Kanisa katoliki lijitafakari

Kanisa katoliki lijitafakari

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Kama kweli kanisa halijawa compromised lijitafakari Ni Mara nyingi kanisa limeteleza haijaanza Leo.

Kanisa likishawahi kuuwa wanasasansi nadhani alikuwa Galileo au Corpenicus sikumbuki vema kisa aliamini kinyume na kanisa kwamba dunia ilikuwa duara.

Kanisa katoliki Tanzania kama kweli dhamira yenu inaongozwa na Roho Mtakatifu basi mjitafakari mara mbili juu ya uamuzi wenu wa kufumbia macho uhalifu uliofanywa na serikali kwenye zoezi la uandikishaji uchaguzi wa serikali za mitaa.

Uhusiano binafsi unaotajwatajwa humu kati ya nyaisonga na magufuli hauna afya kwa kanisa hata kidogo na mtakuwa sehemu ya lawama Mambo yakiharibika.

Mwisho mjitafakari kama bado mna moral authority na credibility ya kula sadaka za waumini wenu wakati mnafumbia macho wanasiasa wanaobaka demokrasia yao?
 
Kanisa limepata viongozi wa hovyo kabisa kupata kutokea, huyo Nyaisonga badala ya kuongea vitu ambavyo vitaliweka taifa pamoja yeye anakwenda kuongea vitu vinavyoleta mipasuko katika taifa.

Nguvu ya Kanisa inatokana na waumini wake sasa subiri waone watakavyobaki peke yao, kumbe kelele zote zile za wakati wa Kikwete zilisikika sababu ya uungwana na upole wake, sasa hivi chuma kinaongoza nchi Kanisa limeukana wajibu wake mara tatu kabla Jogoo halijawika, kama kulikuwa na jambo la kukaa na kusuluhisha basi kanisa ndiyo lilipaxwa kuziita pande mbili hizo ili kusuluhisha badala ya kuutaka upinzani unaoonewa eti uitishe suluhu.

Kumbe Tundu Lissu yupo imara zaidi ya kanisa? Mbowe ambaye anayepitia misukosuko mingi ya kuwekwa ndani, kuharibiwa mali zake, kunyang'anywa mali zake kumbe yupo imara kuliko viongozi wa Kanisa ambao wao wanajali hadhi zao tu na si hadhi ya Kanisa
 
Kanisa katoliki lina historia ya kushabikia ukatili na kujikomba na serikali dhalimu!

Mkililaumu kanisa mnalikosea heshima bure, wakulaumiwa ni Mbowe. Mbowe amecheza mchezo wa kitoto sana amehamisha magori mchana kweupe. Mbowe hataki kutoka madarakani ameamua kutumia uchaguzi wa serikali za mitaa kuwa ndio ngao yake, yaani Mbowe yupo pembeni tu anawazoom jinsi mnavyomfagilia njia yake ya ufalme chamani
 
Hukumbuki hao watu waliouliwa na Kanisa Katoliki na hata kisa kilichofanya wauwawe pia hukikumbuki lakini umepata guts za kusema Kanisa limeuwa! Is that fair Mkuu? Kwa maoni yangu umepotoka

Tanzania kuna madhehebu kadhaa ya dini na madhehebu yenye waumini wengi ni Kanisa Katoliki na Waislamu. Inakuaje umechagua kutoa maneno makali dhidi ya Taasisi moja tena angalau yenye historia ya kukemea maovu huko nyuma lakini hukugusia taasisi kama BAKWATA ambao sio tu wapo kimya lakini huunga mkono jambo lolote la Wanasiasa wa Chama Tawala liwe baya na ovu kwa watu au vinginevyo?
 
Hapana mkuu..ukiacha udini jamaa ana point!ww unataka kuanza kuleta udini..usiitaje kwanza bakwata hapa..maana inajulikana ni mali yao..unakimbuka zaman walikua waantoa waraka kbs kukemea ntantalila za serikali!?ss hv wamelewa sadaka za waamini!
 
Po

Point zangu ni mbili manengelo. Unapotoa madai serious ya kwamba mtu au taasisi imewahi kuua watu lazima uwe precise and certain. Huyu jamaa eti hakumbuki! Sasa kwanini akaandika hoja hiyo?

Pili hizi taasisi za dini zinakua na maslahi yao kwa serikali iliyopo madarakani na kamwe haziwezi kwenda kinyume na serikali hizo ikiwa maslahi yao kama taasisi yanaangaliwa. Kama huko nyuma yaliwahi kufanya hivyo basi ujue maslahi ya taasisi husika yalikua hatarini. Chunguza
 
Nadhan ungespecify kbs kuwa RC wako kimaslah na serikali..huu ujinga ujinga huukuti kwa Wasabato hata siku moja!hakuna siasa kbs kule!bure kabisa RC
 
Hapa tunapingana na kilichosemwa na rais wa TEC. Mimi kama mkatoliki napingana naye pamoja na viongozi wengine kama yeye na nitaanza kulisema kuanzia ngazi ya jumuia na nitahakikisha kulifikisha ngazi ya juu. Kuitwa askofu hakukufanyi kuwa malaika
 
Ili kanisa watu wake ni wakimya cjui tupoje
Hakuna nafasi ya kondoo kuhoji mchungaji. Mchungaji anamwakilisha Mungu. Hakuna kuhoji wala kupinga. Hakuna kujenga hoja. Ni kusikiliza tu na kuishi kadiri ya mafundisho.
 
Back
Top Bottom