Kanisa Katoliki mnataka kutuharibia nchi?

Kanisa Katoliki mnataka kutuharibia nchi?

Unataka nchi iharibike mara ngapi! Viongozi wa dini ni wachumia tumbo tu hawana lolote. Ni wasabato pekee ndio hawaruhusu ujinga huo makanisani kwao kwa sababu hawategemei misaada ya serikali na wanasiasa kuendesha mambo yao

Kijana Rais ni raia ila siyo raia kama wewe kwa dhamana aliyo nayo, rais ni nchi
Mwadhama Cardinal Polycarp Pengo.

Uliza Wakatoliki juu ya hicho cheo watakuelekeza wadhifa alionao Cardinal Pengo.

Niulize wakatoliki gani wakati mwenyewe ni mkatoliki? Pengo ni ASKOFU WA JIMBO KUU LA DSM, JOESPHAT LEBULU NI ASKOFU WA JIMBO KUU LA ARUSHA (Hawa wote wana nafasi sawa). Maaskofu wasidizi mabosi wao ni hao maaskofu wakuu. Hakuna bosi wa maaskofu Tanzania. Hamna askofu mwenye mamlaka kisheria kupitisha jambo na likafanyiwa kazi na wenzake wote ISPOKUWA TEC yenye maaskofu wote. PENGO kuwa kardinali haimpi ubosi kwa maaskofu wengine.
UKITAKA KUJUA JIFUNZE, UKARDINALI INAJITOKEZA TU PALE PANAPOTAKIWA ISSUES ZA KUWAKILISHA KANISA LA TANZANIA KWENYE MAMBO YANAYOAMULIWA HUKO VATICAN.
 
Kwan wale waliopewa nafasi ya kuongea kanisani Roma wakaanza kuponda kuhusu rc mpka wakachapwa viboko walikua wanasiasa? Hujawahi kumuona lipumba akipewa nafasi ya kuwasalimu waumini msikitini? Naona safari hii mmejipanga kulichafua kanisa
 
Asante na mungu akupe maisha marefu mtoa mada...ulichoongea ni ukweli husiopingika kabisa hasa huyu kiongozi wetu Pengo ndo ovyo kabisa hamna kitu,ila mungu atawaumbua tu na ni swala la muda
 
So. Unataka kuniambia hata viongzi wa dini siku hizi wanaongozwa kwa mihemko ya mwwnyekiti wa kitongoji cha wachache?
 
Kwan wale waliopewa nafasi ya kuongea kanisani Roma wakaanza kuponda kuhusu rc mpka wakachapwa viboko walikua wanasiasa? Hujawahi kumuona lipumba akipewa nafasi ya kuwasalimu waumini msikitini? Naona safari hii mmejipanga kulichafua kanisa
Kanisa Katoliki ni Kanisa makini sana, kuiga au kuruhusu mambo yasiyofaa yanayofanywa na Imani zingine si vema.
 
Wanahitaji misaada maana kipindi cha kampein kulikuwepo na kanisa moja la katoliki liliunda kwaya na kuipa jina la Hapa kazi tu.

Mungu tunaomba utupe hekima
 
Asante KWEZISHO,

Hapa najaribu kuepusha migongano ya kidini hapo baadae. Kama mwanasiasa anaona ni muhimu kutoa taarifa zake za kisiasa basi aruhusu mikutano ya siasa au kuwe na press conference au kuwe na hotuba maalumu.
Kwa ujumla ufikapo kanisani au msikitini ile hadhira ina watu tofauti na wenye maono tofauti katika uwanja wa siasa. Ukiingia kanisani au msikitini utakutana na wanachama wa CDM, CCM, CUF, NCCR, TADEA etc. Na wao wamejumika pale kufata ibada na sio siasa, kwa hiyo jambo lolote la kisiasa litawafanya watoke kwenye ibada na kuingia kwenye karaha na kuanza kutengeneza hisia tofauti na kumkaribisha shetani. Kwa ujumla ni kweli kabisa watu wa dini wajiepusha na itikadi za kisiasa.
 
Umenena vema.
 
Sasa tufanyeje kama ni hivyo
Kwa mtazamo wangu hawa tusiwape nafasi ya kuongea mambo yao ya siasa ndani ya nyumba za ibada. Watafute utaratibu wao wa mahali, wakati na jambo la kuongea, lakini si kwenye nyumba za Ibada.
 
Bosi wa Kilaini ni Pengo. Ukiona bosi yupo kimya ina maana
1. Alimpata mgao

au

2. Amekubaliana na hiyo hali
Thibitisha pasipo shaka kuwa bosi wa Kilaini ni Pengo la sivyo hujuujui uongozi wa kanisa Katoliki Mkuu.
 
Thibitisha pasipo shaka kuwa bosi wa Kilaini ni Pengo la sivyo hujuujui uongozi wa kanisa Katoliki Mkuu.
Tofautisha hivi vyeo ndani ya Kanisa Katoliki.

>Mwakilishi wa Papa nchini Tazania

>Cardinali

>Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu

>Askofu wa Jimbo

>Msaidizi wa Askofu

Ukiweza ku-rank hapo utakuwa umenielewa.

Japo lengo langu si hili bali kujikita kwenye TOPIC HUSIKA.

JIKITE KWENYE TOPIC TAFADHALI.
 
Back
Top Bottom