Kanisa Katoliki mnataka kutuharibia nchi?

Kanisa Katoliki mnataka kutuharibia nchi?

Mkuu mleta uzi unaonekana una bifu binafsi na kanisa katoliki kwa sababu yoyote unayoijua ww. Karibu kila dhehebu ama dini viongozi wa kisiasa hupewa nafasi ya kuwasalimia waumin na huzungumza mambo mbalimbali yakiweyo yanayoleta uchochezi, chuki na ubaguzi. Kama ni mfuatiliaji mzur kabla ya uchaguz lowasa alinukuliwa ktk kanisa moja la KKKT akihimiza achaguliwe eti kwa sababu hakujawahi tokea rais mlutheri .mbona hukutokwa na povu kama leo?, Anyway kanisa katoliki lianzaje kukemea serikali eti haijapandisha wafanyakazi madaraja mara hawajalipwa posho are you serious? Ina maana kanisa ligeuke kuwa chama cha wafanyakazi? Kazi ya vyama vya wafanyakazi ni zipi?. Mkuu kwa povu hilo dhidi ya kanisa katoliki "kunywa maji ulale tu hamna jinsi"
 
hahahahahah nlipark mahali jan kurudi nakuta kwa bonet wameweka mitumba uliza kijana parking hapa umepanga juu ya gari anasema tumeambiwa tupange kote penye nafasi nlicheka sanaa nikamwomba aondoe tukaachana ivo yani
 
Hiki kitabia kikianza na kufumbiwa macho wasije wakaanza kutafuta mchawi. Siwezi kusahau jinsi Mwembe Chai ilivyopigwa mabomu kisa kuchanganya dini na siasa. Naona labda Mheshimiwa amejisahau na kwa kuwa yuko juu ya sheria hakuna anayemkumbusha, wakianza wengine kutumia madhabahu asije kulalamika na kuwachukulia hatua zisizostahiki.
 
Mi naona walutheri ,wapentecostal ,anglicana,sabato,menonite,na huduma zote nao waamue tu kupiga siasa na kumpigia debe mwenzao maana hawa kina pengo sasa wamezidi kumpa promo mtu wao maana sasa roman catholic church limekuwa julwaa la siasa bora makanisa yote yapige siasa tu
 
Maneno yako sawia maana haya yangefanyika misikitini ingekuwa kelele sana ni vyema nyumba za ibada zikawekwa mbali na siasa
yangefanyikaa msikitinii washauriwaa watu zamani mabomu yangesharushwaa kumbuka mwembechai magomeni libumbaa kilichomkutaa akawakimbiaa wakaendaa kumvunja mikono mbagala
 
Sioni kama kanisa linashida, utaratibu wake ni ule ule!
Shida ipo kwa hawa wanasiasa, mfano huyu Bwana yule amekuwa mtu wa kutopangiwa kitu cha kuongea, hata akiambiwa hapa hupaswi kusema hivi yeye ng'o atalipuka tu na yale anayoyataka yeye ili apate sifa...
Wanasiasa ndio wenye matatizo!!
 
Unataka nchi iharibike mara ngapi! Viongozi wa dini ni wachumia tumbo tu hawana lolote. Ni wasabato pekee ndio hawaruhusu ujinga huo makanisani kwao kwa sababu hawategemei misaada ya serikali na wanasiasa kuendesha mambo yao
Acha uongo nanii..!!
 
Umesema kweli lakini nawe umetoka nje ya majukumu ya kanisa mambo hayo hayawausu yanayowahusu mi kuimiza upendo,upendo wa kweli kwa muumba,kukemea mambo yanayotofautisha watu kwenye jamii,elimu iliyobora na kuwatia Moyo viongozi wawe na hofu ya mungu tuuuuuuuu.
 
Habari wanabodi..

Awali ya yote ninaomba niwapongeze wale wote ambao wamefanikiwa kuuona mwaka mpya wa 2017.

Pili nawapa pole wale wote ambao wameanza mwaka kwa matatizo mbalimbali. Ninaamini MUNGU atawapa Faraja.

NAOMBA NIJIKITE KWENYE MADA.

Labda nianze kueleza taratibu za Kanisa Katoliki katika ibada zake.

Kanisa Katoliki lina sehemu kuu mbili za katika Ibada;
1. Liturjia ya Neno
2. Liturjia ya Ekaristi

Sehemu hizo zote mbili hazimruhusu mtu kusema neno lolote lililo nje ya utaratibu wa Kikanisa. Hata wakati wa matangazo hutakiwi kutangaza jambo ambalo Kiongozi Mkuu (Paroko au Askofu) halifahamu.

Pia Kanisa halina utaratibu wa kuruhusu mambo ya SIASA ndani ya Kanisa bali hutoa msimamo usiofungamana na upande wowote ili kutoadhiri msimamo wa Waumini. Japo linaruhusu KUKOSOA na KUPONGEZA PIA.

