Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,476
2003 INVASION OF IRAQ: Kanisa Katoliki Vatican na ushawishi wake juu ya msamaha kwa Waziri Tariq Aziz. Mkristo kindakindaki na swahiba mkuu (Inner Circle) wa Saddam Hussein.
Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Iraq katika utawala wa Saddam Hussein na mtu wa upande wake wa kulia (right-hand man) ndugu Tariq Aziz (Mikhail Yuhanna kwa jina la kikristo) alishawishi wanahabari pamoja na wanaharakati huko Vatican kupanga mikakati maalum ili apate utetezi na ushauri wa bure wa kisheria kwa makosa yaliyokuwa yanayomkabili ya uhalifu dhidi ya ubinadamu pamoja na uhalifu wa kivita.
Tariq Aziz, Mkristo kindakindaki anayefanya mazoezi ya sala mara kwa mara ambaye alikuwa msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa dikteta wa Iraq, hatimaye alipata huduma za kisheria na mawakili wa Italia baada ya kuwasiliana na kikundi cha makuhani na maaskofu wa kanisa Katoliki kule Vatican.
Aliiandikia familia yake barua kutokea gerezani huko jijini Baghdad akiwahimiza kuwasiliana na Father/Padri Jean-Marie Benjamin, kuhani wa mrengo wa kushoto ambaye hapo awali alikuwa akifanya mkutano wa kidiplomasia uliojaa mabishano na mvutano kati ya Tariq Aziz na Papa kabla ya vita mwaka 2003.
Padre Benjamin, ambaye alisema kuwa anafanya kazi kwa baraka isiyo rasmi ya kutoka Vatikani, sasa anaandaa msaada wa kidini pamoja na wa kisheria kwa Aziz, waziri mkuu wa dikteta wa zamani, ambaye mpaka wakati ule alikuwa bado hajasomewa na kuelewa maelezo kamili ya mashtaka dhidi yake.
Kampeni hiyo pia iliungwa mkono na Monsignor Emmanuel Delly, Mzalendo na mzee wa kuheshimika sana kwa pale Baghdad na kiongozi wa kiroho wa tawi lenye nguvu la waumini wapatao 500,000 wa Kanisa Katoliki ambalo Aziz ndio kanisa lake. Kuhusika kwa kanisa hilo katika utetezi wa bwana Aziz ni jambo lilioonekana kuwa ni la aibu kwa waziri mkuu wa Italia, ndugu Silvio Berlusconi, ambaye serikali yake ya mlengo wa kulia iliunga mkono uvamizi ulioongozwa na Marekani.
Wafuasi wa Aziz wanasema ya kwamba bwana huyu alikuwa ni mwanadiplomasia tu lakini Waingereza na Wamarekani wanaamini kwamba jukumu lake kama muomba msamaha mkuu kwa serikali ya Saddam linamfanya astahili lawama na apatikane na hatia. Father Benjamin, aliyekuwa na umri wa takriban miaka 58 kwa wakati ule, afisa mkuu wa zamani wa shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia watoto (UNICEF), ambalo lilifanya kampeni dhidi ya vikwazo juu ya Iraq, alisema kwamba: "Bwana Aziz alikuwa rafiki yangu na alikuwa mwanadiplomasia, na sio mwanajeshi."
"Aliiomba familia yake kuwasiliana na mimi mwezi Julai uliyopita kwa msaada wa uratibu wa utetezi, na nilipozungumza na maaskofu wangu na wakurugenzi walisema ndio, kwa muktadha wa maadili unayo haki ya kufanya hivyo. Mawakili watakuwa wakifanya kazi bure kwa kuwa familia hiyo inakosa pesa za kulipia utetezi wake."
