Kanisa katoliki lijitafakari

Kwahiyo naye papa ameubariki huu waraka ?
 
Hapa tunapingana na kilichosemwa na rais wa TEC. Mimi kama mkatoliki napingana naye pamoja na viongozi wengine kama yeye na nitaanza kulisema kuanzia ngazi ya jumuia na nitahakikisha kulifikisha ngazi ya juu. Kuitwa askofu hakukufanyi kuwa malaika
Mimi kama Mkatoliki imeniuma sana kuona Rais wa TEC anatetea ubarudhuli kama huu. Ikumbukwe Rais wa TEC ndiye msemaji wa kanisa kwa hiyo anapokuja kutoa neno inatakiwa afikirie sana. Sipendi kuongelea udini na ukabila ila Nyaisonga kama Msukuma alitakiwa mapenzi yake hayafiche na ajue waumini wake wanafuata itikadi tofauti. Amenikwaza sana hata jana nikamuomba Mungu wangu nyumbani badala ya kwenda kanisani
 
Napendekeza yafanyike mapinduzi ya TEC, huyu Askofu Nyaisonga siyo sawa kabisa, huyu ni kibaraka wa Serikali kwa 100%.
Hatujazoea TEC kuwa na msimamo baridi namna hiyo ingawa tumezowea kuona msimamo binafsi ya Askofu mmoja mmoja dhidi ya Serikali.

Kama TEC inayumba kutoka msimamo wa mwaka 2017 ikiwa chini ya Askofu Ngalelikumtwa wa Iringa basi Wakatoliki tumeingia choo cha kike na hatutoki humo nguo mpaka 2023 baada ya uchaguzi mwingine wa Rais wa TEC. Vitendo vinavyofanywa na awamu ya Meko ni vya kukemewa na kila mcha Mungu. Kweli TEC inahimiza twende tukapige kura tarehe 24/ 11 kwenye haya mazingira ya ukandamizaji wa wazi wa demokrasia namna hii?? Ina maana hawajaona wala kusikia ? Je walitoa kauli gani walipoambiwa 90% ya wagombea wa upinzani wameenguliwa kwa sababu za kijinga?

Ni wakati sasa Baraza la Maaakofu wa Tanzania (TEC) lijitathmini kama liko sahihi kuongoza roho za waumini wao wapatao 10 Milioni. Otherwise wakae kimya tu.

Tunashindwa hata na wa morovian walio na wafuasi 500 nchini?

Big up Dr Shoo kwa kutoa msimamo ya wana KKKT wapatao 6 Milion nchini. Umebaki ndiyo mtetezi wa Wakristu wote kwa sasa.
 
Inaonekana hujui historia na nia ovu ya hilo kanisa, ni bora ukae kimya!!
 
Sasa unashindwa kujua nini? Inamaana msimamo wa TEC ndio msimamo wa makanisa katoliki nchini. Sasa mmekubaliana huko kanisani kwamba mtashiriki uchaguzi halafu mnakuja kutuhadaa huku mitandaoni kwamba mnayapinga maamuzi yenu ya kanisani.
Mi msabato ila kuanzia jumapili hii nahamia kanisa imara na haki kanisa Katoriki
 
Bora ukasali chini ya mti kuliko kusalishwa ndani ya kanisa na Nyaisonga na Yule paroko wa osterbay, wameamua kushirikiana na shetani waziwazi.
nahisi hao wote ni watu kanda maalum(kabda ya ziwa).
 
Kanisa Katoliki libabaishwe na vitisho uchwara kama vyako! Eti waumini watagoma? Hulijui Kanisa Katoliki na waumini wake weweee! Bora ungekaa kimya!
 
Unachoongea hueleweki labda ungesoma nilichoandika badala ya kudandia train mbele
 
Madhehebu mengine yamesemaje?
 

Acheni unafki na ushabiki wa kijinga na ndio maana mnakosa kuwa na sera za kiuongozi. Mnaacha kumbadilisha mbowe wenu ili aje na sera zingine mnaanzisha mambo ya hovyo

Mlitaka wawaunge mkono kwa upumbavu wenu mliofanya kwanza pale hakuzungumzia ccm bali aliwahimiza watu wakapige kura ili wapate kiongozi makini na nyie mmejitoasasa yy Anatatizo gani embu mtuachie dini yetu sie.

Anzeni kupambana na vyama vyenu changa na sio kupambana na chama kongwe hamtokaa kamwe kututawala
 
Hii ni aibu kubwa sana kwa kanisa
 
Kanisa Katoliki libabaishwe na vitisho uchwara kama vyako! Eti waumini watagoma? Hulijui Kanisa Katoliki na waumini wake weweee! Bora ungekaa kimya!
Jayo ni maoni yako, ni vizuri ume share na mimi nina kushauri uyatunze.
 
Unachoongea hueleweki labda ungesoma nilichoandika badala ya kudandia train mbele
Mwananchi tafadhari acha jazba soma unielewe. Ninachomaanisha kanisa katoriki wameridhia kushiriki uchaguzi ( na wewe ukiwepo), baada ya kuridhia huko kanisani mkatuma msemaji wa kanisa atutangazie sisi kuwa mmekubaliana mkapige kura. Sasa mnapojifanya mnapinaga wakati mliadhimia huko kanisani ni kipi? Au kutuhadaa sisi makamanda wa kilutheri?
 
Kanisa Katoliki linaloshutumiwa leo ndiyo lile lile lililokwamisha katiba ya Sitta. Ndiyo lile lile ambalo askofu wake mmoja alinukuliwa akiendelea kuwakumbusha watawala umuhimu wa katiba mpya na baadaye huyo askofu kupokonywa passport yake. Ndilo hilo hilo ambapo tunasikia katibu wake wa TEC kalazimishwa kuachia madaraka aliyokuwa nayo katika mazingira yale yale yanavyotumika kuwanyamazisha watu wenye mawazo tofauti na watawala. Ni kanisa hili hili lilitoa waraka wa kwaresima 2017 na kuwafanya watawala kununa vibaya. Kisha akajitokeza askofu mmoja kuvujisha makusudi kuwa hakushiriki kwenye kuandika huo waraka ingawa jina lake limejumuishwa! Kwa kifupi kanisa kama taasisi halina shida kubwa bali viongozi waliopewa dhamana ndiyo wenye shida. Baadhi ya viongozi wamekuwa compromised na kibaya zaidi ni kuwa wanatumiwa kisiasa. Kuna uwezekano kabisa kuwa kauli zinazotolewa hazina baraka za kanisa bali viongozi wanajiwakilisha wenyewe.
 
Ushuzi alioutamka the so called Askofu ni kinywa cha RC, hivyo ni msomamo wa RC, tofautisha na mtu kusema kama yeye!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…