GE2025 Kanisa Katoliki: Marufuku kwa watawa kujihusisha na kampeni za siasa

GE2025 Kanisa Katoliki: Marufuku kwa watawa kujihusisha na kampeni za siasa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Kanisa katoliki nchini limeweka marufuku kwa watawa wa kike na kiume na kiongozi yeyote wa kanisa katoliki kujihusisha na kampeni za siasa au kutambulishwa na chama chochote cha kisiasa kama mshirika wao. Na kukumbushwa kwamba jukumu lao ni kuinjilisha kadiri ya wito wao

1758801702594.jpeg

Katazo hilo limetolewa Septemba 25, 2025 na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi Mhashamu Wolfgang Pisa O.F.MCap. wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya kilele cha jubilee ya miaka 100 ya seminari kuu ya Mt. Paulo Mtume Kipalala Jimbo Kuu Katoliki la Tabora.

Askofu Pisa amesema kuwa haitaruhusiwa kwa mtawa yeyote au mseminari katika mazingira yeyote yale atakayeruhusiwa kujihusisha na jambo lolote lenye taswira ya kisiasa hata kama mtawa angekuwa na ndugu mwenye kujihusisha na siasa.

Pia soma: Watawa Katoliki Lindi: Tunamuunga Mkono Rais Samia, Tunamuombea Miaka 5 tena




​
 
channeltentanzania_1758712652_3728674438636943695_45981184722.webp

Hawa Masista walizingua, huyu bibi anahangaika sana kujitia anakubalika na kanisa katoliki lakini ukweli ni kwamba kajiharibia..
Hata hii picha ukiangalia hawa masista wamefanya hivyo kwa maelekezo ili kusudi kuonyesha wananchi Chura kiziwi hana tatizo na RC...
Askofu ametisha.. piga marufuku hao kukaribisha siasa zao za kishenzi..
Bibi anahangaika sana...
 
View attachment 3478647
Hawa Masista walizingua, huyu bibi anahangaika sana kujitia anakubalika na kanisa katoliki lakini ukweli ni kwamba kajiharibia..
Hata hii picha ukiangalia hawa masista wamefanya hivyo kwa maelekezo ili kusudi kuonyesha wananchi Chura kiziwi hana tatizo na RC...

Bibi anahangaika sana...
Masista wafute kauli yao ya kuunga mkono au waondolewe kwenye utawa wakavae vitenge vya samia mitano tena.

Katoliki hawashiriki uchaguzi mpaka itakapotangazwa vinginevyo huko baadaye.
 
Masista wafute kauli yao ya kuunga mkono au waondolewe kwenye utawa wakavae bitenge vya samia mitano tena.

Katoliki hawashiriki uchaguzi mpaka itakapotangazwa vinginevyo huko baadaye.
Kabisa, hao masista watolewe.. ili iwe fundisho...
Lakini huyo Askofu ametisha sana...
Atokee mwingine tena akemee vikali..
 
Masista wafute kauli yao ya kuunga mkono au waondolewe kwenye utawa wakavae bitenge vya samia mitano tena.

Katoliki hawashiriki uchaguzi mpaka itakapotangazwa vinginevyo huko baadaye.
Naunga mkono hoja
 
Kabisa, hao masista watolewe.. ili iwe fundisho...
Lakini huyo Askofu ametisha sana...
Atokee mwingine tena akemee vikali..
Kila askofu ana jimbo lake, hao wako kwenye imaya yake yeye ndiye askofu wa jimbo hilo.

Wengine hayajawatokea labda.

Ila kule Tabora niliona kardinali anajihusisha na siasa TEC hawakusema kitu, nitawakumbusha.

Kardinali hakupaswa hata kumsogelea mgombea wa ccm, lakini alikiuka agizo la TEC, alipotiwe kwa papa afukuzwe au apigwe mapumziko ya miaka 5.

TEC wanashindwa kutamka WAKATOLIKI MSIPIGE KURA october 29.

Lakini huo ndio ujumbe hasa.

Sio tu kwa watawa na waseminary hata waumini wote Tanzania.
 
Kila askofu ana jimbo lake, hao wako kwwnye imaya yake yeye ndiye askofu wa jimbo hilo.
Wengine hayajawatokea labda.
Ila kule Tabora niliona kardinali anajihusisha na siasa TEC hawakusema kitu, nitawakumbusha.

Kardinali hakupaswa hata kumsogelea mgombea wa ccm, lakini alikiuka agizo la TEC, alipotiwe kwa papa afukuzwe au apigwe mapumziko ya miaka 5.

TEC wanashindwa kutamka WAKATOLIKI MSIPIGE KURA october 29. Lakini huo ndio ujumbe hasa.
Sio tu kwa watawa na waseminary hata waumini wote Tanzania.
Hakika...
 
Back
Top Bottom