MaxShimba
JF-Expert Member
- Apr 11, 2008
- 35,771
- 4,065
Kanisa kumuombea JK dhidi ya mafisadi
Na Peter Mwenda
WAUMINI wa Kanisa Katoliki nchini, leo watakuwa na ibada maalum ya kuombea taifa liendelee kuwa na amani, utulivu na kuitakia mafanikio mema Serikali ya awamu ya nne katika vita dhidi ya ufisadi.
Hayo yapo katika salamu za Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kadinali Policarp Pengo zilizosambazwa katika makanisa yote nchini.
Paroko Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Ukonga, Padre Joseph Kanduta, akitoa ujumbe wa Askofu Pengo kwa waumini wa kigango cha Kitunda alisema Wakatoliki wote watakuwa na ibada leo itakayokuwa maalum kwa ajili ya kuombea amani.
"Askofu Pengo amewataka waumini kuiombea serikali ya Rais Kikwete isikate tamaa kupambana na ufisadi kwa kuwa ni kazi ngumu ambayo inahitaji baraka za mungu kufanikiwa, tufike kwa wingi kuombea utulivu katika kipindi hiki kinachohitaji ujasiri," alisema Padre Kanduta.
Ibada hiyo pia imeapewa kipaumbele na Wanawake Wakatoliki Nchini (WAWATA) Jimbo la Dar es Salaam ambao wameandaa ibada ya kuombea amani kwa kuwaunganisha wanawake wote wa jimbo hilo kusali pamoja katika eneo ambalo huenda kuhiji lililopo karibu na shule ya Sekondari ya Pugu.
Habari kutoka kwa wanawake hao zinasema akina mama hao wataanza ibada hiyo kwa maandamano kutoka Shule ya Sekondari Pugu kuingia kwenye eneo maalum la hija ambapo wanatarajia Askofu Pengo ataongoza ibada hiyo.
Comment in this Story Nakala inayochapika