenda Mwanza tarehe 08 Oktoba 2025, siku ya Jumatano asubuhi, kwa basi la SUPERFEO, na tiketi alishainunua kwa mtandao. Lakini siku hiyo ya Jumatano mchana tulianza kuhisi kwamba hajasafiri kwenda Mwanza kwani katika chumba chake kilichokuwa kimefungwa ilionekana mizigo yake ambayo alikuwa ameiandaa kwa ajili ya safari. Mtumishi wa nyumba ya mapadre alishangaa kwamba mzigo ambao Padre ilitakiwa auchukue toka kwake haukuchukuliwa. Pia mlango wa chumba ulifungwa, lakini ufunguo haukurudishwa kwa mtumishi.

Baada ya kuona hayo tulianza kumtafuta kwa simu na kwa kuulizia kwa watu aliokaa nao katika nyumba ya mapadre. Hata hivyo hatukufaulu kupata chochote, maana hakupatikana kwa simu na watu hawakujua alikokwenda. Kule Mwanza alikotakiwa kwenda, nako haonekani na hapatikani. Ofisi ya SUPERFEO ilidhihirisha kuwa Padre Nikata alinunua tiketi lakini hakusafiri kwa basi lile.

Baada ya kushindikana kwa jitihada za kumtafuta kila mahali ambapo tulidhani angeweza kuwepo, tumepeleka taarifa Polisi.

Mhashamu Sana Damian Dallu
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea
.
1760090463253.png

G24_pyqWQAAm0Gx.jpeg
 
Tumsifu Yesu Kristu.

Je siku za karibuni alihubiri kuhusu haki dhdi ya madhalimu? Kama ndio basi atakua ametekwa ...au Ile barua ya mcherengwa ya list ya viongozi wote wa dini ambao hawako na serikali washuhulikiwe alikuwamo na yeye...
 
Ukipita mitandaoni kama facebook kwenye magroup ya kidini hususani magroup ya akina Mudi, utakutana na posts nyingi sana watu wakisema kuwa viongozi wa dini hasa wa kiKatoliki wako kwenye vita na raisi muislamu, yaani karibu wote wana amini hivyo...

...na kuna wengine wanaenda mbali kabisa na kutamka wazi kuwa wako tayari kumsaidia raisi(Samia) kupambana kwenye vita hii, na hawatakubali kuona serikali yake ikianguka.. yaan kwa maana fupi tu wako tayari kupambana na viongozi hao wa dini ambao kwa perceptions zao hawamtaki Samia.

Sasa nikikutana na taarifa kama hii, naanza kupata mashaka yawezekana wenzetu wameshaanza utekelezaji wa kile wanachokisema kwenye magroup yao.
 
Kutekwa tekwa hii style mpaka lini?
watu wanapotea daily hii hali itaisha lini?
 
Yaani mtu asionekane halafu Polisi saa hiyo hiyo wajue alipo?Uchunguzi huwa unafanyika kwanini?Kuna Padri alitoweka mkapiga kelele hivi hivi kumbe alitapeliwa na kukumbwa na depression. Bakizeni akiba ya maneno wacheni kukimbilia kulaumu bila kuwa facts zote.
Hii ndio nafasi nahamia kwa mchepuko sababu ninanzo nazima simu kila kitu napiga mwezi mzima kule, nikija kurudi sababu ipo.....
 
Back
Top Bottom