Vatikani, ambayo ilikataa kutoa maoni juu ya suala hilo, inawahimizaga sana mapadre kutekeleza mipango isiyo rasmi kama njia ya kushughulikia maswala nyeti ya kidiplomasia. Katika wakati huu, baada ya Father Benjamin kuiambia ofisi za Upapa kuhusu mipango yake, alipokea barua ya ruhusa kutoka kwa Kardinali Angelo Sodano, katibu (Waziri wa mambo ya nje) wa serikali ya Vatikani, akimshukuru kwa kazi yake "ya kujenga uhusiano imara baina ya watu wa Iraq na ulimwengu mpana wa Waarabu".
Barua hiyo haikuelezea moja kwa moja kesi ya Aziz lakini Father Benjamin alisema: "Kwa usiri na kimoyomoyo, wanaunga mkono kile tunachofanya." Padri Benjamin alikusanya timu ya mawakili watano wa Italia na wachungaji wenzake, pamoja na Askofu, Diego Bona, rais wa Beato Angelico Foundation, ambayo inakuza uhusiano mwema baina ya Waislam na Wakristo.
Alipokuwa kama mkurugenzi wa taasisi hiyo Father Benjamin aliwahi kumwalika Aziz kukutana na Papa mnamo Februari mwaka wa 2001, na kusababisha ukosoaji mkubwa kwamba Roma/Vatican ilikuwa ikitoa heshima ya kapeti jekundu (Red Carpet Treatment) kwa serikali ya kidikteta ya Iraq.
Licha ya Upinzani wa Papa kupinga vita kwa misingi ya maadili, vikundi vya haki za binadamu vilisisitiza kwamba Vatican haipaswi kumpa nafasi ya kusikilizwa mtu ambaye mikono yake "ilikuwa imechafuka damu ya uhalifu dhidi ya ubinadamu". Mwezi mmoja kabla Father Benjamin na timu yake walisafiri kwenda mji mkuu wa Yordani, Amman na kukutana na mtoto wa Aziz, Ziad. "Father Benjamin anamjua baba yangu vizuri sana na amewaomba mawakili kutoka Italia kumlinda bila malipo," alisema Ziad Aziz. "Amesema pia atapata msaada kutoka kwa uongozi wa Vatikani."
Tariq Aziz, ambaye tabia yake njema na uungwana ilimtofautisha na wakatili wengi wa Saddam, ilikuwa hana mawasiliano kabisa na watu wake wa karibu tangu alipojisalimisha kwa vikosi vya Marekani mwaka ule. Siku pekee ambayo familia yake ilikuwa na nafasi ya kumuona ni wakati yeye na watu wengine 11 wa serikali ya zamani walisimamishwa kizimbani na Saddam katika kesi ya kwanza mahakamani huko jijini Baghdad mnamo mwezi Julai mwaka 2004.
Aliposimama kizimbani aliomba kupewa mwanasheria wa kigeni na alikanusha uwajibikaji wowote, akiiambia mahakama kwamba: "Sijawahi kumuua mtu yeyote kwa kitendo chochote cha moja kwa moja." Tangu wakati huo kulikuwa na ripoti kwamba amekubali kutoa ushahidi dhidi ya Saddam, ingawa mtoto wake amekanusha maoni hayo kuwa hayawezekani.
"Mashtaka dhidi ya Saddam hayahitaji mtu yeyote kutoa ushahidi," alisema Ziad Tariq. "Lakini hatujui kinachoendelea kwa sasa kwa sababu hatujapata barua kutoka kwake tangu Julai. Na hiyo ndio haki mliokuwa mkiitafuta kutoka kwa Wamarekani."
NIMEPATA CHANGAMOTO KIDOGO YA KIFAMILIA. NIKIFIKA IRINGA NITAMALIZIA STORY HII NEXT TIME.....!!!!!!!
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
MMENISUSIA VITABU VYANGU: Ninauza Vitabu Vya Kujifunzia Lugha Ya Kijerumani. Ich komme aus der Stadt Dar Es Salaam und verkaufe diese Deutsch-Lernbücher