WAPI KANISA LINATAKA KUTUHARIBIA NCHI?

1. Kuruhusu hotuba za Kisiasa ndani ya Kanisa. Hili nionavyo mimi litaharibu Nchi. Wanasiasa wanayo majukwaa yao ya kuzungumzia mambo yao ya siasa na siyo Kanisani. Siku za hivi karibuni Kanisa Katoliki limekuwa likiwaruhusu wanasiasa kusimama Madhabauni na kutoa hutoba zao za Kiserikali na Kisiasa ama kwa kujibu hoja fulani au kutoa matamko ama kusambaza Kauli Mbiu fulani, (tafsiri yangu ya haraka hapa ni kwamba wanasiasa wanahitaji "mass support" hata kama wanafanya jambo baya). Kwa hili Kanisa halitendi haki maana viongozi wa Nchi hii ni wetu sote. Kama viongozi wetu wanahitaji kujibu hoja, kutoa matamko au kusambaza kauli mbio wasitumie NYUMBA ZA IBADA.

KANISA KATOLIKI WAPENI WATU NAFASI KANISANI YA KUSALIMIA TU NA KUSISITIJA JUU YA AMANI, UPENDO, MSHIKAMANO NA UWAJIBIKAJI NA SIYO VINGINEVYO.

2. Matamko ya viongozi wa Kanisa Katoliki. Hawa viongozi ni lazima wajikite kwenye ukweli na siyo kujipendekeza. Nyakati hizi viongozi wa Kanisa Katoliki wamekuwa ni watu wa kupongeza tu bila kukosoa ukilinganisha na nyakati za nyuma.

a. Mmepongeza yale mazuri = VEMA.

b. Kwa nini hamkosoi na kusema ukweli juu ya mambo ambayo Serikali inakosea au hata kuhoji tu?. Mfano sijasikia mkikosoa au kuhoji juu ya,
i. Ukiukwaji wa Katiba na Sheria za nchi.

ii. Matumizi ya fedha za wahanga wa Kagera.

iii. Nyongeza ya mishahara ambayo ni haki ya mfanyakazi.

iv. nk

KANISA KATOLIKI MKIENDELEA HIVI MTATUHARIBIA NCHI YETU.

Nawasilisha.
Mkuu umenena vyema, kwanza mi nilijuavyo hili kanisa hata hiyo nafasi ya mtu kusalimia kanisani pia ni geni. Ndani ya kanisa ni ibada tu, nimekulia ukatoliki naujua vyema.

Hakuna mazungumzo nje ya ibada kanisani. Labda ndo mabadiliko haya, siku hizi hata wanacheza mdumange kanisani. Mkuu, umewapa ushauri mzuri sana. Nilijuavyo hili kanisa, liko smart litajirudi.
 
Sioni kama kanisa linashida, utaratibu wake ni ule ule!
Shida ipo kwa hawa wanasiasa, mfano huyu Bwana yule amekuwa mtu wa kutopangiwa kitu cha kuongea, hata akiambiwa hapa hupaswi kusema hivi yeye ng'o atalipuka tu na yale anayoyataka yeye ili apate sifa...
Wanasiasa ndio wenye matatizo!!
Hapana, hujamuelewa mtoa mada. Kanisani kwa wakatoliki ni mahali patakatifu hakuna mazungumzo mengine nje ya ibada. Mazungumzo pekee yaliyo nje ya mfumo wa kiibada ni tafsiri ya masomo, anaitoa padri, na matangazo tu. Nje ya hayo, mengine yote hunenwa sawa dunia nzima.

Nje ya wasomaji wa masomo, padri na mtangaza matangazo. Mimbari ya kanisa hakuna apaswaye kunena jambo hapo.
Acha uongo nanii..!!
 
Unataka nchi iharibike mara ngapi! Viongozi wa dini ni wachumia tumbo tu hawana lolote. Ni wasabato pekee ndio hawaruhusu ujinga huo makanisani kwao kwa sababu hawategemei misaada ya serikali na wanasiasa kuendesha mambo yao
Promo only
 
Hapana, hujamuelewa mtoa mada. Kanisani kwa wakatoliki ni mahali patakatifu hakuna mazungumzo mengine nje ya ibada. Mazungumzo pekee yaliyo nje ya mfumo wa kiibada ni tafsiri ya masomo, anaitoa padri, na matangazo tu. Nje ya hayo, mengine yote hunenwa sawa dunia nzima.

Nje ya wasomaji wa masomo, padri na mtangaza matangazo. Mimbari ya kanisa hakuna apaswaye kunena jambo hapo.
Mtoa mada nimemuelewa vyema, pengine wewe ndiye hukunielewa tafsiri yako imekwenda op kwa jinsi nilivyoquote huyo mdau...
 
Back
Top Bottom